Trector aina ya Lovol ni bei nafuu sana

Trector aina ya Lovol ni bei nafuu sana

Nyangabo2022

Senior Member
Joined
Nov 13, 2022
Posts
126
Reaction score
195
Wanajamvi Mimi ni mkulima mdogo mwenye shauku kubwa ya kumiliki trector Kwa mwaka huu 2023, nmechoshwa na gharama kubwa ya matrector huko Songea, heka Moja mwaka huu tumelima Kwa TSH 90000 had 100000, hapo hujarudia wakati wa kupanda!

Hiki ni kilimo Cha mpunga! Nmeona sio vibaya nijchange change huku na Kule niwe na mashine ndipo nkakuta Tangazo la hizi trector nkawapgia wakasema mfn trector 75hp na jembe ni km 47mlns pia wanakopesha nikaona nishee na wenzangu kama Kuna yeyote ameshuhudia uchapaji Kazi wake maana ni trector mpya tumezoea new Holland, Massey, swaraj nk ambazo bei ziko juu ukilinganisha na Hizi.

Karibuni.
 
Kama hutojali na kutokana na kazi unayoifanya ya kilimo Cha mpunga ungepata pawatila Siam Kubota. Kwa upande wa trekta usijali kikubwa angalia spea/ vipuli zake zinaingiliana na kampuni gani na upatikanaji wake upoje. Baadhi ya trekta likizingua unageuza kichanja hata Kama unahela, na nyingine huwa zinaharibika Mara Kwa Mara hasa pampu.

Trekta ukinunua Kwa keshi itakua poa Sana kuliko kukopa. Mfano Efta ilikua ukikopa marejesho ni Kila mwezi Kwa miaka mitatu na Kuna vigezo vya shamba na kiingilio lakini ukifeli marejesho hata Kama umebakiza miezi miwili liwe lako wanabeba.

Ukinunua pia utatakiwa kununua majembe na rota na angalau trela kwaajili ya kubebea mizigo wakati wa kiangazi au uwe unakodi.

Kuhusu pawatila utapata Kwa milioni 12 ikiwa complete na Kama ukiwa na pesa za kutosha unaweza kununua mbili. Ukiwa nazo mbili hapo mwenye trekta mnakula league na unaweza kumzidi kidoogo kutokana na wewe kutumia mafuta kidogo na PAWATILA kufanya kazi hata maeneo mapya au yasiyofikika Kwa trekta.

Kwa trekta roho ya paka ni New Holland, masey Ferguson, valtra, Kubota, ford na nyingine nyingi ambazo spa zake zinapatikana.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wanajamvi Mimi ni mkulima mdogo mwenye shauku kubwa ya kumiliki trector Kwa mwaka huu 2023, nmechoshwa na gharama kubwa ya matrector huko songea, heka Moja mwaka huu tumelima Kwa TSH 90000 had 100000, hapo hujarudia wakati wa kupanda! Hiki ni kilimo Cha mpunga! Nmeona sio vibaya nijchange change huku na Kule niwe na mashine ndipo nkakuta Tangazo la hiz trector nkawapgia wakasema mfn trector 75hp na jembe ni km 47mlns pia wanakopesha nikaona nishee na wenzangu km Kuna yeyote ameshuhudia uchapaji Kaz wake maana ni trector mpya tumezoea new Holland, Massey, swaraj nk ambazo bei zko juu ukilinganisha na Hz. Karbun.
Mkuu unalima heka ngapi kwa mfano
 
Kama hutojali na kutokana na kazi unayoifanya ya kilimo Cha mpunga ungepata pawatila Siam Kubota. Kwa upande wa trekta usijali kikubwa angalia spea/ vipuli zake zinaingiliana na kampuni gani na upatikanaji wake upoje. Baadhi ya trekta likizingua unageuza kichanja hata Kama unahela, na nyingine huwa zinaharibika Mara Kwa Mara hasa pampu.

Trekta ukinunua Kwa keshi itakua poa Sana kuliko kukopa. Mfano Efta ilikua ukikopa marejesho ni Kila mwezi Kwa miaka mitatu na Kuna vigezo vya shamba na kiingilio lakini ukifeli marejesho hata Kama umebakiza miezi miwili liwe lako wanabeba.

Ukinunua pia utatakiwa kununua majembe na rota na angalau trela kwaajili ya kubebea mizigo wakati wa kiangazi au uwe unakodi.

Kuhusu pawatila utapata Kwa milioni 12 ikiwa complete na Kama ukiwa na pesa za kutosha unaweza kununua mbili. Ukiwa nazo mbili hapo mwenye trekta mnakula league na unaweza kumzidi kidoogo kutokana na wewe kutumia mafuta kidogo na PAWATILA kufanya kazi hata maeneo mapya au yasiyofikika Kwa trekta.

Kwa trekta roho ya paka ni New Holland, masey Ferguson, valtra, Kubota, ford na nyingine nyingi ambazo spa zake zinapatikana.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ahsante mkuu nafanyia Kaz ushaur wako mzuri
 
Natarajia kulima heka 60 Kwa msimu ujao hzo ni Kwa zao la mpunga Kisha mahindi hata hekari 10 pia nitaangalia soya maziwa na maharage huko huko na alizet
Heka 60 chache sana kwa trekta mkuu, nashauri anza na power tiller tena moja tu iwe mjapan kubota, ili uitunze vizuri, kama maana ukiwa na power tiller 2 kama una heka sabini yaani 10 za mahindi 60 za mpunga utachoma hela ya manunuzi tu aana kama ziko sehemu moja upiga ndani week 3 au mwezi unamaliza kama una madereva 3.. usipoteze pesa kuchukua trekta kwa hizo hekari.
 
Uzuri wa trekta ni kwamba akishalima shamba lake haimaanishi atalipaki mpaka msimu ujao, trekta ni biashara, akimaliza kwake anawalimia wengine kwa malipo anaingiza pesa!!
 
Heka 60 chache sana kwa trekta mkuu, nashauri anza na power tiller tena moja tu iwe mjapan kubota, ili uitunze vizuri, kama maana ukiwa na power tiller 2 kama una heka sabini yaani 10 za mahindi 60 za mpunga utachoma hela ya manunuzi tu aana kama ziko sehemu moja upiga ndani week 3 au mwezi unamaliza kama una madereva 3.. usipoteze pesa kuchukua trekta kwa hizo hekari.
Trekta ndio ni gharama, ila kwa muda mrefu trekta ni nafuu kuliko hiyo power tiller.

-Kwa siku power tiller utalima eka ngapi?

-Itakuchukua muda gani kumaliza eka 60?

-Umevuna. Power tiller itabeba gunia ngapi kwa trip kufananisha na trekta.

Kama huyu anapanga akimaliza eka 60, alimie na wengine. Basi trekta ni bora mara 20 ya hiyo power tiller. Hata kama hana nia ya kulimia wengine kwa ukubwa huo wa shamba, trekta ni bora zaidi. Dhumuni la kutumia mashine ni kurahisisha kazi na kuokoa muda, sasa power tiller kwenye eka 60 unarahisisha kazi kidogo na kuokoa muda kidogo ukilinganisha na trekta. Asee chukua tu trekta, ukubwa wa trekta uzingatie wingi wa kazi usije chukua dude la hp 90, 4wd afu unaenda kufanya kazi kwa msimu mzima unalima eka 100, tena za mbali mbali. Haitolipa
 
Heka 60 chache sana kwa trekta mkuu, nashauri anza na power tiller tena moja tu iwe mjapan kubota, ili uitunze vizuri, kama maana ukiwa na power tiller 2 kama una heka sabini yaani 10 za mahindi 60 za mpunga utachoma hela ya manunuzi tu aana kama ziko sehemu moja upiga ndani week 3 au mwezi unamaliza kama una madereva 3.. usipoteze pesa kuchukua trekta kwa hizo hekari.
Ni sawa kaka lakin mashamba ya mpunga udongo wake ni mzito ni mgimu pia, ni fulan unapasuka wakat wa kiangaz na Sion uwezekano wa powertiller kufany kaz nzuri! Lingne powertiller hazdumu Kuna moja nlmpa kibarua Tena kuburuza mlkolimwa hakuweza kipowertiller hakikati hata majan, kinatia hasira na trecta litatumika km kitega uchumi
 
Hizo ni Chinese tractor kama zinafanya Kazi vizuri kuilisha China kwann zishindwe.
Kama zilivyoingia lori na bus za Kichina leo zinakimbiza ndivyo zilivyo hizo tractor, nunua mapema zikizoeleka lazima bei ipande
 
Ni sawa kaka lakin mashamba ya mpunga udongo wake ni mzito ni mgimu pia, ni fulan unapasuka wakat wa kiangaz na Sion uwezekano wa powertiller kufany kaz nzuri! Lingne powertiller hazdumu Kuna moja nlmpa kibarua Tena kuburuza mlkolimwa hakuweza kipowertiller hakikati hata majan, kinatia hasira na trecta litatumika km kitega uchumi
Usilime kiangazi,lima masika,sisi huwa hatumilimi,tunasubiria mvua ichanganye kisha tunavuruga na rotavator Shamba likiwa tope kisha ndo tunaingiza rice planter
 
Foton tractor
 
Attachments

  • Screenshot_20230316_153824.jpg
    Screenshot_20230316_153824.jpg
    102.7 KB · Views: 59
  • Screenshot_20230316_154034.jpg
    Screenshot_20230316_154034.jpg
    74.9 KB · Views: 62
  • Screenshot_20230316_154047.jpg
    Screenshot_20230316_154047.jpg
    98 KB · Views: 55
  • Screenshot_20230316_154103.jpg
    Screenshot_20230316_154103.jpg
    112.8 KB · Views: 61
  • Screenshot_20230316_154133.jpg
    Screenshot_20230316_154133.jpg
    80.5 KB · Views: 59
  • Screenshot_20230316_154143.jpg
    Screenshot_20230316_154143.jpg
    87.9 KB · Views: 62
Usilime kiangazi,lima masika,sisi huwa hatumilimi,tunasubiria mvua ichanganye kisha tunavuruga na rotavator Shamba likiwa tope kisha ndo tunaingiza rice planter
Boc hapo umenpa kitu kizur naomba picha ya rice planter na Bei yake
 
China vitu bei rahisi ingia Alibaba, au made in china au buy in china utapata takataka zote utakazo tena kwa bei chee, zana za kilimo hazina ushuru zina VAT
 
Back
Top Bottom