Wafanyakazi wa Kituo cha Mavumbuzi ya Vifaa vya Kilimo cha Kitaifa waliendesha kutoka mbali trekta ya umeme aina ya ET1004-W mjini Luoyang, mkoani Henan, katikati ya China.
Katika miaka hii ya hivi karibuni, Kituo cha Mavumbuzi ya Vifaa vya Kilimo cha Kitaifa kimetengeneza chip ya kwanza ya udhibiti wa mashine ya kilimo katika China Bara, trekta ya kwanza ya umeme isiyo na dereva, trekta ya kwanza ya 5G+ inayotumia hidrojeni na mashine nyingine nyingi za kilimo, pamoja na mifumo ya kidijitali ya mashine za kilimo.