Kwanza nianze na lengo la mtoa mada: Nikijaribu kuweka kwa maneno machache nini kimemsukuma mtoa mada kuleta mada hii ni kwamba:- Kutokana na historia ya mabadiliko ya uongozi wa kisiasa kwenye nchi kadhaa za kiafrika kutoleta mabadiliko yaliyotarajiwa (kama mapambano dhidi ya rushwa na uboreshaji wa maisha ya raia wake), Je kuna haja ya kufanya mabadiliko/kuweka matumaini kwenye mabadiliko hayo hapa kwetu? Jibu ni ndiyo tunahitaji mabadiliko.
Kabla sijaeleza kwanini tunahitaji mabadiliko, ningependa kuelezea masuala kadhaa, kwanza ni kwa kurudi kwenye historia yenyewe na kugusia kidogo mifano uliyotoa; Ukiangalia historia ya Afrika kabla ya uhuru,wakati wa kutafuta uhuru na baada ya Uhuru kuna mshabihiano(kufanana) wa karibu sana. Hoja yetu hapa imejikita kwenye historia ya Afrika baada ya Uhuru.
Sasa ukiyatazama mataifa ya Afrika mara tu baada ya Uhuru yalikua na kazi kubwa mbili;
- Kujenga Utaifa - hii inatokana na historia ya mataifa ya Afrika kuwa na mikusanyiko ya makabila mbalimbali
- Kujenga Mifumo ya Uongozi na Demokrasia - Hapa masuala ya ni siasa za aina gani (ideology) zifuatwe
Bila kugusia mambo mengi tunaona kuwa mwanzoni nchi nyingi za kiafrika zilikumbatia mfumo wa chama kimoja cha Siasa ili kuleta Umoja na mshikamano miongoni mwa watu wao hivyo kujenga UTAIFA. Mwishoni mwa miaka ya 80 vuguvugu la kushinikiza mfumo wa vyama vingi lilianza na nchi nyingi za Afrika zikaanza ku "adapt" mfumo huu.
Sasa hapa something very interesting kinajitokeza: Kumbuka tuna vyama vilivyodai uhuru kama UNIP - Zambia, KANU - Kenya, TANU/CCM - Tanzania na ZANU-PF Zimbabwe, vyama hivi viliwapa tumaini kubwa sana wananchi wake kuwa baada ya uhuru maisha yao yataboreshwa kwa kiwango kikubwa lakini matokeo yake ni kunyume chake.
Miaka takribani 20 baada ya uhuru mfumo wa vyama vingi unaingia Zambia na Kenya tunashuhudia mabadiliko ya uongozi wa kisiasa ila hakuna kinachobadilika kwa upande wa kero za wananchi au mabadiliko yapo ila si ktk kiwango kilichotarajiwa, kwanini? hilo nitaliacha kwasasa..... Ila narudi kwenye suala la mabadiliko..Je tunayahitaji? jibu ni NDIO
Kwanini?
- Tuliukubali wenyewe mfumo wa vyama vingi ili tuwe na uchaguzi kwamba chama kimojawapo kituongoze hasa pale kilichopo madarakani kinaposhindwa kutimiza matarajio yetu - CCM imeshindwa kufikia matarajio yetu hivyo tunahitaji mabadiliko ya Uongozi
- Kuondoa dhana ya Uhodhi wa madaraka (monopoly) kwa CCM ili kujenga utamaduni wa kupokezana madaraka ya nchi baina ya vyama - hapa ndipo utaona kuwa wenzetu Kenya na Zambia wamefanikiwa katika hili na hapa ndipo ukomavu wa demokrasia hii ya vyama vingi tuliyojichagulia wenyewe unapopatikana.
Sasa swali la WOS "IS IT WORTHY to fight so hard kubadili viongozi/uongozi ilhali watakaokuja nao hawatakuwa na jipya?" Hivi how do we know exactly kama hao watakaokuja hawatakuwa na jipya? If a scenario is true in Kenya/Zambia is it necessarily true in Tanzania? Lazima tuwe na imani (kama alivyosema Mkandara) na uthubutu wa kufanya mabadiliko kwa maana vyama hivi ni vyetu tumevilea kwa kodi zetu kupitia ruzuku wanazopata hivyo tuvitumie kutupatia Uongozi mbadala.