TREND YA AFRICAN POLITICS. Historia Itajirudia Tanzania?


I do know the difference in what wenzetu and Us look in a Kiongozi, But believe me you sijawahi ifikiria in comparison katika pande ya kuangalia Viongozi in the lines of Heroes Vs Public Servants... Boss nimeipenda saana. For if one understands what traits and attributes to look in a HERO the same applies in what to look in a Public servant.... Yaaani ni Way over different..... Na hiyo says a lot of what kind of leader we choose. Don't know if we should be blamed thou for we surely need to be rescued...

Mkuu AJ nimeitikia mwaliko wako bado nadadavua mada...!


Karibu Saana Mkuu.... Na asante kwa Mchango wako.
 

Hio wait ishakua in Vain ya CCM Kujiweka sawa AJ…… Hivo saying in the same lines maneno kama UTU, HAKI, USAWA & AMANI na CCM… Ni kuwapaka tu mafuta kwa mgongo wa Chupa…. Wananchi wanaelewa hilo, Wadau wa Siasa wanaelewa hilo na Hata CCM wenyewe wanaelewa hilo…. Lets just call a spade by it's name "spade".

IMO Upinzani utapofanikiwa kuutwa Uongozi… inabidi waangalie saana Uongozi ulopita hasa in the lines of what has to be done hasa kuretrieve what is believed to stolen from the Tanzanian people… Tunaibiwa na hapo hapo tunakua treated kama wajinga na hatuna haki…. Wao upinzani wakija na wakua "React" ni one of the steps ya kuonesha kua wana nia nzuri (ila tu isiwe visasi vya kutiana ndani bila pesa/mali kurudishiwa; kikubwa sheria zifuatwe, ushahidi uwekwe peupe na HAKI itendeke) Hayo yakifanywa haina maana kua ndo UTU, HAKI, USAWA & AMANI vitakua vimerudi… No! ila itakua ni one step ya kuelekea huko! Hivo AJ hata sishangai kua bado watafakari…..


Chatu D Asante for the acknowledgment... Na nakubaliana nawe kua kweli tuna safari ndefu saana; thou ningependa saana kujua huo mfumo mwingine unasuggest uwe vipi??
 


Mkandara.... Words can not suffice.... IMO GREAT Analysis in relation to the Topic.... THANK YOU.
 

ADii, kwa maelezo haya napata picha kuwa unakubalina kuwa MABADILIKO should be in place ..au vipi? But is this going to solve the*dilemma which is the force originating this thread...? Kwa sababu tumeona kuwa mabadiliko ... yanakuwa basicaly sio mabadiliko kwani ..Historia inajirudia... Is what you*explained*going to take care of that ..?
 


Mawazo matatu….. The insight umetoa I have appreciated…. Na hio ya kusema kua Vyama vilivodai Uhuru hadi kuweza fanikiwa in most cases tunaona kua vilionesha kushindwa. If an interested person aki-observe hilo ndio atajua kua ni kwa nini kwa kiasi kikubwa CCM imeweza shamiri na Kufika mpaka leo na bado inadunda! Naamini kabisa kua kama Kaunza (Zambia) angefanya alivofanya Mwalimu hapa Tanzania; kuachia ngazi kwa fresh blood within the Chama maybe nayo ingekuwepo mpaka leo-for nature ya wale watu ni passive….. Ndio waweza lalamika but sio wapiga kelele for instance nikii compare na Kenya.

Kwatika vipengele vyako hivo viwili vya KWA NINI; I am more interested na hio ya pili….. Genuinely speaking ukitaka uangalie mfumo wa Uongozi wa Tanzania sasa hauna tofauti kabisa na Libya; In the sense kua Libya imekua under the same leadership reign for more than Forty years…. Tuna tofauti gani na sisi Tanzania kama for all these years tupo under the same Chama, with the same agendes combine with the same attitude kwa Wananchi no matter the President?? Milipuko ya Kashafa NDIO ni kweli kua recently ndio yameshamiri but the roots za most kashfa ni dhahiri kua si ya leo wala ya jana….

Hivo basi nikirudi hapo ulipomgusia WoS Kwamba how would we know if wanaokuja watakua na Jipya…. I think it is worth it… Hao watakao kuja whether wachemka ama lah! Kitendo cha kubadilisha Chama leave alone the President from another Chama is a first step to Positive change (hio ni IMO); Na moja la kutambua ni kua Watanzania should brace themselves, for kuja kwa new Chama mwanzoni mambo yatakua hata worse if kweli hicho Chama kitakuja na Changes za kumgusa Mwanachi….
 

SOBY in supplementary words you are saying that a new Party and a President from a fresh party is ineffectual if it is still an equivalent constitution….Which of course I do agree with; Thou I don’t have faith nor confidence kua a new Party will amend areas of which would affect an almost absolute control of Leadership as much as all the opposing parties walalama sasa. The only way for the Constitution to be there for the people is as you have said ni to let the people more involved…. (which I still regard as a daydream for it to really occur)
 
Adii
Tunashukuru kwa very informative thread na michango mingi iliyotolewa! Mimi sioni shida sana hasa kama nia ipo kwenye kurudisha mali za watanzania.

Changamoto niionayo ni kuhusu mikataba mingi mibovu iliyosainiwa! Je utawala Mpya waweza au kutoweza fanya nini? I am interested to know Satta atafanya nini na Wachina huko Zambia!
 
Thats what most of us fail to uderstand,
We need a leader that will tell us "We are te problem".
Power is not taken, it's given (directly or indirectly).
 
faida za upinzani (hapa kwetu tz) zinajionyesha wazi, kupata ubunge/udiwani sio tena 'easy peasy lemon squeezy' business na ticket ya chama tawala pekee haimpi mtu guarantee ya kushikilia madaraka miaka nenda miaka rudi huku akihudumia tumbo lake na wanawe bila kujali jamii....

upinzani umesaidia kuwaamsha wanavijiji wengi ambao walikuwa wamelala, na wengine wengi tu wanazidi kuamka .naamini huu ni mwanzo mzuri wa ukombozi. miaka 10 iliyopita nani angeamini kwamba chama chochote cha upinzani kinaweza kuitoa CCM jasho kwenye uchaguzi wa IGUNGA!

naamini Tanzania itakapopata nguvu na uwezo wa ku tumia nguvu ya balot kubadilisha viongozi wazembe mambo yatakuwa tofauti na nchi nyingi za chini ya jangwa la sahara kwa sababu tupo tofauti katika maswala ya ukabila. Hatutachagua viongozi ambao bunge ni sehemu yao ya kujipatia utajiri wa haraka haraka na sifa za kuitwa mzee ati kwa sababu tu wanatoka kwenye kabila zetu, hatuachagua kiongozi kwa sababu tu ameonyesha dalili kuwa atajali maslahi ya kabila letu na kuwa kuwaonyesha cha mtema kuni wale wa lile kabila jingine. tutachagua viongozi kutokana na uadilifu, uchapakazi na kujali maslahi ya wanyonge...that will make a HUGE difference I believe. whether tutawaweka ndani masifadi au la hilo bado sina uhakika nalo. Ila maendeleo na mabadiliko lazima yataonekana wazi...
 
Jamani naona hoja kubwa hapa ni "Je hao tutakaowapa madaraka baada ya CCM wana jipya?" suala la kuwa na jipya au la..! its a relative term, kwangu mimi CDM imeonyesha mapya mengi tu hata kabla ya kupewa madaraka ya nchi, kuanzaia Bungeni, kwenye Majukwaa ya Siasa(kufichua uovu n.k), mpaka kwenye manispaa wanazoziongoza...sasa sijui watanzania wenzangu nyie mnataka nini? labda tumuombe Mwenyezi Mungu atuazime malaika wake waje watuongozee nchi.
 


Your english is top notch bro, love it
 

Thats what most of us fail to*understand,We need a leader that will tell us "We are te problem".*Power is not taken, it's given (directly or indirectly).

I see to this and understand that, CHANGES are*Inevitable and to solve the DILEMMA which founded this thread .. we have to*involve*more*people*and make them face their own truth*with*the effect of restoring their own POWER.
 
MawazoMatatu,

Polepole uzi unavyokwenda tunapata jibu. Sioni kama bado hatana mwelekeo .. Hoja ni nzito ..lakini mwelekeo ni mzuri kuwa*MABADILIKO*ni muhimu na ili kuondoa*KIGUGUMIZI*cha kurudia Udhaifu wa Mabadiliko kadhaa yaliyotangulia kwa nchi mbalimbali za kiafrika kuwa ... hatimaye mabadiliko yanakuwa hayakuwa na TIJA ..tunajribu kuangalia ..Nini kifanyike...*

Na ninafikiri hadi hapa mjadala ulipo ni kuwa Kwa vile hakuna namna Nchi inaweza kuwepo bila Uongozi wa KisiaSA .. na sisi hatuna budi kuona hilo na kujua ni kweli lazima ..kwa wakati wowote ..lazima tuwe na Uongozi...*

Sasa ni wazi CCM wako katika muda wao wa mwisho na lazima Chama kingine au mfumo mwingine uwepo ... ukiangalia kwa ukweli wote ... CHADEMA ndio wanamwelekeo ... Lakini ... KIGUGUMIZI .. wasije wakayarudia ya CCM mara tu muda ukipita baada ya kuwa madarakani.

Wewe umeonyesha kuwa .... Kuwa MABADILIKO ni lazima na kuwa CHADEMA ...wameonyesha *... mambo kadhaa (kwenye bluue) waliyoyafanya yanayokupa moyo *na kukuondolea KIGUGUMIZI. .. amabocho ndio msingi wa kurusha huu uzi!!
 
Good! Mkubwa hapa unenikuna, kwanza hiyo misamiati ni darasa tosha.ur in +ve myopic uropheria.
 

I get what you are saying... This thread is a cry and a reminder to all Wapinzani kua We are watching.... We are Knowledged of what is going on... We are interested in what is going on and most importantly they should know that our only hopes is for them to succeed and that if they do succeed we expect them to act accordingly.... Ndio nime admit kua in most cases MABADILIKO has been for the worse, but nimeelezea hata katika this thread in many posts kua a new Party is just one step towards the journey of CHANGE.... Na sababu saizi tunaongea more out of assumptions tukichukua tu case studies.... Let the changes happen na tuone kama itakua for better or for worse!!

Thats what most of us fail to uderstand,
We need a leader that will tell us "We are te problem".
Power is not taken, it's given (directly or indirectly).

Soby Mkuu you have to note that hio in blue is not really a guarantee for positive CHANGE....
Kumbuka the way JK alipokelewa uchaguzi wa kwanza... Na the way majority ya walompa uongozi the way saize wanamshutum...
 
Big up, AshaDii!!
Sikuwa najua kuwa una interest ktk politics, lakini nimekupata. Thread yako ni nzuri sana for a fact that it's like a double-edged saw. Inagusa madhambi ya the incumbent administration na at the same time inatoa clear warning kwa the opposition kwamba wakiingia madarakani na wasipo-deliver na wao nao watakuwa tena ni wabaya kuliko magamba.
Kuna mdau mmoja amesema huko nyuma kuwa suala sio kubadili rais na chama pekee bali ni kui-revamp the entire polictical system. Hilo litafanikiwa endapo itakuja constitution ambayo itakuwa wazi na isiyo na mizengwe na ambayo itakuwa na zero tolerance kwenye wizi, uzembe, ufisadi, rushwa etc. kwa yeyote yule i.e. nobody will be above the law. JK, Slaa, Mkapa, Pinda, Maalim Seif, Mbowe, Shein etc yani akipindisha mambo anakwenda kwenye sheria na kuishia jela. Sio jela ya kupeana sentesi za usanii akina Liyumba, NO!! Jela ya kumpoteza mtu miaka 400
Again, big up AD.
Take care
 
Nikiendelea kuchangia mada zaidi kwa sababu ina mafundisho mengi sana hasa tunapotafuta asili na dawa kwani magonjwa ya binadamu sii ya viungo tu hata FIKRA pia ni ugonjwa mbaya sana..Katika yote haya bado swala la TRUST kwa mtu mweusi linajitokeza zaidi ktk hoja nyingi nilizowahi kuzisoma na hii trust ni baina ya mtu namtu au WATU na chama au viongozi wake. Na hakika nimejifunza sana ktk mahojiano yangu na baadhi ya watu hapa hapa JF kutambua jinsi wanavyofikiria na imani zao..Hakika tusijidanganye, na nitaendelea kusisitiza kuwa Trust haiwajawahi kuwa utamaduni wa Mtanzania toka tupate Uhuru isipokuwa kwa ushawishi wenye malengo ya kuwaunganisha. Tunajaribu sana kuitumia trust au kutaka kuamini watu au vyama lakini tunashindwa kwa sababu huu sii utamaduni wa mwafrika kumwamini mtu asiyekuwa wa jamii yake au dini yake.

Labda nitashabihisha zaidi kwa kusema kwamba Waafrika hatuna kitu Trust, historia inajieleza kama nilivyosema huko mwanzo. Tumepitia mengi yenye kutoaminika kwa sababu tunajidanganya ya kwamba UONGO usiodhuru moja kwa moja sii dhambi. Kutoa ahadi za uongo sii kosa ikiwa utanusurisha balaa ya ukweli wakati wenzetu wazungu na Mataifa mengine UONGO ni kosa kubwa kuliko hata Jambazi. Shahidi muongo anaweza kabisa kufuta kesi ya Jambazi na asiaminike tena kwa lolote wakati sisi tunaongopa bila kupima kwani ni mila yetu kuongopa ili kujinusuru, hivyo ndio maana sisi ni wanafiki wakubwa na vigumu hata kuaminiana.

Unaweza kushindwa kuelewa hasa maana yangu lakini jiulize ni watu wangapi kuwaamini kwa moyo wako wote. Sidhani kama watajaa mkononi na pengine huna hata mmoja!. Na wala hatuna utamaduni wa kujenga uaminifu kwa sababu sii swala kubwa ktk maisha ya mwafirika maskini ambaye hakuzoea kujitawala isipokuwa kutawaliwa, hivyo uongo humpoa nafuu ya madhara ya kutawaliwa.

Hili swala la kujiuliza wakiondoka CCM, je ni wapinzani gani tunaoweza kuwapa dhamana ya kutuongoza na wakafanya vizuri? Hakika asilimia 80 ya Watanzania hawaamini chama wala mtu yeyote na hivyo kubakia ktk ushabiki kwa sababu hata wayasemayo viongozi wa Chadema au CUF wananchi wanajua kuna UONGO ndani yake na hata kesho yakitokea kuwa uongo haiwezi kuwaathiri zaidi kwa sababu walijua toka mwanzo kuna uongo. Niulize mimi kama namwamini Dr.Slaa au JK au Mbowe sintakujibu kwa sababu sielewi niwaamini ktk lipi? na siwezi kuwapa roho yangu kwa kuaminisha wataweza kufanya jambo fulani isipokuwa nasukumwa na uchungu wa kuona jinsi CCM ilivyoweza kuimarisha UFISADI hali Chadema wakijaribu kutukomboa, na siwachukii CCM isipokuwa kwa matendo yao ya udhalilishaji na ujenzi wa mfumo ambao utakuja teketeza kabisa jamii yetu.

Kwa hiyo CCM wameendelea kujiboresha ktk sehemu ambazo zina udhaifu wa wananchi wenyewe na kwa bahati mbaya tumeshindwa kujifunza kutokana na historia ya kwamba sisi waafrika tumeweza tu kujikomboa ktk adha mbali mbali kutokana na UMOJA wetu. Wakati Marealle na Mtenvu wakihubiri Ukabila, TANU walijiweka nguvu kubwa ktk ujenzi wa UMOJA wa Watanzania bila kujali makabila yao na dini zao. Wakawapa imani wananchi kwamba mapambano yao yalijikita ktk kumuondoa mkoloni na sii tofauti za Makabila na Udini, hivyo kila mmoja wetu akasahau tofauti zetu na kumtazama mkoloni kama adui yetu. Vivyo hivyo kwa kina Kaunda, Obote na Kenyatta wote hawa walijaribu zaidi kuwaunganisha wananchi na sii kujitofautisha nao ktk harakati za ukombozi wa Mataifa yao.

Hata ukitazama coalition ya vyama vya Kenya kufikia kumwondoa KANU au ZANU ya Zambia ilikuwa ni nguvu ya kutafuta UMOJA, kuondoa tofauti zao za kiasili kwani ilikuwa mara ya kwanza Mjaluo na Mkikuyu, kuunganisha nguvu ya pamoja against chama tawala. Na imetokea nchi na mataifa kwamba mageuzi yeyote yameweza tu kufanikiwa ikiwa nguvu kubwa itawekwa ktk kuwaunganisha wananchi badala ya kukubali tofauti zao na kuzitumia ktk chaguzi au mageuzi lakini leo hii tunaona kwamba vyama vyetu vimetumia sana tofauti zetu kueneza siasa za majitaka hata kama waathirika ni sisi wenyewe.

Mwisho, najiuliza sana kwa nini mtu afikirie zaidi kutomuamini Dr.Slaa au Zitto kutuongoza ikiwa ndani ya nyoyo zetu hatuna mtu mmoja tunamwamini wote - nambieni mtu mmoja ambaye kweli ktk mioyo yenu mnamu amini? - HAKUNA! na ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho! pia sii swala la kuwaamini Chadema kwa sababu wewe mwananchi ndiye unayekiunda chama hiki sii Mbowe au Dr.Slaa hawa wote wamekuja kuwa maarufu ndani ya chama. Ni kazi ya kila mwanachi kupiga vita utengano na kuhubiri UMOJA wetu na sii kukitazama chama kwani tulotengana ni sisi.

CCM leo hawawezi kuzungumzia UMOJA kwa lengo la kufanya mabadiliko kwa sababu hawawezi kuzikarifu nafsi zao kupingana na yale waliyoyakumbatia isipokuwa watatukuza UMOJA kwa lengo la sisi wananchi kukubali kutawaliwa wakitumia sanduku la kura ambalo chimbuko lake ni mgawanyiko wa wananchi wenyewe ktk makundi ua Udini na Ukabila. UHURU na UMOJA ni misingi ambayo ilitufikisha kuwa huru lakini laeo tunazungumzia UMOJA wakati hali ya UHURU wetu ni tata...
 

Mkuu labda suala hili tumelichukua juu juu sana bila kuchunguza hasa undani wake, kusema mabadiliko mengi kwenye nchi za Afrika yalishindwa kukidhi haja bila kuangalia nini kilisukuma mabadiliko hayo tunakuwa tunapotea njia na hatuwezi kukokotoa mlinganyo ulio mbele yetu (kile unachokiita DILEMMA)

Nitatoa mifano michache kuhusu hili:

Kenya:
Kwa wanaofuatilia mambo tunajua kuwa baada ya Moi kuona sasa inafaa kwa yeye kuachia ngazi alimpendekeza Uhuru Kenyata awe mrithi wake kupitia KANU jambo lililowaudhi wenzie na ndipo KANU ikamegeka na viongozi wengi waliokuwa wana matarajio ya Urais walipoamua kukihama chama na kwenda kutengeneza National Alliance Party of Kenya (NAK) huku Kibaki aliyewahi kuwa makamu wa rais kipindi cha Moi akisimama kwa tiketi ya NAK.
Sasa swali linakuja: Kama Kibaki na wenzie walikuwa sehemu ya serikali wakati wa Moi tena wakishikilia nafasi nzito unategemea walipoingia madarakani wangekuja na chochote kipya? Je mabadiliko ya Kenya yalisukumwa na kero za wananchi au yalikuwa tu ni matokeo ya minyukano kwenye kunyang,anyana madaraka?

Zambia:
Baada ya utawala wa miaka 27 kwa chama cha UNIP chini ya uongozi wa Keneth Kaunda, Zambia inajikuta kwenye machafuko makubwa yanayotokana na vurugu za wananchi juu ya ukosefu wa chakula na hali mbaya ya Uchumi. Kaunda ili kuwafurahisha wananchi anaruhusu mfumo wa vyama vingi (hiyo ni mwaka 1991) na vyama 11 vinaundwa kikiwemo MMD cha F.Chiluba, mwaka huo huo October 31 uchaguzi mkuu unafanyika Chiluba anamshinda Kaunda kwa asilimia 76% na kuchukua viti 125 kati ya 150 vya Bunge.
Sasa swali linakuja: Je mabadiliko ya Zambia yalisukumwa na nini? Tunaona pamoja na kuwa Chiluba alijulikana kama Kiongozi mzuri wa vyama vya Wafanyakazi, hakuwa na Chama imara kinachoweza kuongoza nchi (kumbuka chama chake kilishika madaraka ya nchi kikiwa na less than a year toka kimeundwa)

Congo:

Kwakweli suala la Congo sina hata haja ya kuongea mengi kwakuwa hatuwezi kupima mabadiliko ya Congo. Tutakuwa hatutendi haki kama tutadai maendeleo yoyote kwa nchi ambayo bado iko kwenye changamoto ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mpaka sasa

Kwa kumalizia naweza kusema tumeangalia mabadiliko ambayo hayajafanikiwa Afrika, Je kuna mabadiliko yoyote ambayo yameleta neema Afrika?
Jibu ni NDIO: Rwanda yanayotokea huko wote tunajua, Ghana ambako ripoti zinasema uchumi wao sasa unakua kwa zaidi ya asilimia 14% kwa mwaka.

Watanzania tuache visingizio, muda wa kufanya kitu kujikwamua kutoka kwenye Uongozi wa kubabaisha ni huu, tunahitaji kudhubutu, tunahitaji kuwa ma risk taker. 2015 Inshallah..!
 
Exactly!.. ndio maana tatizo ni watu wenyewe.
 

Tai Ngwilizi yawezekana kweli you have a point unaposema kua tupo tofauti na nchi zingine… But I really hope you have observed and seen the changes zilizotokea kwa sie Wananchi and in a short time with a speedy rate siku zinapozidi kuenda…. Hili suala la CCM Vs CDM laweza change a lot of things katika clouding kwa judgment ya the majority on the basis ya "Udini" sababu ya watu wachache wenye Ufikiri mdogo ambao wanataka pronounce dini kama moja ya Vigezo…. Issue ambayo haijawahi tokea inchini kwetu…. Sad.

Kuhusu Mafisadi… mie hata sina shida kua watiwe ndani… Shida yangu warudishe Mali ambayo itaonekana wazi ni ya Wananchi…. Vitu kama migodi… na Assets kibao ambazo kabisa ni wazi ni za Wanachi kweli inabidi ziwepo taratibu za kurudisha or else haina maaana. Napenda the angle you have drawn from, it has given me something to chew….


Mawazo matatu.... Hilo swali in blue kwa sasa ni "Million Dollar Question" And the price tutalipa ni TIME.... Only time will tell, Hivo tu i think tuwe atleast Optimistic saizi, for Pessimism ikizidi nayo it wont give us a logical and Reasoning full of Clarity...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…