Kuwa na tabia ya uchoyo ni matokeo ya malezi lakini si sababu ya mtoto kuwa peke yake. Siku zote kile unachomfundisha mtoto ndicho anachokuwa nacho.
Nakumbuka mimi binafsi tulizaliwa wawili lkn mdogo wangu alikuja kuzaliwa mimi nishamaliza darasa la saba kwa hiyo ni kama maisha ya utoto nilikuwa mwenyewe. Mama yangu alichokuwa ananifundisha hakuwahi kutoa kauli ya hiki ni cha kwako,,ukienda sehemu yoyote kusalimia lazima atakupa maharage, karanga au chochote kupeleka kama zawadi. Kwa hiyo nikawa najua kumbe tunapaswa kuwajali wengine.
Nimekua mtu mzima binafsi siwezi kwenda kwenye mji wa mtu kusalimia bila kubeba chochote yaaan siwezi. Kama sina huwa naahirisha hadi nitapopata. Na isitoshe watu wanaonizunguka nawajali kwa moyo wangu wote,,hata kama nina kidogo hii imenijengea na kunipa familia ya watu ambao hatujazaliwa pamoja na kujaliiana kama tuliozaliwa.
Binafsi pia nimebarikiwa mtoto mmoja.ana umri wa miaka 4 sasa Najitahidi kumlea katika misingi ile ninapoenda kumnunulia kitu mfano pipi nitanunua mbili nampa moja namwambia hii mpelekee rafiki yako ,,kwa maana ya mtoto wa mpangaji mwenzangu. Hivyo anabeba anampelekea,, au wakati mwingine nikimnunulia kitu dada wa kazi nampa yeye aende akampe.
Imefika wakati hata kama nimejisahau kununua pipi mbili akifika yupo radhi ampe rafiki yake akija unamuuliza pipi iko wapi anakwambia nimempa fulani.
Si kwamba watu hawatamani kuzaa watoto wengi lkn unaangalia na uwezo wa kulea watoto hao. Na kikubwa ni kusimama tu kwenye malezi ambayo unatamani mtoto wako unatamani aje kuwa.
Sent using
Jamii Forums mobile app