JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Ajali imetokea baada ya mabehewa sita (6) ya treni kuacha njia na kupelekea majeruhi 70, wanawake 26 na wanaume 44. Treni ilikuwa na jumla ya abiria 571 wakisafiri kutoka Kigoma kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
TRC kwa kushirikiana na Kitengo cha Afya cha Mkoa wa Kigoma walifanikiwa kuwapeleka majeruhi katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza kwaajili ya matibabu. Hali za afya za abiria zinaendelea kuimarika, majeruhi 57 tayari wameruhusiwa, nane (8) wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza na watano (5) wamehamishiwa Hospitali ya Maweni kwaajili ya matibabu. Treni iliendelea na safari kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
Shirika linawapa pole majeruhi na linaendelea na jitihada za kuwahudumia. Hakuna taarifa ya vifo vilivyotokana na ajali, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.