KERO Treni ya mchongoko Dar-Dodoma imeharibika porini toka saa 2 asubuhi kati ya eneo la Pugu na Soga

KERO Treni ya mchongoko Dar-Dodoma imeharibika porini toka saa 2 asubuhi kati ya eneo la Pugu na Soga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Marekebisho ya kiufundi ?

Kifaa kipya!

Ufundi wa nini ???

Niliishi Brooklyn, New York. Subway lao limejengwa mwaka wa 1904.

Sijawahi kuona limekata moto.

La kwetu lina miezi miwili unusu. Kila siku linakata moto porini.

Tatizo nini ????
Ulikuwepo huko New York mwaka 1904 wakati treni yao inaanza kazi na ukashuhudia haikuwahi kupata hitilafu?

Treni ya hapa na miundombinu yake ina muda gani tangu ianze kazi, na hiyo ya New York ina muda gani hadi sasa?

Tarehe 20/08/2024, The New York Times waliripoti taarifa ya kusimamishwa kwa huduma ya treni za umeme kati ya Philadelphia na New Haven, kutokana na hitilafu ya umeme.

Tarehe 17/07/2024, ABC News waliripoti kusimamishwa kwa huduma ya treni kwa saa kadhaa kutokana na hitilafu ya umeme. Wameandika, "In New York City, a power outage on the third rail at Delancey St-Essex St. in Lower Manhattan shut down the J subway line in both directions between Manhattan and Brooklyn." Tatizo ni hitilafu ya umeme.

Tarehe 20/06/2024, the New York Times waliripoti kusitishwa kwa huduma ya treni kati ya New Jersey na New York kutokana na hitilafu ya umeme.

Hizi kesi sio za 1950, ni za 2024. Na zimetokea huko kwa walioendelea na wenye uzoefu wa zaidi ya miaka 100 kwenye hii industry. Punguza ujuaji mzee. Hizi changamoto zipo tu.
 
Shida ni treni jipya limekwama porini.

Kwa nini mitambo mipya inaharibika haribika ovyo ?

Limekuwa gari la mkaa ?

Hata lori la mkaa halikati moto porini likiwa jipya.

Tulinunua mitambo chakavu ? Kwa nini ma VX yao mapya hayakati moto porini ?
Treni ni mtumba Lile sio jipya..
 
Imetoka Dodoma saa 12 kamili asubuhi.

Tangu saa mbili asubuhi, treni imekwama. Sasa inaenda saa 7 mchana, na hakuna matumaini ya kuendelea.

Treni iko kilomita 45 kutoka Dar, porini. Wengine wanashuka na kupanda boda; wanaenda wapi, sijui. Tangazo la TRC linasema mafundi wapo kazini.

Chombo ni kipya, mitambo ya umeme ni mipya, na umeme upo. Nadhani juzi TANESCO walisema tunakimbia na ziada, na maji pia, kama ilivyosemwa na DAWASCO siku tatu zilizopita. Lakini leo, Jumapili, maji yamekata!

Abiria wapo, hivyo operesheni na mtaji wa matengenezo vipo.

Tatizo nini?

Wazalendo ndani ya TRC, tafadhali tujulishe kupitia njia zetu za kujuzana. Viongozi watatudanganya. Hawana dini. Waliwahi kusema Rais ametingwa na kazi Ikulu, kumbe ameshanyooka. Na waliongelea msikitini. Astakafullulilah Ladhim.

=====
Ufafanuzi wa TRC soma hapa: TRC yaomba radhi Treni ya Mchongoko Dar-Dodoma kusimama ghafla kati ya Pugu na Soga
Ilipoharibika ni jirani na Kongowe Kibaha hivyo wanachukua Pikipiki wanaenda Morogoro Road kupanda Mabasi
 
Niko stesheni Dom mpaka sasa hivi treni ya kuondoka saa kumi na moja haijaja. TRC ikubali tu leo imepata loss hivyo iwarudishie fidia wasafiri wote waliopata changamoto leo.
Namba za simu wanazo kwenye data base ya ticket. Hawawezi shindwa kufanya hivyo. Japo iwaback nauli zao tu.
Ni juzi tu hapa mmejisifia mnapiga mabilioni ya faida. Mkubali na hasara basi ndio biashara ilivyo leo faida kesho hasara.
Niko palee kama watatekeleza hili.
 
Niliishi Brooklyn, New York. Subway lao limejengwa mwaka wa 1904.
Ungekuwepo miezi miwili au mitatu ya miradi hiyo kuanza hiyo 1904 nadhani ingekuwa valid presidency nzuri otherwise is invalid yet!
 
Hawa jamaa wa TRC ni wajinga sana, tripu za mwanzoni supplier alitakiwa atoe dereva na mafundi ambao watatembea na wale wazawa mpaka walau miezi sita au mwaka.

Kuna kitu kinaitwa after sale service, hakitumiki hapa?
 
Ishu ni kwamba Serikali ya Korea zilipoundwa hizi treni walitoa maelekezo kwa TRC kuwa locomotive drivers & others responsible kuwa lazima wakafanye mafunzo Korea kwa almost 3 yrs Sasa ikawa kinyume drivers hao wamepewa mafunzo ya 2 weeks na kulipwa @ 1.5 M then watawala wakapiga mipunga iliyobaki na wao kujipa route ya Korea as drivers Hadi wakorea wakawaambia hii ni too much na italeta shida. Koreans wao imewa cost 6yrs ku masters mitambo hiyo Sasa Leo hii locomotive driver hajui abc on how to operate mitambo kwann isibume,kwann nyani na bundi wasi haribu mitambo? TRC HQ wanajua A to Z hili. Tume iundwe Ila ukweli ni huo kozi hii ilipaswa kuanza miezi 4 imepita fedha imepigwa na wahuni wachache
 
Aisee tuna viongozi wa ajabu sana. Kweli fisiemu ni janga
 
Imetoka Dodoma saa 12 kamili asubuhi.

Tangu saa mbili asubuhi, treni imekwama. Sasa inaenda saa 7 mchana, na hakuna matumaini ya kuendelea.

Treni iko kilomita 45 kutoka Dar, porini. Wengine wanashuka na kupanda boda; wanaenda wapi, sijui. Tangazo la TRC linasema mafundi wapo kazini.

Chombo ni kipya, mitambo ya umeme ni mipya, na umeme upo. Nadhani juzi TANESCO walisema tunakimbia na ziada, na maji pia, kama ilivyosemwa na DAWASCO siku tatu zilizopita. Lakini leo, Jumapili, maji yamekata!

Abiria wapo, hivyo operesheni na mtaji wa matengenezo vipo.

Tatizo nini?

Wazalendo ndani ya TRC, tafadhali tujulishe kupitia njia zetu za kujuzana. Viongozi watatudanganya. Hawana dini. Waliwahi kusema Rais ametingwa na kazi Ikulu, kumbe ameshanyooka. Na waliongelea msikitini. Astakafullulilah Ladhim.

=====
Ufafanuzi wa TRC soma hapa: TRC yaomba radhi Treni ya Mchongoko Dar-Dodoma kusimama ghafla kati ya Pugu na Soga
Haya sasa ngedere na bundi wasubiri lawama nyingine ama waundiwe kikosi cha kuwaangamiza kama tulivyozoea
 
Mungu ajaalie "mifumo ya uendeshaji" ndege zetu isitokee.

Watanzania ni bogus sana, utakuta maereva waliamka na pombe, wa kichwa cha mbele anaenda Dodoma wa kichwa cha nyuma anaenda Dar.

Hakuna cha "hitilafu" wala nini kwenye mifumo ya uendeshaji, ni uzembe tu.
Unaambiwa hiyo treni ni mpya watuwamekula hela za mafunzo kwa madereva.
So madereva hawana training
 
Fikiria siku mchongoko huo wa Korea utakapokwama ndani ya lile handaki kubwa kati ya manne kule Kilosa....Du!. 😲 Hivi watanzania hasa hawa viongozi na watendaji, wanaweza kufanya kitu gani kwa ukamilifu? 😢
Nashauri viongozi wote waache kusafiri kwa mashangingi watumie joka ili wajue wakizembea tu nao wanamezwa
 
Hawajasema wataanza safari "sio muda mrefu.'

Wamesema ndani ya saa moja!

Itakuwa mida ya saa nane!

Treni limebuma saa mbili asubuhi. Itakuwa limebuma masaa sita.

Treni la Gongo La Mboto halijawahi kugoma masaa 6. In fact, halijawahi kugoma, for all we know!

Hili jipya, la kisasa, la kitaifa, kwa nini likate moto porini masaa sita ???
Jiwe lilikuwa chuma
 
Unaambiwa hiyo treni ni mpya watuwamekula hela za mafunzo kwa madereva.
So madereva hawana training
Mafunzo wamepewa.

Unajuwaje kuwa kosa ni la madereva au uzembe wa mtu mwengine.

Kwenye hivi vyombo vya usqfiri, uzembe husababisha maafa, pengone dereva kaliona kosa akaamuwa kusimamisha treni mpaka ifanyiwe marekebisho.

Usowe mwenye kuhukumu kabla hujapata taarif kamili, huo unakuwa ni ukondoo.
 
zimetokea huko kwa walioendelea na wenye uzoefu wa zaidi ya miaka 100 kwenye hii industry. Punguza ujuaji mzee. Hizi changamoto zipo tu.

Nipunguze ujuaji, halafu iweje ???

Niongeze ujinga ???

Yani mnataka kila namna ya public discourse, mijadala ya kitaifa, iwe ni ya mtindo wa kutufanya sisi ni recipient wa kudumu wa "kutupa elimu" ????

Kwa nini Mwafra akidai maboresho, maendeleo, akikosoa mifumo, akikosoa watumshi wa umma, akikosoa viongozi, anaambiwa anajifanya mjuaji ? Sasa ajifanye mjinga ???? Mnataka maraia zezeta ???

Hell freaking no! Hatukubali ma third world mentality mgando yenu.

TRC is a dumpster fire. Which is a microcosm of the whole Samia administration.

Hayo matreni ya Marekani uliyosema yalikwama, yalikwama masaa tisa ???? Yalikwama na abiri njiani ???

Jana watu wamekaa porini Soga masaa tisa. Hiyo inakuaje ni sawa ? Kwa nini tusiseme?

Imetokea lini hiyo huko USA unakosema nako inatokea ???
 
Back
Top Bottom