Kanusho la taarifa ya kuanza kwa huduma za safari za treni za kisasa Dar es Salaam - Morogoro.
- Tunachokijua
- Kumekuwa na taarifa zilisosambazwa sehemu mbalimbali ya kwamba Shirika la Reli Tanzania limezundua huduma zake za usafirishaji wa Treni za Kisasa zinazotumia umeme Dar es Salaam kuelekea Morogoro.
Taarifa ambazo zimekanushwa na Shirika hilo na kusema kuwa hazina ukweli wowote. Shirika hilo limekanusha taarifa hiyo yenye lengo la kupotosha umma na kusema kuwa siyo taarifa ya kweli na kwamba shirika halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na tarehe ya Uzinduzi wa huduma ya usafiri wa Treni za kisasa kwa kipande cha Dar es Salaam- Morogoro na hivyo linafuatilia ili kujua waliosambaza taarifa hiyo ili kuwachukulia hatua stahiki za kisheria.
Pia shirika limeongezea kwa kusema wapo katika hatua za mwisho za Ujenzi wake na pia ujenzi mradi huo unaridhisha hivyo wananchi na wadau wanaombwa kupuuzia taarifa hizo.