Treni ya SGR imekuja kukomboa au kudidimiza wananchi? Hayati Magufuli asingekubali nauli hizi

Treni ya SGR imekuja kukomboa au kudidimiza wananchi? Hayati Magufuli asingekubali nauli hizi

Hoja hapa nikuleta nafuu kwa wanannchi. Kumbuka hii ni mali ya umma, sio ya wamiliki wa mabasi
Nyankuru

Kitu chochote ambacho huwa kinaokoa muda lazima kiwe na thamani.
Mfano; ukitoka Gongo la mboto kwenda posta kwa daladala kama sikosei nauli ni 750, lakini kwa umbali huo huo ukitumia pikipiki ambayo utaokoa muda zaidi nauli inafika mpaka elfu5 unafikiri ni Kwanini?

sababu muda ni kitu chenye thamani zaidi kuliko kitu chochote. Lakini pia mkuu uelewe tunatofautiana hali za kimaisha, kuna wa tabaka la chini, tabaka la kati na tabaka la juu.

Kama mtu anapanda ndege kwenda Zanzibar kwa dakika 20 ina maana kwamba anaokoa muda kitu ambacho ni cha thamani zaidi, wewe tazama tu katika maisha ya kila siku kitu chochote ambacho kinaokoa muda lazima gharama yake iwe tofauti.
 
Kuna maintenances na marekebisho ya kila wakati
Kuna waharibifu ambao ni nyie wenyewe yaani mpaka mshuke na kitu hamuoni raha
Mikono iliyozoea uharibifu na wizi

Yaani bora wafanye hata laki ili kila mkiharibu mlipe
Na akioza mmoja muoze wote
Hatuwezi kuwa na taifa lisilobadilika
 
Bus Dar-Dom linatumia masaa 8 mpaka 9 mnalipa 35,000 leo utumie masaa sijui 3 au 4 bado unaona 50,000 ni nyingi? Basi pandeni hayuo mabus mshinde barabarani siku nzima
Huyu ni aia ya watu wasio na uelewa kabisa! Serikali ni mali ya wananchi, inatakiwa kutoa huduma, haitakiwi kutafuta mafaida makubwa na kuumiza wananchi!
Madogo Masanja alisema walitumia umeme wa laki tatu tu kufika Morogoro na kurudi Dar, sasa hayo manauli makubwa ni ya nini?
Ni kuumiza wananchi tu bila sababu! Hii serikali haiwapendi watu wake!
 
Nini maana ya kuwa na shirika la umma?

Dar-Dodoma elfu hamsini? Badala ya elfu 20?

Bwawa la JNHEP limekilika. Umeme upo wa kutosha. Kwanini nauli ziwe juu?

=====

Kufahamu zaidi nauli za maeneo mengine soma:

Thread 'Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000' Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000
Kweli aseee tuache kulalamika jamabo lhaaaa hatuna heri hata moja ? Key board warrior
 
Back
Top Bottom