Treni ya SGR imekuja kukomboa au kudidimiza wananchi? Hayati Magufuli asingekubali nauli hizi

Treni ya SGR imekuja kukomboa au kudidimiza wananchi? Hayati Magufuli asingekubali nauli hizi

Kwani kuna mtu kashikiwa bunduki kuwa lazima apande hiyo treni? Watakaoona umuhimu wa kusave time watapanda
 
Alafuuu jamani hii ni TRRRENI sio gari moshi😂😂😂 inatumia umeme sio kama ile ya Kigoma. Ni ya kisasa zaidi ko investment yake ni kubwa mno. Afu mtu unataka ulipe 20k kweli? Tatizo watanzania tunaona kama kitu cha serikali kinatakiwa kiwe bure bure kwasab tunalipa kodi. Ni kweli tunalipa kodi lakini kodi pekee hazitoshi kuendesha hii miradi yote, lazima miradi ijilipe ili isife. Vitu vya serikali sio bure ila ni nafuu sanaa,

sasa kama wewe kwako 50k sio nafuu basi hatuna msaada na wewe panda Baiskeli tu.
 
Miradi yote inayofanywa na serikali kupitia mikopo inatakiwa kuwasaidia wananchi na sio kuwadidimiza.

Kukamilika kwa ujenzi wa bwala la Nyerere kusaidie kupunguza gharama za umeme ili mwananchi wa kawaida aweze kutumia umeme kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani, ofisini na viwandani.

Vivyo hivyo, na kukamilika kwa ujenzi wa SGR kusaidie wananchi katika nyanja ya usafirishaji. Serikali iweke ghqrama nafuu za nauli ili watumiaji wawe wengi na pesa iliyokopwa iweze kurudishwa. Kama wakikomaza mafuvu na kuweka gharama kubwa za nauli itashindwa kuendesha SGR kwa kukosa watumiaji na mwisho wa siku mradi kutokuwa na tija.
Serikali kusaidia wananchi manake ni kutenga bajeti kubwa ya ruzuku kwa TRL ili kuziba pengo la gharama ya hizo huduma za usafiri. Manake ni tozo zaidi kwa raia. TANESCO hivyo hivyo mkitaka nafuu ya malipo ya umeme. Hakuna njia ya mkato.
 
Nini maana ya kuwa na shirika la umma?

Dar-Dodoma elfu hamsini? Badala ya elfu 20?

Bwawa la JNHEP limekilika. Umeme upo wa kutosha. Kwanini nauli ziwe juu?

=====

Kufahamu zaidi nauli za maeneo mengine soma:

Thread 'Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000' Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000
Kutokana na mfumo wa uvutaji mabehewa ya treni huwezesha gharama za usafirishaji kuwa chini sana kuliko mabasi. Nauli zilizopangwa ni za uswahilini sana, ni zile za kusema watapanda tu asiyeweza shauri yake.
 
Waweke nauli elf 20, wagogo wapande na mbuzi kabisa?
 
Mnafikiria mtalipaje hayo madeni mliyotumia kujenga??
Biashara ya serikali ni tofauti na ya mtu binafsi.

Serikali inakusanya mapato/kodi, serikali inawekeza na kutoa ruzuku, serikali inafadhiliwa na kupewa mikopo kujazia pale kwenye mradi.

Mkopo unalipwa kutokana na mapato ya serikali, ruzuku inatoa kusaidia biashara ya serikali.

Nauli ikiwa 9,000 hadi Morogoro na 25,000 mpaka Dodoma badala ya behewa 4 unaunga behewa 8 hadi 12 kwa one way na hapo unaweza kuweka moja kwa mbili, yaani zinapishana kwa muda sawa.

Hapo utakusanya pesa nyingi kwa mara moja kuliko pesa nyingi kwa muda mrefu.

Tunajua tatizo lipo kwa wafanyabiashara ambao wanamiliki mabasi na maroli ambao wapo hadi huko black room, pamoja na wale wanaoiba mali ya umma.

Jiulize kwa nini gari moshi la Dar - Arusha linakufa?.
 
Back
Top Bottom