Treni ya SGR imekuja kukomboa au kudidimiza wananchi? Hayati Magufuli asingekubali nauli hizi

Kwani kuna mtu kashikiwa bunduki kuwa lazima apande hiyo treni? Watakaoona umuhimu wa kusave time watapanda
 
Alafuuu jamani hii ni TRRRENI sio gari moshi😂😂😂 inatumia umeme sio kama ile ya Kigoma. Ni ya kisasa zaidi ko investment yake ni kubwa mno. Afu mtu unataka ulipe 20k kweli? Tatizo watanzania tunaona kama kitu cha serikali kinatakiwa kiwe bure bure kwasab tunalipa kodi. Ni kweli tunalipa kodi lakini kodi pekee hazitoshi kuendesha hii miradi yote, lazima miradi ijilipe ili isife. Vitu vya serikali sio bure ila ni nafuu sanaa,

sasa kama wewe kwako 50k sio nafuu basi hatuna msaada na wewe panda Baiskeli tu.
 
Serikali kusaidia wananchi manake ni kutenga bajeti kubwa ya ruzuku kwa TRL ili kuziba pengo la gharama ya hizo huduma za usafiri. Manake ni tozo zaidi kwa raia. TANESCO hivyo hivyo mkitaka nafuu ya malipo ya umeme. Hakuna njia ya mkato.
 
Kutokana na mfumo wa uvutaji mabehewa ya treni huwezesha gharama za usafirishaji kuwa chini sana kuliko mabasi. Nauli zilizopangwa ni za uswahilini sana, ni zile za kusema watapanda tu asiyeweza shauri yake.
 
Waweke nauli elf 20, wagogo wapande na mbuzi kabisa?
 
Mnafikiria mtalipaje hayo madeni mliyotumia kujenga??
Biashara ya serikali ni tofauti na ya mtu binafsi.

Serikali inakusanya mapato/kodi, serikali inawekeza na kutoa ruzuku, serikali inafadhiliwa na kupewa mikopo kujazia pale kwenye mradi.

Mkopo unalipwa kutokana na mapato ya serikali, ruzuku inatoa kusaidia biashara ya serikali.

Nauli ikiwa 9,000 hadi Morogoro na 25,000 mpaka Dodoma badala ya behewa 4 unaunga behewa 8 hadi 12 kwa one way na hapo unaweza kuweka moja kwa mbili, yaani zinapishana kwa muda sawa.

Hapo utakusanya pesa nyingi kwa mara moja kuliko pesa nyingi kwa muda mrefu.

Tunajua tatizo lipo kwa wafanyabiashara ambao wanamiliki mabasi na maroli ambao wapo hadi huko black room, pamoja na wale wanaoiba mali ya umma.

Jiulize kwa nini gari moshi la Dar - Arusha linakufa?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…