Treni ya shirika la reli (TRC) inayoenda mikoa ya kaskazini yalaza watu porini

Treni ya shirika la reli (TRC) inayoenda mikoa ya kaskazini yalaza watu porini

Kwayu

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2007
Posts
502
Reaction score
96
Treni ya shirika la reli (TRC) inayofanya safari mikoa ya kaskazini yakwama maporini huku abiria wakikosa chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu.

Treni hiyo iliyotoka Dar jana mchana kwenda Arusha ilitarajiwa kuwasili Moshi asubuhi saa 12 leo. Ila mpaka sasa imekwama katikati ya Korogwe na Same. Mamlaka ziwaonee huruma abiria wawapelekee mabasi yawafikishe kwao.

Kuna abiria wengine ni wagonjwa wa kisukari n.k wanapata tabu sana.
 
Nilichomaanisha hapo ni kuwa na roho ya kigaidi (Roho isisyokuwa na huruma kwa walanguzi)
Hata mimi pia nimejibu kwa kumaanisha hivyo.

Unakumbuka kelele za vyuma vinebana? Je, ulibanwa na vyuma? Ulilalamika?

Kama jibu ni ndiyo, basi hutaki rais wa namna hiyo.
 
Treni ya shirika la reli (trc) inayofanya safari mikoa ya kaskazini yakwama maporini huku abiria wakikosa chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu. Treni hiyo iliyotoka Dar jana mchana kwenda arusha ilitarajiwa kuwasili moshi asubuhi saa 12 leo. Ila mpaka sasa imekwama katikati ya korogwe na same. Mamlaka ziwaonee huruma abiria wawapelekee mabasi yawafikishe kwao. Kuna abiria wengine ni wagonjwa wa kisukari n.k wanapata tabu sana.
Tanzania Railways Corp njooni huku. Mnakumbuka nilichowaambia asubuhi ya Leo?
 
Nilichomaanisha hapo ni kuwa na roho ya kigaidi (Roho isisyokuwa na huruma kwa walanguzi)
Magufuli hakuwa na upeo wa kuchanganua mambo. Nakubaliana na wewe kuwa tunahitaji kiongozi mkali na active ila afuate sheria na katiba kwenye kutimiza majukumu yake. Halafu awe na maono na atumie sayansi kuongoza na siyo mihemko.
 
Hii nchi bila kupata Kiongozi mwenye roho mbaya,Gaidi,muuwaji na mtesaji kwa walanguzi (KAMA MAGUFULI)

HAKIKA HATUWEZI KWENDA TUNAKOTAKA!
Yaani mtu mzima,unamuona magufuli wa maana labda kuliko hata babaako
 
Back
Top Bottom