Treni zote za SGR Kupewa majina ya Viongozi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio kauli mpya kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi Mh Makame Mbarawa

HATA HIVYO MIMI NAPINGA JAMBO HILO KWA NGUVU ZOTE NA NITAHAKIKISHA HALITEKELEZWI KWA SABABU HALINA MAANA YOYOTE KWA WANANCHI NA WALA HALITOSAIDIA CHOCHOTE

Majina ya viongozi yabaki kuwa mali ya familia zao kwa faida ya koo zao

Muhimu: Tunatoa wito kwa familia za viongozi walio hai na waliokufa wakatae jambo hili kwa heshima ya watu wao, Wasijiingize kwenye LAANA YA UBINAFSI
---

Treni zetu za umeme za SGR tutazipa majina mbalimbali zipo ambazo zitapewa majina ya Marais na wakuu wa Nchi kama Samia Express au Magufuli Express na zipo nyingine tutazipa majina ya vivutio kama Sengereti express ili kuzifanyia branding mtu hata ukiwa nyumbani uwe unajua unasafiri na treni gani na muda gani hivyo natoa wito kwa watanzania huu ni usafiri wetu tuutumie na tuupende"

"Treni ya umeme ya SGR itakuwa na uwezo wa kubeba hadi tani elfu 10 ambayo ni sawa na malori 500 kwa wakati mmoja na inatarajiwa kuwa itapunguza msongamano wa mizigo bandarini na kupunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara, Tanzania ndio nchi pekee Afrika yenye mtandao mkubwa wa reli ya umeme ambapo kwasasa zaidi ya kilomita 720 zimeunganishwa" - Prof Makame Mbarawa, Waziri wa Uchukuz
 
Ni upuuzi tupu.

Mbona Jalala (Dampo) Kuu la takataka la Pugu Kinyamwezi hawaligombei ili liitwe kwa majina yao??? Kwa nini??
 
Hospitali, mabwawa, madaraja, makaburi yao, mitaa, barabara na vituo vya mabasi vyote niali ya CCM! Wanatuona mazoba kwa sababu hatuna GenZ.
 
Mpaka sasa treni zote za mchongoko zilizofika zina majina ya viongozi. Treni ya kwanza kufika ilipewa jina la Nyerere Express, kisha zikafatia Samia Express, Magufuli Express nk.
 
Huyu anasema nini?
Ukiingia kwenye train zenyewe ni matangazo ya samia mwanzo mwisho hadi kero.
Hayo hayatoshi?
 
Huyu Waziri si ndiye yule alifundishwa kuvuta bangi na Magufuli , apuuzwe tu atakuwa ameshalivutatena lile la Njombe.
 
Watu wengine kujidhalilisha hawajui yaani anatangaza hadharani kabisaa sasa majina ya viongozi ya nini kwa mfano
 
Ni upuuzi tupu.

Mbona Jalala (Dampo) Kuu la takataka la Pugu Kinyamwezi hawaligombei ili liitwe kwa majina yao??? Kwa nini??
Unataka liitweje, DAMPO LA SAMIAπŸ˜‚πŸ€£

Mie sipingi miradi kuipa majina yao, majina si kitu, muhimu ni maendeleo, vitu vya maana vifanyike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…