TRIBUTE: Pumzika Lowassa. Kazi umekamilisha, umeacha alama, mwendo umeumaliza. Watanzania wazalendo tutakukumbuka daima-1



Unauonaje mwelekeo wa Taifa letu mpaka sasa? Nini mchango wa EL?

Nani alimchafua Dr. Salimu wakati wa kugombea uongozi wa juu na kwanini?

Waandishi wa habari mna mambo sana, we Paskali...pengine leo mambo yangekuwa tofauti
 
Sidhani kama CCM imebakiwa na watu 5 wa aina ya Lowasa!
Lowasa alikuwa;
sio mtu wa majungu
Sio mtu wa fitna
Sio mtu wa gilba
Sio mtu wa visasi
Sio mtu MNAFIKI
Sio mtu mwongo
Sio mtu wa kutukana
Sio mtu wa kutusi wengine
😭😭😭
RIP KOMRED LOWASA
 
"Toka kumetokea msiba wa Edward Lowassa kule Jamiiforums tukimuita kwa jina maarufu la Mwamba wa Kaskazini, ile Jumamosi iliyopita, mpaka Jana alipopumzishwa kwenye makao yake ya milele, mimi sikufanikiwa kuandika kitu chochote kumhusu Mwamba huyu, na baada ya kupumzishwa sasa ndio angalau nimeweza kutulia na kuandika kitu"

Mkuu PASKAL kwani amehifadhiwa?,sio ya kwamba ni kesho trh 17?
 
Kazi ya kwanza ni kumtafuta mtu wa kujifanya ndie cameraman wangu, nikampata nikampiga picha na kumsajili ni mpiga picha wa TBC!, Wakati wa kusaini posho, si wale jamaa wa malipo, wakaomba kila mtu aonyeshe kitambulisho cha ofisi!. Duh…nikajiuliza sasa itakuwaje?, akili ikaninijia mimi na yule mtu wangu tukaingia stashnari, tukaduru kitambulisho change, tukatoa kitambulisho kingine chenye jina ka mpiga picha halisi wa TBC lakini picha ya mtu mwingine. Mpango huu ukafanikiwa, nikavuta mpunga wa nguvu, na pesa shetani, baada ya kuzishika, yule jamaa ambaye tulikuwa tugawane, baada ya kulipwa, aliingia mitini!, kitu kibaya zidi sio kunitapeli pesa, bali alitokomea na kile kitambulisho fake chenye jina halisi la mpiga picha wa TBC

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimekuelewa, lakini PM akiwa na ziara si anatengewa bajeti?

Kwenye hiyo hiyo bajeti yawezekana mzee akamuelekeza katibu wake abane matumizi ili posho kwa waandishi ipatikane
 
Aliuchukia umaskini kwa vitendo. Edward Lowassa alikuwa hapendi njaa na hata mtu mwingine kuwa na njaa.
 
Paskali mbona wewe ni mwandishi wa habari mkongwe lakini unafanya makosa ya kitoto kitoto sana?!

Mwanzo uliandika kanakwamba Lowassa kazikwa tayari!
Nikakushauri uache Kuandika ukiwa na " Maji" kichwani! Vizuri naona ume-edit.

Sasa kituko kingine unasema akishapumzishwa ndo utaandika kitu kumhusu, ungekomea hapo basi!
Sasa umeendelea kutapika mambo mengi wakati bado hajapumzishwa!

Uandishi kama huu ambao una demonstrate lack of focus and consistency una undermine sana credibility ya waandishi wa habari wa Bongo!

Jifunzeni kwa wenzenu hapo Kenya, Mwanahabari ni Mwanahabari kweli kweli! Si utumbo utumbo kama wenu huu!!
 
Thanks Mayalla!
You telling the story/eulogy of how Lowasa changed people way of life, whatever aspect you bring to the story, that's how you and him got to interact each other! I have fallen in love with an element of funny fact that most people choose to ignore! Tupe radha tofauti ya maisha ya Ngayai katika nyanja nyingine zenye uhalisia wa maisha ya mwanadamu yeyote! Nasubiria sehemu ya pili!
 
Makala mwendelezo Lowassa alikipenda kiti moto kipindi!. Aliokoa maisha yangu Rome Italy!. He was "Of the People, By The People, & For The People!" ADIOS... AMIGOS...!.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…