Rogojin The Idiot
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 2,969
- 3,392
Pumzika Lowassa Pumzika, Kazi Umekamilisha, Mwendo Umeumaliza, Pumzika!.
Toka kumetokea msiba wa Edward Lowassa kule Jamiiforums tukimuita kwa jina maarufu la Mwamba wa Kaskazini, ile Jumamosi iliyopita, mpaka Jana alipopumzishwa kwenye makao yake ya milele, mimi sikufanikiwa kuandika kitu chochote kumhusu Mwamba huyu, na baada ya kupumzishwa sasa ndio angalau nimeweza kutulia na kuandika kitu.
Nilivyomfahamu Edward Lowassa
Kwa nature ya kazi yangu ya uandishi wa habari, nikihudumu kwenye vyumba vya Habari toka mwaka 1990 – 2020, na Lowassa alikuwa ni kiongozi, hakuna mwandishi yoyote wa Habari, hard news ambaye hakuwahi kukutana na Lowassa, hivyo nimekuwa nikim cover kwenye kazi mbalimbali za kihabari.
Siku zote na dunia nzima, Habari ni bure, hivyo sisi waandishi wa zamani, zaidi ya mishahara kwenye kazi zetu, tulikuwa tunaandika Habari bure, na japo mpaka sasa Habari bado ni bure lakini kuna Habari za bure, na kuna Habari lazima utumie gharama kuzipata ili uziandike.
Ziara za Lowas ana Kuasisiwa kwa Mishiko kwenye Sekta ya Habari.
Lowassa akiwa Waziri wa Mifugo, nikapangiwa kuzungunguka nae kwenye ziara ya kutembelea ranchi za taifa, ofisi tulilipwa fedha za kujikimu na wizara ya mifugo ilitoa usafiri. Waandishi tukahesabiwa tuko wangapi, kwa kawaida waandishi huwa hatupangiwi gari maalum bali tunabananishwa katika magari yoyote ya kwenye pool na most times huwa ni magari mikweche na tunakuwa wa mwisho kufika kwenye tukio, lakini kwenye ziara za Lowassa, waandishi tumetengewa gari maalum na sio mikweche!, gari la waandishi lilikuwa magari ya mwanzo kwenye msafara na sio mwisho. Na kila tunapokwenda tunakuta tumeisha tafutiwa mahali pa kulala hote nzuri wanazofikia viongozi, hivyo atakapo fikia yeye ndipo waandishi mtafikia na zimelipiwa!, hizo ile per diem yote ya ofisini, unakunja!. Kama hiyo haitoshi, kila jioni, unasainishwa bahasha nyingine yenye posho nene!, hivyo kwangu mimi ziara za Lowassa ndizo zilizonifungulia mishiko ya waandishi au bahasha za waandishi.
Toka wakati huo Lowassa akaagiza kwenye mikutano, semina, warsha, makongamano na ziara za viongozi, kama mnalipana posho, waandishi wa Habari nao pia ni binadamu, hivyo nao wanastahi kulipwa posho, na hapa sasa ndio bahasha rasmi za waandishi zikaasisiwa na kurasimishwa. Siku hizi kuna baadhi ya Habari, bila kuwaangalia waandishi kwa hizi bahasha za posho, hawatoi kitu, na imefikia hatua baadhi ya waandishi kuwa wawazi kama tukio halina posho, mimi sinialike!
Wiki ya Maji.
Akiwa Waziri wa Maji, aliasisi Wiki ya Maji, enzi hizo nikiwa TBC Newsroom, ukaja ofisi mwaliko wa kuhudhuria wiki yam aji, barua ikasema wajigharimie usafiri, watarejeshewa fedha zao, mwaliko ule nikampanga Mhariri nipangiwe mimi, enzi hizo Mhariri Mkuu wa TBC ni Mshana, Siku zilipokaribia nikaulizia vipi hii trip, nikaelezwa kumetokea kazi nyingine nyingi muhimu zaidi, hivyo sisi TBC hatuna mtu wa Camera Kwenda ku cover, nikamwambia mhariri mimi nina camera yangu na nita cover mwenyewe, nikapewa ruhusa.
Hapa sio kuwa najidai, mimi ndio mwandishi wa Habari wa kwanza wa Tanzania kufanya kitu kinaitwa VJ (Video Journalist). Vyombo vyote vya Habari vinatumia watu wawi mmoja ni mwandishi wa Habari ni mwingine ni mpiga picha. Mimi licha ya kuwa ni mwandishi wa Habari, pia nilikuwa ni mpiga picha, hiivyo ikitokea upungufu wa wapiga picha, naaandika Habari mwenyewe, napiga picha mwenyewe, na nikifika newsroom naingia cut to cut mwenyewe kuihariri, na baadaye naingia studio kuisoma.
Hivyi wiki yam aji nikabeba camera yangu nikasafiri kwa gharama zangu, ilikuwa Arusha, japo nilitumia usafiri w abasi, kule Arusha nikajiongeza kwa kujisajili tuko wawili na tumetumia usafiri wa ndege, ili kurudishiwa nauli nene.
Kazi ya kwanza ni kumtafuta mtu wa kujifanya ndie cameraman wangu, nikampata nikampiga picha na kumsajili ni mpiga picha wa TBC!, Wakati wa kusaini posho, si wale jamaa wa malipo, wakaomba kila mtu aonyeshe kitambulisho cha ofisi!. Duh…nikajiuliza sasa itakuwaje?, akili ikaninijia mimi na yule mtu wangu tukaingia stashnari, tukaduru kitambulisho change, tukatoa kitambulisho kingine chenye jina ka mpiga picha halisi wa TBC lakini picha ya mtu mwingine. Mpango huu ukafanikiwa, nikavuta mpunga wa nguvu, na pesa shetani, baada ya kuzishika, yule jamaa ambaye tulikuwa tugawane, baada ya kulipwa, aliingia mitini!, kitu kibaya zidi sio kunitapeli pesa, bali alitokomea na kile kitambulisho fake chenye jina halisi la mpiga picha wa TBC.
Nilirudi ofisi, nikaandika story yangu na kuwatengenezea kipindi, huku nyuma yule kanjanja wangu akiendelea kufanya ukanjanja kwenye matukio mbalimbali mbali ya kihabari kwa kujifanya ni mtu wa TBC, siku ya siku, akadakwa, akanitaja!, moto ukaniniwakia!.
Jee nini kilitokea baaya huyu jamaa kujitaja mimi ndio nilemtegengeneza kitambulisho fake cha TBC, kisa ni ili tuu kuvuta mishiko ya Edward Lowassa.
Tukutane wiki hiyo kwa sehemu ya pili ya Buriani ya Lowassa ambapo pia utakisikia kisa jinsi Edward Lowassa alivyookoa okoa Maisha ya Mtanzania mmoja huko Rome nchi Italy.
Pumzika Lowassa Pumzika!, Kazi Umekamilisha, Umeacha Alama, Mwendo Umeumaliza, Watanzania Wazalendo, Tutakukumbuka Daima, Pumzika!.
Paskali
Unauonaje mwelekeo wa Taifa letu mpaka sasa? Nini mchango wa EL?
Nani alimchafua Dr. Salimu wakati wa kugombea uongozi wa juu na kwanini?
Waandishi wa habari mna mambo sana, we Paskali...pengine leo mambo yangekuwa tofauti