Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili iliyopita.
Naendelea na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", leo ikiwa ni makala ya Tribute to certain Silent Heroes and Heroines, na kuipongeza “Idara” kwa kuwahudumia wastaafu wake hadi mwisho!” kifoni, lakini nina swali, nikiamini binadamu wote
ni sawa na watumishi wote wa serikali ni sawa, na wastaafu wote wa serikali wako sawa na wanastahili kuwa treated equal, kwa usawa sawa kabisa, kwanini wengine walipwe mafao makubwa manene manono, na kuhudumiwa hadi kifoni, huku wengine wakilipwa mafao madogo, kiduchu, membamba na siku wakifa, huachiwa familia zao tuu kupambana na hali zao?!. Kama binadamu wote ni sawa na wastaafu wote wa serikali ni sawa, they are supposed to be treated equally, kwanini Serikali yetu sikivu, inawabagua baadhi, isiwahudumie mashujaa wake wote kwa sawa sawa kwa haki sawa?.
Kwa vile tulirithi katiba sheria zetu zote, taratibu na kanuni toka kwa wakoloni, na wakoloni walitumia mfumo wa indirect rule, kuwagawa ili uwatawale, vivyo hivyo kwenye utumishi wa umma, walipanga madaraja kwa ubaguzi kuwabagua wengine kwa kuwapa umuhimu, kuwajali hadi siku wanakufa serikali inagharimia mazishi, halafu kuna wengine, inawaacha wapambane na hali zao!, huu sio ubaguzi?. Kama ni ubaguzi ambao serikali yetu imeurithi toka kwa wakoloni wazungu, je kuna haja ya kuuendeleza?, au ni ukweli kwa vile watu hawalingani, kuna wastaafu wengine ni muhimu kuliko wengine hivyo they deserves some preferential treatment hadi siku ya kifo, serikali inagharimia hadi mazishi halafu wale wasio muhimu, kuachwa kujifia na familia zao kuachiwa kupambana na hali zao?.
Ushujaa na uzalendo ni kitendo cha kufanya jambo kubwa kwa taifa lako. Mashujaa hawa wako mashujaa wa aina mbili, mashujaa wa wazi, Open Heroes & Heroines, na Mashujaa wa Kimya, “Silent Heroes & Heroines”. Mashujaa wa wazi ni wale wanaotambulika na kutambulishwa rasmi kuwa ni mashujaa, kama wale mashujaa wa majeshi yetu, ya JWTZ, Polisi, Uhamiaji, Magereza na Zimamoto, ambao huvishwa nishani za ushujaa, wazi wazi huku vyombo vya habari vikialikwa. Lakini mashujaa wa "Idara" wenyewe pia wanavishwa nishani, ila wanavishwa kimya kimya kwenye makambi yao no media publicity!.
Jumamosi iliyopita, tarehe 05/02/2022, katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo Moshi, (kiko mbele ya Himo kuelekea Moshi mjini unapandia Kawawa Rd)tumempumzisha kwenye makao yake ya milele, mmoja wa mashujaa hawa, “silent heroines” wa "Idara", kwa jina la Graciana Morris Kundi, amehifadhiwa baada ya kufariki dunia peacefully akiwa usingizini na umri wa miaka 86.
Kufuatia unyeti wa "Idara" japo sijui Graciana Morris Kundi, alifanya ushujaa gani, ila Mwaka 1985 alitunukiwa nishani ushujaa na rais Nyerere, kisha mwaka 1991 akatuukiwa tena nishani nyingine ya ushujaa na rais Mwinyi.
Graciana Morris Kundi, alizaliwa tarehe 30/09/1936 katika kijiji cha Iwa Kirua Vunjo, Moshi. Kati ya 1944-1949, alipata elimu ya Msingi, shule ya Iwa. Mwaka 1950-1954 - akaendelea na masomo ya sekondari Ndala, Kipalapala Tabora. 1955-1958 akajinga Tabora Girls. Mwaka 1960 akajiunga na Chuo cha KNCU kusomea kozi ya Stenograph. Mwaka 1961, aliajiriwa rasmi serikalini, na kufanya kazi hadi kustaafu mwaka 1992, ikiwa ni amelitumikia taifa kwa miaka 31.
Baada ya kustaafu, alirudi kijijini, Kirua Vunjo Moshi, na kuishi maisha ya kawaida hadi mauti yalipomkuta, Jumatano ya tarehe 02/02/2022 kwa kufariki akiwa usingizini na kuzikwa Jumamosi ya tarehe 5/2/2022 kwenye shamba lake, kijijini kwake Uparo Kirua Vunjo Moshi.
Japo huko nyuma, nimewahi kuilaumu "Idara" kwa haya TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! lakini kwa hili la Idara kundelea kuwajali watumishi wake wastaafu miaka yao yote ya maisha yao, hadi kifoni, Idara inastahili pongezi, kwani baada ya Idara kupokea taarifa ya kifo hicho, maofisa wa Idara, walifika nyumbani na kutoa rambirambi kubwa nene ya kutosha kugharimia mazishi.
Kama nilivyosema, sikuujua ushujaa wa mama huyu zaidi ya kuvishwa Nishani na Rais Nyerere na rais Mwinyi. Kikawaida majeshini, wale wanaovishwa nishani na CinC in personal ni maofisa wa ngazi za juu. Wale maofisa wa ngazi za chini, huvishwa nishani na wakuu wa vikosi vyao. Hivyo Graciana Morris Kundi, itakuwa ni alikuwa ofisa wa juu wa idara ila hadi kifoni, sikuwahi kumjua alikuwa nani.
Kwa vile nimetokea kufahamu kiwango cha pensheni aliokuwa akilipwa, na kwa vile nayafahamu mafao ya kisasa ya viongozi wakuu wanapostaafu, hulipwa asilimia 80% ya mshahara wa ofisa aliye madarakani, hivyo wastaafu hawa, waliolitumikia taifa miaka yao yote na maisha yao yote, nao wana haki ya pensheni zao zipangwe kwa asilimia, ili mishahara ya ofisa wa ngazi yake ikipanda, na pensheni za wastaafu hawa nazo zipande. Mwalimu Nyerere aliamini katika falsafa ya binadamu wote ni sawa, na baada ya kuwa rais wa Tanzania, akakuta jinsi mshahara wake ulivyokuwa juu kulinganisha na wengine, aliupunguza mshahara wake ili kujenga usawa.
Kama ni kweli binadamu wote ni sawa, hivyo maofisa wa ngazi zote za serikali ni sawa na wanastahili kutendewa haki sawa. Iwaje maofisa
wakuu tuu ndio wanajipangia mafao makubwa, manene, manono ya kustaafu kwa kiwango cha asilimia 80% ya ngazi husika, halafu kwanini wastaafu wengine, wa zamani, wanalipwa mafao madogo, kiduchu ajabu?. Kama ni kweli tunamuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwenye usawa wa binadamu, maofisa wote wa serikali, wanapaswa kutendewa haki sawa na wengine, na sio haki kwa maofisa wakuu tuu halafu wengine, kuachwa kupambana na hali zao, huu ni ubaguzi!.
Nimeipongeza Idara kwa kuwajali Wataafu wake sio tuu kwa kuendelea kuwalipa maisha yao yote, toka uhai, hadi kifoni, kwanini ni baadhi tuu ya wastaafu na sio wote?. Wastaafu wengine wanaojaliwa na serikali hadi kifoni, ni majaji wastaafu, na hili la majaji pia niliwahi kulizungumzia humu Hongera Jaji Mkuu kutumia uadilifu wa kaisari, kwanini Majaji wastaafu hawatibiwi?, wanasubiriwa wafe tuu? na sio mahakimu au watumishi wengine wa mahakama, swali ni kwanini, baadhi tuu ndio wajaliwe hadi kifoni, lakini wengine waachwe wajifie na hali zao?, Huu sio ubaguzi fulani hivi?.
Watu wanapojiunga na idara fulani ya serikali, na kuitumikia serikali maisha yao yote hadi kustaafu, kitendo tuu cha kufanya kazi serikalini maisha yao yote, na viwango duni vya mishahara ya serikali, hilo pekee tuu ni ushujaa. Hivyo watumishi wote wastaafu wa serikali, ni mashujaa kimya, “silent heroes”, kama walijitoa kuitumikia serikali maisha yao yote, japo wanalipwa pensheni kiduchu, lakini inapofika kifoni, serikali, inyooshe mkono wake kuwajali hadi kifoni katika safari yao ya mwisho.
Kuna msemo usemao, “mwana wa nyoka ni nyoka”, I has happened wazazi wangu wote wawili walikuwa wanafanya kazi ofisi moja, hivyo kwa watu wanao nifahamu mimi Pascal Mayalla, kama mwanahabari jasiri, asiyeogopa, kumuuliza kiongozi yoyote swali lolote, ujasiri huo nimeurithi kutoka kwa Silent Hero Baba yangu Mzee Andrew Mayalla na Heroines huyu, Graciana Morris Kundi, kwasababu huyu ni mama yangu mzazi!.
Kwa Baba Mzee Andrew Mayalla (RIP), kwake nimerithi tabia zake nzuri fulani za Kisukuma ambazo naomba nisizitaje hapa maana....
Kwasababu enzi hizo recruitment ilikuwa inafanywa kwa walio in service kupeleka majina ya watoto wao kuwa recruited, sisi tumezaliwa 8, we can't all be recruited, mimi najizungumzia mimi kama mimi kuwa I'm not, ila kitu nilicho jaaliwa kuwa nacho kutoka kwa wazazi wangu ni ile natural intelligence mind ya kwenye damu, hivyo vitu ninavyoshaurigi humu, kama ushauri huu
Kwa niaba ya Familia ya Shujaa huyu mwanamke,
SHUKRANI
Wasalaam.
Paskali

- Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?
- US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali?
- Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?