Trilioni 16 Vs Bilioni 700

hivi Jusa na Maalim Seffu huwa wanakujaga naye jf!?
 


NB: Sikubaliani na wewe naona wewe ni ANTI-Tanganyika......Lazima tupate Tanganyika yetu
 
Ndoto za ujio (kurudi?!) wa Sultan kama mkombozi wa kiuchumi na kisiasa wa Zanzibar.
 
nchi tajiri zinawaza kuungana,sisi tunawaza kupeana talaka,aibu sana,Nyerere aliona mbali na akaacha usia kuhusu hii dhambi ya ubaguzi na lazima itatutafuna tu
Ni kweli kuwa umoja ni nguvu! Lakini inapotokea katika umoja huo hakuna maelewano basi ni heri kutengana!

Viongozi wa Zanzibar wanatamani nchi yao iwe dola kamili; ili wawe na amiri jeshi, wawe na kiti umoja wa mataifa, wawe na mabalozi wao nje nk! Haya ni matamanio ya ubinafsi!

Hata huko Ulaya katika nchi zilizo katika muungano wa Euro wamefika mahala wanataka kuwatenga wenzao wa kusini kwa kushindwa kuwajibika kusimamia uchumi wa nchi zao na kusababisha fedha ya Euro kuingia matatani!
 

kwani sisi hatuna gesi yetu ? Mbona mapato yetu ya dhahabu tunatumia wote ?
Kama hamtaki muungano tokeni,kwani sisi tunakula kwenu ?
Msepe tu
 

Tume ya Warioba imekuja na mahesabu haya:
Swali: Gharama za uendeshaji wa Serikali hizi utakuwaje, huoni kama Rais wa Muungano atategemea zaidi fedha na msaada kutoka Tanganyika na Zanzibar?


Warioba: Katika Katiba ya sasa mapato ya Muungano yanatokana na vyanzo vitatu, Kodi ya Mapato (income tax), Ushuru wa Forodha (custom duty) pamoja na ushuru wa bidhaa (excise duty).


Kodi ya mapato ndiyo inatoa fedha nyingi sana na inafuatiwa na kodi ya ushuru wa bidhaa na ushuru wa forodha. Kutokana na hesabu tulizopiga, tumeona matumizi katika Serikali ya Muungano yapo katika sehemu mbili, moja ni yale ya Muungano na ya pili ni yale ya Tanganyika ambayo yanachukua fedha nyingi.


Mwaka 2010/2011 mapato ya kodi ya mapato yalikuwa Sh2 trilioni na mapato ya ushuru wa bidhaa yalikuwa Sh1trilioni na mapato ya ushuru wa forodha yalikuwa Sh600 bilioni.


Ni kwamba matumizi ya mambo ya Muungano yalikuwa chini ya Sh1trilioni, ndiyo maana tumechagua ushuru wa bidhaa, kwani tukipata fedha zile zitaweza kumaliza matumizi yote ya Serikali ya Muungano.


Hivyo basi kama tukiendelea na utaratibu huu wa Serikali tatu, ni wazi kwamba Serikali ya Muungano haitakuwa na haja ya kukopa fedha kwa kuwa itakuwa nazo za kutosha,......

Chanzo Warioba: Serikali ya Muungano haitakopa fedha - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Kwa mahesabu haya, Serikali ya Muungano itatumia chini ya Trilioni 1....Usisahau pia mambo ya muungano pia yanaingiza fedha sio kuwa yanatumia fedha tu.(Mapato na matumizi). Wengi tunajikita katika matumizi tu bila kuangalia mambo ya muungano yanaingiza mapato kiasi gani.


Upo uzi huu pia ambao ulitoa changamoto ya matumizi ya shughuli za mambo ya muungano na serikali shirikishi.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiinimacho-cha-muungano.html


Lakini hatuhitaji serikali tatu. Mwalimu alisema kama kutakuwa na EAC ambayo imeazimia kuunda Shirikisho la Kisiasa basi kupunguza utata,kufanya urahisi wa mambo tuwe na serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar tu.

Mwalimu alisema haya mwaka 1994:

Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.Uk 11-12 link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
 
Kwanza la kujiuliza je wananchi wanautaka muungano?
 
Nimekasirika sana jana nilivyokua naangalia habari i.t.v,,nakumbuka miaka miwili mitatu nyuma kulikuwa na tetesi znz kuna gesi,wale watu walitaka kuvunja muungano na kusisitiza gesi ni ya wa znz na sio wabara,,,,sasa hivi gesi yao haijapatikana na yetu imepatikana wanaanza kuuliza eti watanufaika vipi na gesi yetu?,,kikubwa we should let them go and see the results,,,,
am a proud Tanganyikan
 

215. Vyanzo vya mapato ya Serikali ya Jamhuri yaMuunganovitakuwa:
(a) ushuru wa bidhaa;
(b) maduhuli yatokanayo na taasisi za Muungano;
(c) mchango kutoka kwa Washirika wa Muungano; na
(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano.
 

huo ushuru wa bidhaa zinazoagizwa na Bara ni kiasi gani na zinazoagizwa na wazanzibar ni kiasi gani, ndipo tuzichanganye na kuona hiyo trillion moja inatoka wapi? maana tusizungumzie tu kwamba zinazo hitajika ni trillion 1, wakati wenzetu kwenye serikali ya muungano wanataka 15:15, ubalozini wanataka nafasi, siwa nk wakati kuchangia hawawezi, mimi nafikiria ile formular ya 40m:2m ifuatwe au ile ya imf ya 4.5% Zanzibar 94.5% bara au Tanganyika
 

Mimi naungana na Mwalimu Nyerere. Umeuona ushauri wake hapo juu?

Hatuhitaji serikali tatu. Tunahitaji serikali mbili tu, ya Tanganyika na Zanzibar. EAC ndio kiungo kitakacholeta shirikisho la Afrika Mashariki(Muungano).
 
215. Vyanzo vya mapato ya Serikali ya Jamhuri yaMuunganovitakuwa:
(a) ushuru wa bidhaa;
(b) maduhuli yatokanayo na taasisi za Muungano;
(c) mchango kutoka kwa Washirika wa Muungano; na
(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano.

Kama umesoma hayo majadiliano ya mwandishi na jaji Warioba,utagundua kuwa hivyo vifungu b,c,d havitakuwa na ulazima. Ndio sababu Warioba alisema serikali ya Muungano haitohitaji kukopa na itakuwa na fedha za kujiendesha za kutosha na kuwa na ziada.
 
Kama umesoma hayo majadiliano ya mwandishi na jaji Warioba,utagundua kuwa hivyo vifungu b,c,d havitakuwa na ulazima. Ndio sababu Warioba alisema serikali ya Muungano haitohitaji kukopa na itakuwa na fedha za kujiendesha za kutosha na kuwa na ziada.
Nadhani kuna hoja hapa haizingatiwi!

Serikali ya muungano ya sasa kwa kiasi kikubwa inagharimiwa na Tanzania Bara na hivyo siyo rahisi kuiainisha au kuichanganua kwa usahihi!

Serikali ya shirikisho inayopendekezwa na rasimu ya katiba mpya itakuwa na mawaziri wasiozidi 15, kwa maana hiyo itakuwa kubwa kuliko ilivyo sasa kwa kuwa itakuwa na rais wake na makamu wa rais wake; itakuwa na mahakama yake na mwanasheria mkuu wake; itakuwa na bunge lake na polisi wake; Aidha JWTZ itakuwa chini ya serikali hii ya shirikisho!

Kwa kifupi serikali ya shirikisho itahitaji fedha nyingi kujiendesha na si hiyo trilioni 1! Hivyo vyanzo vyote vilivyoorodheshwa hapo juu vitahitajika!
 
Kweli mkuu. Hata mimi mara nyingi nawaza hivyo. Kuwe na serikali ya Tanganyika na kuwe na serikali ya Zanzbar. Huo muungano wala hauna haja. Kama bado tunapendana kwani hatuwezi tukakutana au kushirikiana kwenye EAC au SADC!
Mimi naungana na Mwalimu Nyerere. Umeuona ushauri wake hapo juu?

Hatuhitaji serikali tatu. Tunahitaji serikali mbili tu, ya Tanganyika na Zanzibar. EAC ndio kiungo kitakacholeta shirikisho la Afrika Mashariki(Muungano).
 
jitoeni sasa!!!!
na watu wenu wajiandae kurudi mapema. wapemba ambao wametapakaa kila kona ya bara, wapemba maarufu kwa maduka makubwa huku na majumba bara, naombeni mjitoe mapema--la sivyo hamtarudi na kitu pemba, vijana wetu wanaokabiliwa na umaskini mkubwa wnayahitaji hayo.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…