Trilioni 16 Vs Bilioni 700

Trilioni 16 Vs Bilioni 700

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Endapo rasimu ya katiba mpya itapitishwa na wananchi na hivyo kuwepo kwa serikali tatu basi kitakachoiua serikali ya muungano ni rasilimali fedha!

Bajeti ya Tanzania bara ni takribani trilioni 16 na bajeti ya Zanzibar ni pungufu ya bilioni 700! Kwa serikali zote mbili fedha hizi hazitoshi!

Sasa je serikali hizi mbili zitamudu kuchangia serikali ya muungano pamoja na taasisi za kimataifa ambazo serikali hizi zitakuwa wanachama?! Na mchango wa serikali hizi mbili kwa serikali ya muungano utakuwaje?!

Kwa vyo vyote vile mchango ukiwa sawa Zanzibar haitaweza! na Kama Tanzania bara(Tanganyika) itachangia zaidi basi Zanzibar itajikuta inamezwa jambo ambalo Zanzibar haitakubali!

Hakika sasa ni wazi kifo cha muungano kinaandaliwa na kwamba kuna uwezekano mkubwa serikali ya muungano ikafa miaka michache baada ya kuundwa!!
 
Ndo maana tunadai serikali moja! Uchumi wa Visiwa hivi ni mdogo sasa! Kama Rhode Island unalingalisha California.

Uchumi wa bara ni mara 22 ya ule wa Visiwani!!!

Ndo maana muda wote bara kiuchumi ktk Wizara za Muungano ilibeba visiwani! Viswani hawana cha kuchangia!

Jibu serikali moja!!!

Tofauti na hapo kila nchi na mamlaka yake kamili!
 
Serikali moja nchi moja, km itakua nchi moja inayotokana na Tanganyika na ZNZ sawa, pia km ni nchi moja inayotokana na Tanganyika pekee sawa.
 
Niliposikia hili la bn 700 I was shocked. Sasa katika hali kama hii tumeshawabeba sana halafu hawana shukrani badala yake wanatulaumu? Let them go. When they are gone tutajipanga upya kama Tanganyika na kufurahia maisha.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hizo Trillion 16 ni budget ya serikali ya Tanzania au Tanganyika?
 
Hivi mumeshawahi kulinganisha mapato ya nchi kama Ujerumani na Uholanzi? Hivi mumeshawahi kulinganisha mapato ya Burundi na Kenya? tofauti ya mapato yanakujaje hapo? Mtu si ana contribute kile atakachotumia kwenye muungano?
 
trilion 16= billion 16,000=million 16,000,000
idadi ya watanganyika 44million
ukigawa unapata wastani wa 36,3636.Tsh kwa kila mtu
watanganika wamewazidi wazanzibar kwa mara 31

trilion 0.7 =700bilion=million700,000
idadi ya wazanzibar 1.4million
ukigawa unapata wastani wa 500,000 Tsh kwa kila mtu
sasa tunaukataa muungano kihesabu huenda mkaelewa zanzibar ikiwa nje ya muungano itakusanya kodi zote yenyewe ikiwemo 50$ za visa,leseni za mabenki,kodi ya ushuru wa bidhaa,kodi ya mapato,ushuru wa forodha,leseni za viwanda nk....tunategemea baada ya miaka miwili bajeti ya znz itafikia 1trillion pamoja namikopo na misaada ya nje ambayo hatutakumbana na vikwazo nya bara tena. kuna ongezeko la gharama za uendeshaji lkn hilo litakua ndani ni mzunguko wa kiuchumi ndani fedha itakayotumika kulipa itazunguka ndani. hatujaaza kuingia kwenye mafuta na gesi iliyojazana baharini ambayo mliitaka sana watanganyika...tushafanya hesabu mnatuchelewesha na jinchi lenu kubwa sana limejaa ufisadiiiii
ZANZIBAR BILA MUUNGANO INAWEZEKANA
 
Endapo rasimu ya katiba mpya itapitishwa na wananchi na hivyo kuwepo kwa serikali tatu basi kitakachoiua serikali ya muungano ni rasilimali fedha!

Bajeti ya Tanzania bara ni takribani trilioni 16 na bajeti ya Zanzibar ni pungufu ya bilioni 700! Kwa serikali zote mbili fedha hizi hazitoshi!

Sasa je serikali hizi mbili zitamudu kuchangia serikali ya muungano pamoja na taasisi za kimataifa ambazo serikali hizi zitakuwa wanachama?! Na mchango wa serikali hizi mbili kwa serikali ya muungano utakuwaje?!

Kwa vyo vyote vile mchango ukiwa sawa Zanzibar haitaweza! na Kama Tanzania bara(Tanganyika) itachangia zaidi basi Zanzibar itajikuta inamezwa jambo ambalo Zanzibar haitakubali!

Hakika sasa ni wazi kifo cha muungano kinaandaliwa na kwamba kuna uwezekano mkubwa serikali ya muungano ikafa miaka michache baada ya kuundwa!!

Mbona huu wasiwasi ni wa bure! Mnapozungumza gharama za serikali tatu mnatakiwa mjuwe kuwa Serikali ya zanzibar tayari ipo na inajihudumia. Itakapoundwa serikali ya Tanganyika kitachofanyika ni kuwa serikali hiyo italipia yale mambo yanayohusu Tanganyika tu.
Kuna mambo ambayo yatakuwa ya Muungano haya Serikali ya Tanganyika na ile ya Zanzibar hazitokuwa na wajibu wa kuyashughulikia. Yatabaki mambo ya Muungano ambayo haya ndio yatashughulikiwa na serikali ya Muungano.
Mambo haya ya Muunganokwa sasa hayamo katika gharama za serikali ya Zanzibar hivyo itakuiwa pia kwa serikali ya Tanganyika. Hata hivyo ikumbukwe kuwa mambo haya ya Muungano hivi sasa yanagharamikiwa na ile Serikali Mseto ya Tanzania/Tanganyika na kwa maana hiyo haitakuwa gharama mpya yatakapokuwa yanagharamikiwa na Serikali ya Muungano.

Kuhusu la kuchangia gharama za Serikali ya Muungano bila shaka proposition itabidi itumike. Nikitowa mfano wa Wizara ya Mambo ya Nje kule Zanzibar idara labda ina wafanyakazi 10 tu, Wizarani Wazanzibari hawatimii 10 na nje Mabalozini pengine 10. Sasa ukichukuwa idadi kamili ya wafanyakazi wa Mambo ya nje wapatao tuseme 500, utategemea Zanzibar ilipe sawa na Tanganyika? Hali hii ni kwa kila sehemu ya Wizara za Muungano.
Katika mfumo wa sasakuna mambo mengi yanayopoteza fedha kwa hili la kungangania mfumo wa serikali mbili. Wabunge wa Zanzibar wanapokea fedha za bure kule Bungeni ambapo asilimia 80 ya mambo ni ya Tanganyika. La kutisha zaidi wabunge hawa wanachaguliwa katika kamati zisizowahusu na kuwafanya kuwasemea Watanganyika na huku mambo ya Zanzibar yanazungumzwa na Wazanzibari wenyewe watupu.

Umoja ni moyo na kama kweli kuna moyo wa umoja basi umoja unanoga zaidi kwa wale wanaojitegemea lakini mmoja kumtegemea mwenzake si umoja bali ni ukujidhalilisha basi.

trilion 16= billion 16,000=million 16,000,000
idadi ya watanganyika 44million
ukigawa unapata wastani wa 36,3636.Tsh kwa kila mtu
watanganika wamewazidi wazanzibar kwa mara 31

trilion 0.7 =700bilion=million700,000
idadi ya wazanzibar 1.4million
ukigawa unapata wastani wa 500,000 Tsh kwa kila mtu
sasa tunaukataa muungano kihesabu huenda mkaelewa zanzibar ikiwa nje ya muungano itakusanya kodi zote yenyewe ikiwemo 50$ za visa,leseni za mabenki,kodi ya ushuru wa bidhaa,kodi ya mapato,ushuru wa forodha,leseni za viwanda nk....tunategemea baada ya miaka miwili bajeti ya znz itafikia 1trillion pamoja namikopo na misaada ya nje ambayo hatutakumbana na vikwazo nya bara tena. kuna ongezeko la gharama za uendeshaji lkn hilo litakua ndani ni mzunguko wa kiuchumi ndani fedha itakayotumika kulipa itazunguka ndani. hatujaaza kuingia kwenye mafuta na gesi iliyojazana baharini ambayo mliitaka sana watanganyika...tushafanya hesabu mnatuchelewesha na jinchi lenu kubwa sana limejaa ufisadiiiii
ZANZIBAR BILA MUUNGANO INAWEZEKANA

Pole sana , Hujuhi kuwa katika hizo 0.7 tril. 0.68 zinatoka bara kama msaada na nyinyi makusanyo yenu ni 0.12 tril kwa mwaka.

Uchumi wa kila mtu 500,000/= muutoe wapi? Mngekuwa nao huo saa hizi si mgeshanzisha vita.
 
huu ni uwongo..angalia bajeti ya muungano kuna fedha hii wapi inayopelekwa zanzibar ....nambie ni wizara gani kifungu kipi kwenye bajeti 2013/14 ya tanzania. nikikiona sito pinga tena muungano na nitaazisha vuguvugu la wapenda muungano...
thubutu kwa mapenzi gani mliyonayo kwa zanzibar rabda iwe ni mishahara ya majeshi ya kikoloni mloyaweka znz.
mm sikatai ukweli niambie niangalie haraka
 
Pia kumbuka kuna Wazanzibari wengi wameajiriwa huku bara katika sekta ambazo si za muungano!
 
Exactly!
Hata Waziri wa Afya huku Bara kwa sasa ni Mzanzibari na analipwa pesa na Wizara isiyokuwa ya Muungano ingawa ni Mbunge toka Zanzibar!

​Siyo hivyo tu pia amewahi kuwa mbunge huku bara!
 
nchi tajiri zinawaza kuungana,sisi tunawaza kupeana talaka,aibu sana,Nyerere aliona mbali na akaacha usia kuhusu hii dhambi ya ubaguzi na lazima itatutafuna tu
 
Niliposikia hili la bn 700 I was shocked. Sasa katika hali kama hii tumeshawabeba sana halafu hawana shukrani badala yake wanatulaumu? Let them go. When they are gone tutajipanga upya kama Tanganyika na kufurahia maisha.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Si mkaungane na kenya wenye bajeti sawa na tanganyika.
 
Back
Top Bottom