True story: Babu yangu kama mshikaji wangu (2)

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu (2)

Sehemu ya 4

Babu yangu mzee bhuhabhi alimwelezea tatu ubaya wote wa yunge pamoja na washirika wake kuwa walipanga njama za kunila nyama mimi pamoja na kijana mmoja ambae nilieleza huko nyuma kuwa mtoto wake alikamatwa na fisi wa kimiujiza huku mama yake mzazi akihusika na fisi yule.

Ndipo mwisho kabisa babu alimwomba tatu moja kati ya pembe tatu zilizokuwa chini ya mtungi mkubwa wa maji ya kunywa uliokuwepo sebleni nyumbani kwao tatu.

Nilimwona tatu akipigwa bumbuwazi huku hofu na mashaka yakimjaa usoni mwake kutokana nayale aliyoyasema babu,
Babu kwetu hakuna vitu hivyo unavyovisema na wala sivielewi kabisa, aliongea tatu kwa sauti ya uwoga sana.

Sikia mjukuu wangu, hapa sio siri tena, bila kufanya hivyo utampoteza mwenzako huyu na kijiji chetu kitakuwa cha misiba kila kukicha, hivyo ondoa shaka nikimaliza tu kazi hii ya kuwanyoosha hawa washenzi, nakurudisha upembe wako, alisihi babu.

Tatu alijiinamia akifikiri, kisha aliinua uso na kusema, hapana babu, mimi sijui mambo hayo.

Upotayari kumpoteza huyu?
 
Sehemu ya 5

Babu alimwuliza tatu huku akioneshea kidole kwangu.

Sikiliza tatu nikwambie, kabla ya bibi yako kufariki, alikuwa mtu wangu wa karibu sana na mambo kama haya tulisaidizana, alikuwa mshirika wangu katika kukomesha vitendo vya uonevu, tulikuwa na siraha 4 za kujikinga na maadui na kuwazuia pale tulipopaswa kufanya hivyo, kati ya siraha hizo, tatu alikuwa nazo yeye bibi yako na moja nilibaki nayo mimi, alieleza babu na kuuliza,

Je umesahau kama mimi na bibi yako tulivyokuwa tukisemwa kwa uchawi hapa kijini mpaka bibi yako alivyofariki jina hilo uchawi likabaki kwangu? Najua hata wewe unaamini mimi ni mchawi, lakini uelewe kwamba, watu wa hapa kijijini walianza kuupakaza sifa mbaya mimi na bibi yako, ila ukweli ni kwamba, tuliwazuia wasifanye uonevu wao kwa watu wasokuwa na hatia, lakini kifo cha bibi yako kilinifanya nikakosa nguvu ya kukabiriana nao kwani siraha niliyonayo haijakamilika, alieleya babu mpaka jasho likawa linamtoka.

Naomba msaada wako mwanangu tukomeshe huu upuuzi, alisihi babu.
 
Sehemu ya 6

Hapa nilijifunza ukiwa mchawi usiwe mwepesi wa kukubali kwamba unajihusisha na mambo hayo, kwani licha ya msichana tatu kubanwa na kuelezwa kinagaubaga, aligo kwamba haelewi chochote juu ya vitu vilivyofukiwa chini ya mtungi wa maji sebuleni kwao.

Uso wake ulionesha mambo anayoelezwa na babu yanaukweli, lakini tatu alishikiria msimamo wake kwamba hajui chochote, mpaka inagota saa 12 hatukuwa tumefanikiwa kumshawishi tatu.

Mpaka najuta ninani alinituma likizo hii nije huku kuja kuliwa nyama,
Niliongea tukiwa wawili na tatu tukitembea kurudi nyumbani mara baada ya jitihada za babu kumshawishi tatu atuazime makombora ya kuwadungua walozi.

Wakati huu tukiwa tumemwacha babu kule mbugani amejiinamia bila matumaini.

Nzehe nikwambie ukweli mambo hayo mie siyatambui kabisa, alisema tatu.

Basi sawa, niliongea kwa kukata tamaa huku machozi yakinishuka, nilijiona ninanafasi ya kumshawishi tatu mpaka akubali kuupa ile mitambo ya maangamizi ikafanye kazi ipaswavyo.

Inamana yunge anataka kula nyama yako?
 
Sehemu ya 7

Aliniuliza tatu huku sasa tukiwa tumefika pale njia zinapo tawanyika, moja kuelekea kwao tatu huku nyingine ikielekea kwetu.

Tatu mchumba, yote aliyokuambia babu yanaukweli kabisa na kama tukichelewa kidogo tu utanikosa mmeo, nilitia huruma mbele za tatu lakini tatu aliweka ngumu na hapo nilijiona kumbe sipendwi kabisa.

Basi sawa usiku mwema, nilisema kwa hasira huku nikianza kupiga hatua kwa haraka kuelekea nyumbani, masikio yalikuwa nyuma kusikiliza labda huenda tatu ataniita na kuniambia kwamba alikuwa amekubali kutupatia tulichokuwa tunataka, lakini wapii, nilijidanganya.

Umeona wenzio waliokwiva kwenye haya mambo? Aliniuliza babu tukiwa ndani mwangu usiku huu wa saa 5 mara baada ya kuwa tumekula chakula cha usiku.

Babu huyu msichana hanipendi nimegundua kwani richa ya kumsihi huku nikilia machozi kwamba naenda kuliwa nyama na yunge, lakini kagoma kabisa, yaani sitaki hata kumwona mbele yangu, niliongea kwa hasira.

Hapana usiseme hivyo mdogo wangu, unajua yule binti hatuamini kabisaa!
 
Sehemu ya 8

Nafikiri bibi yake hakuwahi kumwambia ushirika tuliokuwanao baina yetu, ila yule binti aliachwa amekwiva kabisa, japo macho yake kidogo bado hayajakomaa kukabiliana na ukweli, alisema babu.

Huyu kwakua amekataa kutoa msaada, sio mbaya sana kwani hata siraha niliyokupa juzi inaweza kutusaidia katika vita, kikubwa ni utayari wako na umakini tu, utaweza kuwakomesha hawa wote, alisema babu jambo lililonipa wasiwasi.

Kwamba utayari wangu utaweza kukisambaratisha kilinge chote cha kina yunge, bibi na wenzao wote? Niliikumbuka siku ile ya kwanza nilipopelekwa kule na yunge, ule wingi wao pamoja na mafisi, mabundi na mapaka makubwa ningeweza kukabiliana nao tena kwa siraha ambayo hata babu mwenyewe alionekana kuwa na mashaka nayo?

Kazi hii tunaianza leo, hakuna kulala kwani inaoneka leo yunge na watu wake wanajambo kubwa ambalo litaleta mtikisiko na litatuathiri hata sisi, hivyo jiandae kwa mapambano, nakwenda kulala na ifikapo saa 7 usiku nitakuja.

Aliondoka babu na kuniacha na wasiwasi mwingi sana.
 
Tuliishia hapa Funny boe
 
Nilikuwa naifatilia kabla hata hujabadili jina na kujiita Mafisango Chama, kwa kweli ulizingua ukatuacha inanifanya hamu ya kufatilia nikose sababu unaweza kutuacha tena halafu episode fupi yaani episode 4 fanya iwe moja.
 
Sehemu ya 9

Nilijiegesha kitandani, mawazo yalizonga, nilijaribu kuvuta picha itakuwaje kwenye uwanja wa vita dhidi ya yunge, bibi na watu wengine wengi wenye uchu na nyama za watu? Huku sio kujitaftia matatizo kweli? Niliwaza.
****

Nilishtuliwa na babu akinitikisa niamke haraka, nilikurupuka nikidhani muda wa kwenda kufanya maangamizi ya yunge na washirika wake sasa umewadia, lahaulaa! Nilijidanganya hakika, kulikuwa kumekucha tena jua limechomoza, niliangaza huku na kule, yalikuwa mazingira tofauti na ndani nilimokuwa nimelala.

Tulikuwa makaburini asubuhi ile, niliogopa sana, yani nilale ndani usiku, ila kunakucha nimelala makaburini? Nilishangaa na hofu ilinikamata vibaya mno.

Tuondoke haraka, aliamrisha babu aliyeonekana kuchanganyikiwa na kitendo kile,
Hawa wajinga wametushtukia, na hali itakuwa mbaya sana, wametuwahi, alisema babu kwa masikitiko.

Kwani imekuaje babu, maana jana uliaga kwamba saa 7 ungerudi ili tukainze kazi yetu, ukaniacha ndani nmejilaza, inakuwaje kunakucha tupo makaburini? Dah!
 
Funny boe jamaa kakuzingua hukuuuu
 
Back
Top Bottom