Pettymagambo
JF-Expert Member
- Aug 21, 2017
- 1,490
- 8,227
- Thread starter
- #61
Sehemu ya 4
Babu yangu mzee bhuhabhi alimwelezea tatu ubaya wote wa yunge pamoja na washirika wake kuwa walipanga njama za kunila nyama mimi pamoja na kijana mmoja ambae nilieleza huko nyuma kuwa mtoto wake alikamatwa na fisi wa kimiujiza huku mama yake mzazi akihusika na fisi yule.
Ndipo mwisho kabisa babu alimwomba tatu moja kati ya pembe tatu zilizokuwa chini ya mtungi mkubwa wa maji ya kunywa uliokuwepo sebleni nyumbani kwao tatu.
Nilimwona tatu akipigwa bumbuwazi huku hofu na mashaka yakimjaa usoni mwake kutokana nayale aliyoyasema babu,
Babu kwetu hakuna vitu hivyo unavyovisema na wala sivielewi kabisa, aliongea tatu kwa sauti ya uwoga sana.
Sikia mjukuu wangu, hapa sio siri tena, bila kufanya hivyo utampoteza mwenzako huyu na kijiji chetu kitakuwa cha misiba kila kukicha, hivyo ondoa shaka nikimaliza tu kazi hii ya kuwanyoosha hawa washenzi, nakurudisha upembe wako, alisihi babu.
Tatu alijiinamia akifikiri, kisha aliinua uso na kusema, hapana babu, mimi sijui mambo hayo.
Upotayari kumpoteza huyu?