Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mambo hayoooo...69
Shangwe zililipuka na kumfanya yule mwanamke azidishe madoido na majigambo kuonesha ushujaa wake.
Alimtundika juu ya kijiuchanja ambacho kilitokea ghafla pale katikati ya kilinge.
Iiiii mayhuuu? Ilikuwa sauti ya chini ya mtu aliekuwa pale jirani yangu juu ya mti akimaanisha ayaa mama yangu? Nilimsikia lakini sikumtazama.
Tusikilizane sasa, alisema yunge tena,
Ng'wana jong'hela unatowa sadaka hii kwa sababu gani?
Natoa sadaka hii kwa sababu zawadi mliyonipa ni kubwa kuliko sadaka hii! Alijibu mama yule kwa mbwembwe zote, ili kuonesha furaha yangu nakuomba mkuu unipatie kile kisu kikuu ili niwathibitishie niyasemayo, aliongeza mama yule mnene.
Shangwe zililipuka tena kisha zikakoma baada ya mkuu (yunge) kunyosha mkono juu.
Nilimwona yunge akipenyeza mkono kwenye chungu ambacho nilikiona punde tu alipopeleka mkono na kutwaa jisu kubwa na kuukuu, alimkabidhi yule mwanamke ambae alikipokea na kuwatazama wenzio kwa jicho la mnataka niwaoneshe?
Walimshangilia huku akimsogelea yule mtoto pale kwnye uchanja!
Mkubwa.Pettymagambo huyu Yunge kiongozi wa hili genge, Ni Yunge mdogo au Yunge shemeji?
inaonekana ni shemeji huyu.Pettymagambo huyu Yunge kiongozi wa hili genge, Ni Yunge mdogo au Yunge shemeji?
Asante.Mkubwa.
Nimecheka sana.tahadhari humu ukiona maneno huyajui usiyasome yaruke unaweza jikuta kumbe umekula kiapo ukajikuta gambosh.
Shusha vitu mkuuNimecheka sana.
Ngosha vitu si vya mchezo, lete vitu leo weekend...70
Alitamba mwanamke yule kisha akaikamata shingo ya mtoto yule alieonekana kusinzia usingizi wa kifo pale juu ya uchanja, aliwatazama wachawi wenzie ambao walipaza sauti senzaga, senzaga, senzaga (chinja, chinja, chinja,)
Kilisogezwa kibuyu kikubwa pale kwenye kichanja na yule mwanamke akang'ata meno kwa nguvu huku akikandamiza lile jisu butu shingoni mwa yule mtoto.
Yeee mayhu wansenza ung'wana wane gete? (ayaa mama unamchinja mwanangu kweli?).
Ilikuwa sauti kutoka jirani yangu mkono wangu wa kuume kwa yule jamaa niliyehisi nae kaletwa kuja kujionea mambo, kumbe yule mtoto aliwa kuchinjwani ni wake! Sauti ile ilinistua na kunifanya nisaha maagizo ya yunge ya kutomtazama yule mtu, niligeuka na kumtazama kitendo kilichopelekea astuke sana na kusahau kama yupo mtini, ilionekana hakuwa ameniona kabla, aliachia mti na kudondoka chini kulikopelekea lile kundi kustuka na kuahirisha walichokuwa wanakifanya na kuanza kusogea kule kishindo cha mtu kuanguka kiliposikika.
Fumba macho kisha ruka chini na utimue mbio
Ohooooo...71
Fumba mcho, ruka chini kisha timua mbio, usiutupe upembe wala miwani, fanya haraka vinginevyo utafanywa kama alivyotakiwa kufanywa yule mtoto, ilikua sauti ya yunge kupitia upembe uliokuwa mkononi mwangu, wakati huu watu wale wanaukarbia mti ule, nilifumba macho na kujitupa chini huku nikiamini nakwenda kuvunjika kama si miguu, basi kiuno hakitakuwa na kazi tena, ajabu nilishuka kiulaini tu kisha nikasikia tena upembe ukitoa maelekezo, kimbia kushoto kwako, na ukifanya utani tutakuchanganya chungu kimoja na yule mtoto, niliogapa sana kusikia vile, yaani nyama yangu nipikwe kama ambavyo alitakiwa kupikwa yule mtoto.
Nilitimua mbio hukt nikiwa sielewi naenda wapi!
Ebu geuka nyuma uone walivyokukaribia, sauti ile nikaisikia tena.
Niligeuka nyuma nione nini kinachojiri! Kudadeq, hapo sasa nianza kuzisikia sauti ambazo sikuwa nazisikia kabla sijageuka.
Kundi kubwa la watu wapanda mafisi, wengine mabundi na mapaka makubwa huku wamebeba mikuki na mapanga wakipiga kelele
Wakija kasi,
Nchimagi nchimagi...!