True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

...89
Sitomwonea huruma mpuuzi ambae anatambua kabisa hii ni mali ya mkuu wake, lakini kwa hila zake kamshawishi mpaka kalala nae, alikoroma yunge.
Kiufupi huyu kijana mbele yenu ndo alikuwa baba yenu mtarajiwa ambae ningemtambulisha kwenu alhamisi ijayo, lakini ameshanajisiwa na huyu mtoto wa yule bibi mlozi kutoka ukanda wa dakama (kusini), sasa nataka kwakumwonesha kwamba ukanda wangu unanguvu na si wakuchezewa hata kidogo, aliendelea kupaza sauti kwa hasira huku machozi yakimtoka na kunifanya huruma ianze kuniingia.
Nzehe kwanini umekubali kushawishiwa na huyu mtoto wa mlozi mpaka unikosee mchumba wangu? Aliniuliza yunge huku akitusogelea na panga refu lenye makali na damu damu iliyogandamana.
HAKUPENDI!
Alijibu yunge mdogo kwa hasira huku akimtazama yunge mkuu kwa jicho la shari?
Nimekuuliza wewe mbwa? Aling'aka yunge mkuu huku sasa akiliinua panga lake lenye kuogofya.
Tukimbie, alinong'ona yunge mdogo ambae aliinuka ghafla huku akiwa kanishika mkono wa kulia.
Kwa kasi tuliwavaa wachawi watatu.
 
...90
Tuliwavaa wachawi watatu walioonekana ni wazee waliokua upande wa mashariki, walianguka vibaya na kutufanya tupate upenyo wa kukimbia, sikuamini yunge mdogo alikuwa mwepesi mno, alikimbia kuniongoza njia huku nyuma yunge mkuu na washirika wake wakija kasi! Japo leo sikuwa nimewaona bibi na yule mzee wa kiwanjani pamoja na yule mama mnene ambao jana walikosa kunitia mikononi, yunge alikua na speed ya hatari huku akiwa amepanda lijifisi kubwa kuliko la yule mama kibonge.
Ajabu niliweza kuwaona wote japo niliwategea mgongo, walikua wanatimua mbio kali mno, wapo walipanda mafisi kama yunge, wangine mapaka makubwa meusi pii, wengine juu ya mabundi makubwa na wengine juu ya nyungo, walikuwa na siraha za jadi zenye kuogofya sana.
Kunja mguu mmoja tukimbie kwa kutumia mguu mmojamoja, alinielekeza yunge mdogo, nilifanya vile tukaanza kurukaruka kwa mguu mmojammoja, Ewaa! tulianza kuwaacha mbali yunge na wenzie.
Sekunde kama 10 tangu tuanze kurukaruka, tuliwaacha mbali mno.
Puuumbav sana leo mwisho wenu nyote.
 
...91
Ghafla tulisikia sauti ya kitu mfano wa chupa tupu ikirushwa inavyotoa sauti (vu vu vu vu) nilitazama juu na kuuona upembe ule alionipa jana yunge niushikilie, sasa ulitupita kwa juu na kwenda kudondokea mbele yetu ambapo punde tu mara baada ya kudondoka uliwaka moto mkubwa mno.
Dah! Ametuwahi mshenzi huyu, sina njia ya kujiokoa zaidi mpenzi, najua nitakufa mimi, ila ukweli nakupenda mno nzehe, na usikubali kulala na huyo mchawi hata siku moja ukiwa na akili yako timamu, aliniambia yunge mdogo kwa kukata tamaa.
Mshenzi kabla sijakufikia anza kusali sala za mwisho, na sijui sala zako utamsalia nani maana MUNGU wako hakupendi kwa ushenzi mnaofanyaga na bibi yako mlozi maarufu wa kanda ya kusini, aliongea kwa ukali yunge mkubwa akimtishia yunge mdogo huku sasa zikiwa zimebaki hatu kadhaa watufikie.
Niliyaangalia mafisi yalivyokua yanatokwa udenda mdomoni kwa uchu, nikayatizama mapaka yenye macho mabaya, nikamtazama pia yunge mkubwa alivyobadilika macho nakuwa kama ya mapaka.
Nishike kwa nguvu tunaondoka..!
 
...92
Nilimwambia yunge mdogo akaze mkono, huku mbele yetu moto mkubwa na waajbu unawaka, na nyuma yunge na kundi lake sasa walikuwa wanatembea kwani walijiamini wameshatutia mbaroni.
Ghafla nilivuta pumzi na kujikaza bila kupumua, nilishangaa naanza kuinuka juu na kuicha aridhi (kupaa) lakini nilirudi chini haraka kwani sikuweza kuhimili uzito wa yunge mdogo.
Unataka kufanya nini nzehe? Hapo ndo mwisho na hakuna atakae jinasua na kiama kilichopo mbele yenu, wewe pia umeniudhi na sasa nitaanza na wewe kukata kichwa chako ili huyo malaya wako ashuhudie ninavyokula nyama ya mpenzi wake, nadhani sasa nimekujibu vyema swali uloniuliza kama nakula nyama za watu ama la, alinitisha yungu huku sasa wakiwa wamebakiwa kama mita 40 watufikie, walikuwa wanatembea taratibu kwa kujiamini, wakiwa na imani kuku wako manati ya nini.
Nilikuamini sana, nikakupa usichana wangu, nikakuonesha na siri zangu za ndani kabisa, ajabu siku moja tu umenitenda makusud...
Kabla hajamaliza kauli yake nilimbana kiunoni yunge mdogo na kupaa.
 
...92
Tulianza kama masihara vile, taratibu tulianza kupanda juu kwa mwendo wa unyoya wakuku, (hapa waliokulia kijijini wataelewa unyoya unavyoeleaga angani taratiibu).
Tuliendelea kupanda juu huku wale washirika wa yunge wakicheka kwa dharau.
Yunge alikuwa kimya akishangaa kwamba yanawezekanaje mambo yale mtu kupaa bia mbawa wala ungo?
Hata mimi mwenyewe nilijishangaa uwezo ule wa kupaa huku nimemshika mtu kiunoni.
Alikuja kushtuka yunge mkubwa tumeshafika mita kama 90 au 100 angani na sasa speed ilikuwa inaongezeka.
Nilimwona yunge akiwa na hasira nyingi juu yetu, alipiga kelele,
Nyanineng'we (***** zenu) leo nawatafuna wote.
Nilitahamaki kuona mafisi yanakatisha anga yakija kwa kasi huku yunge sasa akiwa mpaka machozi yanamtoka.
Vu vu vu vu, ilikuwa sauti ya upembe wa yungu ukipita juu yetu.
Hamadi! Tulianza kushuka kwa kasi kuelekea chini ambapo yalionekana mawe makubwa yalichongoka kwa juu na kuwa na ncha kali mno, sasa tulikuwa tumegeuka na kutanguliza vichwa chini miguu juu, mamaaaa! Uwiii! Tunakufaaa!
 
Amkaaaa unaotaa mkuuu utajikojoleaa [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
...93
Alipiga kele yunge mdogo kwa hofu kuu.
Kasi ilikuwa kubwa kuelekea chini ambapo ilikuwa tunakwenda kupiga vichwa juu ya yale mawe mabaya na yatishayo kwa kuyatazama.
Yunge na watu wake walikuwa wanacheka vicheko vya ushindi na dharau kwetu.
Yunge mdogo aliendelea kupiga kelele kwa hofu huku akiniomba nimsaidie, ghafla aliniponyoka na kutanguli chini kwa kasi ambapo alipiga kichwa vibaya mno juu ya jiwe baya lililochongoka na kumfanya asambaritike vibaya mno huku damu zikitapakaa juu ya mawe yale yote.
Hapanaaa! Nililia kwa sauti huku nikiwa nakaribia kabisa kulifikia jiwe refu kuliko yote hukulikima limejitengenezea ncha kali mno, lilikuwa linaningoja mimi huku kelele za shangwe zikisikika, ni yunge mkuu na wafuasi wake walikuwa wakishangilia kwa nguvu mno, huku mapaka yakilia kama watoto wadogo na mafisi yakipiga yowe zilizokuwa kero mno maskioni mwangu, mabundi hayakuwa nyuma yalitoa sauti nzito kwa kushinda, kiukweli nilipitia mateso mabaya muda huu ambao nilikuwa nakwenda kusambaratishwa vibaya mno
 
...94
Zikiwa zimebaki kama sekunde 10 nilifikie lile jiwe bawa, nilihisi joto la hatari mno, sasa nilikuwa nahesabu kabla sijajibamiza juu ya jiwe lile.
moja, Mbili, tatu...!
Nilistuka kutoka usingizini huku mwili wangu ukiwa umelowa jasho vibaya mno.
Ndoto. Ndio, ilikuwa ndoto mbaya sana kuwahi kuiota, ajabu nilikuwa natokwa machozi machoni, niliogopa sana, nilikumbuka yunge mdogo alivyopasuliwa na jiwe lile baya na kusambaratishwa vipande vipande, nikakumbuka sauti zile mbaya za watu kutucheka, mabundi mapaka na mafisi mwili ulinisisimka vikali.
Maswali juu ya jibu la yungu kula nyama za watu yalikuwa mengi mno kichwani mwangu, sasa nilianza kumchukia yunge mkubwa na kumpenda mno yunge mdogo, nilitamani sana kuamka usiku ule nikamwone yunge mdogo.
Nilinyanyuka haraka na kuvaa sweta langu, nilitoka na kufunga mlango wangu, nilianza kuzipiga hatua kuelekea kwao yunge mdogo, lakini kabla sijavuka mpaka wa kiwanja cha pale nyumbani kwa babu nilikumbuka jambo moja lilonifanya nigeuze kurudi ndani kwaunyonge..!
 
Umeanza kuharibu ulipofika sehemu ya 36 na hasa 37. Mimi ni mwanaume kunidanganya acha!
Kikawaida kwa mwanaume kupita muda mrefu bila kufanya,siku akitunukiwa dakika 6 ni nyingi tukio zima linakuwa limekamilika,labda next round sasa ndipo hizo mbwembwe sijui kulamba mara blaablaa ndipo zitafuata.

Lkn pia ninahisi wewe ndiye uliyewahi kuandika thread yenye heading HOW I MET MY WIFE.
Sina uhakika sana ijapo kwa kipindi hicho sikuwa member bali nilikuwa mpenzi msomaji tu.
 
Pole ila huyo bundi wa babu yako ungemfyatua tu manati maana anakunyima uhuru wa kutoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…