True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Tatizo hawasemi ukweli kama ni hadithi za kutunga
Nyinyi ndio hamna akili,mods wameweka jabisa kwenye platform ya entertainment,ingekuwa ni story za jweki ingewekwa habari mchanganyiko,hizi ni tunzi kama za shigongo tu
 
119
Heheee! Dunia imevaa sketi sasa, naona siku hizi mambo waziwazi, ukiwa na aibu fumba macho tu, alisikika mama mmoja kati ya wengi waliokuwepo pale baada yamimi kumkumbatia yunge, minong'ono ilikuwa mingi sana iliyopelekea sasa nikumbwe na soni kiasi.

Mwenye wivu ajinyonge mamaa, alisikika mwanadada mwingine, niyule tatu mwenye maneno mengi ambaye jana tu alisutwa na wenzie kwa kuisema vibaya familia ya babu.

Baada ya kusalimiana na yunge, ilibidi nibebe dumu zangu na kuondoka haraka, kwani nisingeweza kumgoja mpaka zamu yake ya kuchota ifike kutokana na watu wengi waliokua mbele yake.

Nilizipiga hatua za haraka kwa lengo kwamba niwahi kufika na kurudia maji ili nimkute yunge pale bombani.

Nilifika nyumbani na kuingia jikoni, nilimimina maji mtungini kisha nikatoka na dumu zangu ili nifate maja tena.

Weka madumu yako twende huku kwanza, ilikuwa sauti ya babu.

Nilirudisha dumu ndani kisha tukaongozana babu tukiifuata njia ile ya kisimani, muda huo babu alikuwa anaimba nyimbo za kisukuma kwahisia sana.
 
120
Alikuwa anaimba nyimbo za malenga wa kisukuma waliokuwa wanashindana zamani enzi za mababu.

Tulifika pale bombani na babu aliwasalimia wote waliokuwa pale, nilitupa jicho kuona kama nitamwona yunge mkubwa, lakini sikufanikiwa kumwona na badala yake nilimwona yunge mdogo ambae tulipokutanisha macho tu, aliangalia pembeni kama mtu ambae hajafurahishwa na uwepo wangu.

Tuliendelea na safari kwa muda wa dakika 10 tukayafikia majaruba mengi yaliyonyooka huku nyasi laini zikiwa zinakaribia kumezwa na maji, kwa mbele kidogo kulikua na majembe matatu ya kukokotwa na ng'ombe (plau) yakiigeza ardhi na kufanya zile nyasi laini zimezwe na ardhi ile.

Haya yote ni majaruba yangu, na hawa wanatulimia sisi, alisema babu na kuongeza, hapa kila mwaka napata junia 30 mpaka 40, na shamba silimagi lote, ila kwa mwaka huu kwakuwa umekuja mdogo wangu nitaongeza majaruba manne kwaajili yako, hapa utakuwa na uhakika wa kupata junia 15 mpaka 17.

Kiukweli nilifurahi mno, kwani nilianza kupiga hesabu ya gunia 15 x 50000 =750k.
 
121
Niliwaza pia yunge alikuwa ameniahidi jaruba 3 za kupanda tu kwani zilikuwa zimeshalimwa tayari, hapa pia nilijipa maximum junia 5 hivyo nilijiona tayari nina milioni njenje, watanikoma huko nyumbani, nilivimba kichwa.

Tuliwasalimia wale vibarua ambapo nilivutiwa na wale waliokuwa wameshikilia plau wakilima, yaani niliona wanafaidi sana hivyo nikatamani kujaribu, jamaa mmoja akanipatia.

Nilikamata vizuri mikono ya plau like na kukanda miza chini kwa nguvu huku nikifurahishwa na ardhi inavyobanduka na kutupwa pembeni ikiwa imejigeuza, niliona ng'ombe wamepunguza speed na plau likawa linabinuka kwa mbele, usikandamize kwa nguvu, tutaumiza ng'ombe, alinambia jamaa aliyekuwa anaswaga kuwaongoza wale ng'ombe.

Tulifika mwisho wa jaruba na kugeuza mpaka tulipomwacha babu na yule mshika plau ambapo babu alinitaka nimkabidhi yule jamaa aendelee kulima ili sisi tufanye mambo mengine, nilimkabidhi tukaondoka pale.

Babu alinitaka niingie kwenye kijumba kidogo cha nyasi kilichokuwa juu ya kichuguu, niliingia mle.
 

natia nukta
 
122
Niliingia ndani ya kijumba kile ambacho kilijengwa kwa tofali za tope na kuezekwa kwa nyasi, hiki kilijengwa kwaajili ya kuamia ndege na kujikinga na mvua.

Nilichukua mkaa kiasi, mafuta ya taa na kiberiti kama alivyokuwa ameniagiza babu na kutokanavyo nje ambapo alinitaka nikoke moto juu ya kichuguu, nilifanya kama nilivyoagizwa.

Haya twende huku, alisema babu mara baada yakuwa nimewasha moto.

Nilimfata kwa nyuma mpaka tukafika kwenye lambo kubwa kiasi ambalo alisema ni lakwake, nilimwona babu akisogea ukingoni mwa lambo na kuchuchumaa, alipapasa majani kisha nikamwona amekamata kijiufito chembamba sana, alivuta taratibu na hatimae akatokeza samaki mkubwa (kamongo) aliyekuwa amenaswa na ndoano, babu alimnasua na kumhifadhi kwenye mfuko wa sandarusi kisha akahamia sehemu nyingine na nyingine kadhaa ambapo kote huko alikuwa anatoka na samaki wakubwa wakiwemo kambale (mumi).

Tuliwabeba mara baada ya babu kuwa ametegesha tena ndoano zake, tulirudi mpaka pale tulipowasha moto na babu kunitaka tuwatumbue.
 
Tuendelee Ngosha
 
123
Tuliwatumbua baada ya kuwa tumeongeza mkaa kwenye moto, kisha babu aliwapanga vizuri juu ya wavu kambale wakubwa watatu na kuwaweka juu ya moto.

Walibaki kambale 6 na kamongo 3 wakubwa ambao tuliwahifadhi kwaajili ya kuwapeleka nyumbani.

Twende huku, alisema babu na kuanza kuondoka, tulivuka mahindi marefu yaliyokomaa ambayo babu alisema ni yakwake pia, mbele kidogo tuliingia kwenye bustani kubwa la migomba ambamo tuliona mikungu kadhaa iliyokomaa, baada ya kuzunguka kwa dakika 1, tulikutana uso kwa macho bonge moja la mkungu wa ndizi mbivu, mate yalinitoka kwa uchu.

Tuliukata na kuubeba mkungu ule mkubwa na kuanza kurejea kwenye kichuguu ambapo nilikuwa na hofu huenda wale samaki watakuwa wameungua vibaya.

Tulifika pale tukatua mkungu taratibu na babu kuwahi pale penye samaki na kuwageuza.

Hatimae samaki waliiva vizuri, babu aliingia kwenye kile kijumba kutoka na chumvi na pilipili, tulianza kuwashambulia samaki wale kwa pupa mpaka tukatosheka, tuligeuza mashambulizi kwenye mkungu ule wa ndizi..!
 
Nyinyi ndio hamna akili,mods wameweka jabisa kwenye platform ya entertainment,ingekuwa ni story za jweki ingewekwa habari mchanganyiko,hizi ni tunzi kama za shigongo tu
Basi aondoe hiyo 'true story' kwenye kichwa cha habari
 
124
Baada ya kula babu alinitaka nihamishe ule moto niuingize ndani ya kile kijumba kidogo kwani sasa mvua ilikuwa karibu kuanza kunyesha na baridi kali ilipuliza, baada ya kuhamisha tuliingia ndani na kuuzunguka moto ule kwaajili kuota, ndipo babu akanza kusema.

Babu: mimi ni nani
kwakoko?
Mimi: babu yangu.
Babu: unauhakika mimi
ni babu yako?
Mimi: ndio na uhakika.
Babu: sawa kama mimi
ni babu yako natumaini hutonificha kitu chochote unachokijua juu ya mambo waliyokutuhumu wale wazee jana, na kama kweli wanakusingizia naimani leo utanambia ukweli kwani hakuna rafiki yako wa ukweli kunizidi mimi na hata hao wapenzi wenu sijui mademu zenu hawawezi kuwa na upendo kama wangu juu yako.
Naweza kufa leo, mashamba haya ni mali yako, pia kuna ng'ombe watatu kwao yunge ni mali yako, lakini pia tayari nishakuwekea kinga kuonesha namna gani nakujali mwanangu,
Basi nambie ukweli wote juu ya tuhuma zile, alimaliza babu.

Nilikumbwa na hisia flani za uchungu zilizopelekea nitokwe machozi..!
 
Mkuu zinakuwa fupi sana duh!!
 
125
Nawezaje kumficha babu mambo ya hatari kiasi kile? Nilitokwa machozi huku babu akijipa kazi ya kunituliza.

Babu hata usingesema yote hayo, nikata shauri ya kukueleza kila kitu tangu usiku nilipoingia kulala, nipo tayari kukwambia kila kitu pasipo kuficha hata 1.

Nilianza kumsimulia babu kila tukio tangu nilipokutana na yunge mdogo na mkubwa mpaka kuanzisha nao uhusiano na mpaka yunge kunipeleka kwenda kujionea kilinge cha wachawi mpaka niliponusurika kufyekwa shingo na mzee yule wa kiwanjani pamoja na yule mama mnene ambao walikuwa hoi vitandani kutokana na pigo moja hatari la upembe wa yunge.

Katika kumsimulia mkasa ule, nilijipa angalizo kutomtaja bibi hata mara moja, na hatimae nilimaliza kumsimulia babu stori ile na yeye kuanza kunitwanga maswali.

Ebu nambie bila kuficha, ni nani mwingine unaemjua ulimwona kilingeni?
Mimi: mwingine niliemwona pale ni kijana mmoja ambae alikuwepo uwanjani siku niliyoenda kufanya mazoezi pale uwanani.

Niambie ukweli mwanangu, je bibi yako hukumwona kule?
Daah!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…