Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Asante kipenzi ndio nasoma hapa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kipenzi ndio nasoma hapa
Msimualiaji haringi?masai dada hii pia
Nyinyi ndio hamna akili,mods wameweka jabisa kwenye platform ya entertainment,ingekuwa ni story za jweki ingewekwa habari mchanganyiko,hizi ni tunzi kama za shigongo tuTatizo hawasemi ukweli kama ni hadithi za kutunga
Hana shida msimuliaji huku arosto ndogo sanaMsimualiaji haringi?
Naogopa arosto
Niliagana na yunge huku akiniahidi atamwomba mama yake kuna majaruba matatu yamebaki, kuliko yabaki bila kulimwa bora wanipatie niyalime mimi, ikizingatiwa familia zile mbili walikua na ukaribu sana,
Nilirudi mpaka pale nyumbani kwa babu ambae niliambiwa aliondoka asubuhi kwenda mnadani kununua mbuzi,
Nilikaa pale nje nikiota moto mpaka bibi aliponiambia nichukue maji kwenye mtungi nikaoge,
Nilioga kisha nikaingia ndani ya ile slopu, kulikuwa na kitanda kizuri tu cha futi 4×6, nilitoa mafuta ndani ya begi langu na kujipaka, nikabadili nguo huku onyo la yunge likiwa kila mara linajirudia kichwani mwangu, nikikumbuka nimemwambia sikuja pale kwa ajili ya mademu, bali nimekuja kwa mambo muhimu tu,
Huku akinijibu tutaona,
Pia ile kauli ya binti tuliemwulizia kwa babu mara ya kwanza kabisa kule senta na kutustua kwa kusema mnaenda kwa wale wachawi? Dah! Niliogopa, saa2
Nkiwa naota moto pale nje mara ghafla nikasikia kelele kule senta, ambapo umbali wa kutoka pale kwa babu kufika senta ni kama daki 5 hivi..
Tuendelee Ngosha122
Niliingia ndani ya kijumba kile ambacho kilijengwa kwa tofali za tope na kuezekwa kwa nyasi, hiki kilijengwa kwaajili ya kuamia ndege na kujikinga na mvua.
Nilichukua mkaa kiasi, mafuta ya taa na kiberiti kama alivyokuwa ameniagiza babu na kutokanavyo nje ambapo alinitaka nikoke moto juu ya kichuguu, nilifanya kama nilivyoagizwa.
Haya twende huku, alisema babu mara baada yakuwa nimewasha moto.
Nilimfata kwa nyuma mpaka tukafika kwenye lambo kubwa kiasi ambalo alisema ni lakwake, nilimwona babu akisogea ukingoni mwa lambo na kuchuchumaa, alipapasa majani kisha nikamwona amekamata kijiufito chembamba sana, alivuta taratibu na hatimae akatokeza samaki mkubwa (kamongo) aliyekuwa amenaswa na ndoano, babu alimnasua na kumhifadhi kwenye mfuko wa sandarusi kisha akahamia sehemu nyingine na nyingine kadhaa ambapo kote huko alikuwa anatoka na samaki wakubwa wakiwemo kambale (mumi).
Tuliwabeba mara baada ya babu kuwa ametegesha tena ndoano zake, tulirudi mpaka pale tulipowasha moto na babu kunitaka tuwatumbue.
Kwa hiyo unakinzana na mwandishi???Nyinyi ndio hamna akili,mods wameweka jabisa kwenye platform ya entertainment,ingekuwa ni story za jweki ingewekwa habari mchanganyiko,hizi ni tunzi kama za shigongo tu
Basi aondoe hiyo 'true story' kwenye kichwa cha habariNyinyi ndio hamna akili,mods wameweka jabisa kwenye platform ya entertainment,ingekuwa ni story za jweki ingewekwa habari mchanganyiko,hizi ni tunzi kama za shigongo tu
Mkuu zinakuwa fupi sana duh!!124
Baada ya kula babu alinitaka nihamishe ule moto niuingize ndani ya kile kijumba kidogo kwani sasa mvua ilikuwa karibu kuanza kunyesha na baridi kali ilipuliza, baada ya kuhamisha tuliingia ndani na kuuzunguka moto ule kwaajili kuota, ndipo babu akanza kusema.
Babu: mimi ni nani
kwakoko?
Mimi: babu yangu.
Babu: unauhakika mimi
ni babu yako?
Mimi: ndio na uhakika.
Babu: sawa kama mimi
ni babu yako natumaini hutonificha kitu chochote unachokijua juu ya mambo waliyokutuhumu wale wazee jana, na kama kweli wanakusingizia naimani leo utanambia ukweli kwani hakuna rafiki yako wa ukweli kunizidi mimi na hata hao wapenzi wenu sijui mademu zenu hawawezi kuwa na upendo kama wangu juu yako.
Naweza kufa leo, mashamba haya ni mali yako, pia kuna ng'ombe watatu kwao yunge ni mali yako, lakini pia tayari nishakuwekea kinga kuonesha namna gani nakujali mwanangu,
Basi nambie ukweli wote juu ya tuhuma zile, alimaliza babu.
Nilikumbwa na hisia flani za uchungu zilizopelekea nitokwe machozi..!