135
Alinitaka nimhakikishie kwamba saa 7 tutakutana kisimani tuongee, nami nilimwondoa wasi kwani mida hiyo ya saa 7 mchana watu hupungua kabisa kule kisimani hivyo ingekua nafasi nzuri ya kuonge.
Alikubali na kutaka nimsindikize, nami sikuwa mvivu, nilimsindikiza huku akipitisha mkono wake wa kulia na kuushika wakwangu wa kushoto hivyo tukawa tumeshikana kirafiki, nililihisi joto la mkono wake lililopelekea manyanda wangu aanze kufurukuta.
Sasa ulijuaje kama nalala mle? Nilimwuliya
Nilifika mapema nikawa nangojea muingie tu ndani, hivyo nilikuona unaingia mle, na hata kama nisingekuona ningejua tu kwamba unalala mle kwani najua kwamba ile nyumba ya nyasi ni jiko na hiyo slopu ndo kuna kitanda kwani huwa tunakuja kulima hapa, na wakati wa kula mara nyingi huwa tunalia kwenye slopu hasa inaponyesha mva, alitoa maelezo marefu tatu.
Basi sawa, we uende sasa, kesho tutaonana, nilimuaga.
Usinidanganye bwana, naingojea kesho kwa hamu, Alisema tatu.
Sitokudanganya, usku mwema msalimie mamkwe.
Nimsalimie nani?