True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

142
Tuliondoka mara baada ya msosi wa mchana huku babu akimuaga bibi tunakwenda kukagua ndaono zake.

Hapa kijijini mdogo wangu usimwani mtu kabisa, inasemekana wasichana wengi wamerithishwa uchawi na eitha mama zao ama bibi zao, wasichana wengi unaowana hapa kijijini ni wachache sana ambao hawajihusishi na ulozi, hivyo kwakuwa umekuja kwangu mwanangu, huu mwezi mmoja utakaokaa hapa lazima nikukinge, alisema babu.

Hata huyo mwanamke wako yunge kusema anakupenda mno na atakulinda ni sawa kabisa, huenda ikawa hivyo kweli, lakini siku mkikorofishana tu, utaliwa nyama hata ukiwa umeenda zanzibar, alizidi kunitisha babu.

Tulifika kwenye vichaka vingi baada ya kuwa tumeuvuka mpaka wa shamba la babu, kimvu kiliendelea kunyesia taratibu kikitulowesha japo tulivaa majaketi.

Huko vichakani baada ya kutembea kwa dakika kadhaa tuliufikia mti flani wenye mwonekano kama mwembe kwa mbali, tulifika pale na babu akanitaka nisimame kwa kutulia.

Niliona babu anakata matawi ya mti ule na kuwasha moto, nilistaajabu sana!
 
mtu akikutia shit unajibu maelezo marefu kuliko ata story yako yenyewe
 
143
Inakuwaje kuni mbichi inawaka moto kama imemwagiwa mafuta ya taa? Niliwaza.

Shiiii! Ilikuwa ni ishara ya babu akinitaka nisiseme wala kuuliza chochote, nilitakiwa kutulia.

Muda kidogo alinitaka nikae ili niote moto ule, alinipa kigogo kidogo nami nikakaa, babu alinitaka nifumbe macho, nilifumba ndipo nikawa nasikia puh, puh, puh, nikajua moto unazimwa ule, na kweli muda kidogo joto nilokuwa nalisikia likapungua sana.

Nilimsikia babu akiongea maneno kadhaa kwa kiluga ndipo aliponitaka nifungue mdomo pekee {kuachama} nilitii agizo na babu alinitaka nigeuze shingo kumwelekea yeye kwani mbele yangu kulikua na moto.

Aliongea kwa kiluga kichaa akawa ananitemea mdomoni, alifanya vile kwa dakika nzima ndipo alinifunika na kitu chepesi ambacho nilihisi itakuwa nguo japo wakati wa kwenda hakuwa amebeba chochote kitu.

Moshi ulikuwa mzito mle ndani ya nguo nilofunikwa lakini babu alinitaka nijikaze kidogo tu mambo yangekuwa tayari.
****
Nilishtuka jasho jingi linanitoka mfululizo, niliangaza maeneo nilipokuwa.!
 
Hivi mbona wengine hatuwezi kutukana,nyie mnaotukukana mmekulia wapi, mmesoma shule zipi, marafiki zako ni watu aina gani?

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
144
Nilikuwa ndani ya kile kijumba kidogo kilichokuwa kimejengwa mbugani juu ya kichuguu, nikile ambacho siku moja nyuma tulikaa na babu nikimsimlia ulozi wa bibi na yunge.

Niliangaza macho nisione mtu, ila niliona chungu kichafu sana kwa nje kikiwa juu ya mafika na moto wa mkaa unawaka.

Nilihisi miwasho mwilini mwangu, nilipojikuna shingoni kwa nyuma nilihisi kama tope limekaukia, pia ngozi ilikuwa inajivuta kila nikijigeuza, ndipo baadae niligundua nimechanjwa chale mwili mzima na zilikuwa zimekauka sasa.

Baada alikuja babu na majani ya mti ambao sikuwa naujua, aliipua kile chungu kichafu na kunitaka nivue nguo zote,
Nilivua nguo na babu akawa analoweka yale majani ya mti aliyokuja nayo ndani ya kile chungu kilichoonekana kinadawa ndaniye.

Alianza kunitonesha zile chale kwa kunisugua nayale majani yaliyochovywa kwenye dawa, alitoa kikopo kidogo cheusi na kukifunua, alitoa ungaunga na akaanza kuniwekea kila palipo na chale, alihakikisha kila chale ameitia dawa kwani alikuwa makini mno asiache hat moja.!
 
145
Hutakiwi kulala na mwanamke kwa muda wa siku 3, hapa sasa ndo nitajua kama umekuwa ama hapana, kiufup hutakiwi kulala mtu yeyote zaidi yako pekeyako, aliongea kwa msisitizo babu.

Nilikubali sharti hilo liloambatana na jingine la kutokuoga siku zote hizo 3.

Tunaweza kwenda na hutakiwi kugeuka nyuma mpaka tunafika nyumbani sawa?
Sawa babu niliitikia na tukatoka mle ndani babu akitangulia, nilijipa kazi ya kufikiri jambo moja tu kwamba sitakiwi kugeuka nyuma, kweli nilifanikiwa kwani mpaka tunafika nyumbani sikupata shida yoyote kunifanza nigeuke.

Ilikuwa saa 1 kasoro dakika kadhaa tulipofika pale nyumbani, babu alinitaka niingie ndani na kazi ya kukoka moto nimwachie yeye.

Niliingia ndani na kufungulia redio, nikawa nawaza mambo mengi mno hasa kuhusu babu kuishi na bibi zaidi ya miaka 60 na asijue kama ni mchawi wakati yeye babu anasema hakuna mtu wa kumgusa?

Baadae babu aliingia ndini mle na haraka nilimwuliza inakuaje anasema hajui kama bibi ni mlozi wakati siku ile walinitesa jikoni kwakuhamahama?
 
Leta story
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…