True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Ila we mwamba noma sana

Hata mwezi huna tayali umeshakua KING wa wachachi wote hadi unaogopwa
 
Nakuibia hii story yako naipeleka bongo Muvi wanipe pesa ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
154
Nilifumbua macho nikashangaa sana, nilikuwa pale nyumbani chini ya mwembe huku babu na mzee mmoja ambae niliwahi kuja pale nyumbani siku moja akiongozana na wazee wengine wawili pamoja na babu.

Huyu hakuwa mwenye maneno mengi, bali alikuwa ananiuliza maswali kwa ustaarabu tofauti na yule ambae aliniita mchawi, nilimkumbuka vizuri na nilimsalimia nae akaitikia na kunipa pole japo sikuwa na kumbukumbu kwa muda huo ya nini kimenipa.

Unajisikiaje sasa? Aliniuliza yule mzee mwenye mapengo asiwe na jino hata moja.
Najisikia vizuri mno, nini kimetokea kwani? Nilimwuliza mzee kibogoyo.

Tulia utajua tu, alinituliza mzee kibogoyo.
Sasa naona yupo vizuri, natakiwa kuondoka kwani muda umeenda sana, dawa hii ataogea kwenye maji ya uvugu na aoge kwa kuteremsha maji chini (sikutakiwa kujipapasa mfano wa kujipaka mafuta, bali niwe najimwagia maji yenye dawa kisha nayateremsha chini)

Aliondoka mzee mapengo huku akisindikizwa na babu, muda kidogo babu alirejea na kunitaka ninyanyuke kwenye mkeka nilipokua nimekaa.
 
155
Nilinyanyuka pale nikaingia ndani mwangu bila kujua naenda kufanya nini, nilisimama kwa muda pale sebleni nikijaribu kuvuta kumbukumbu ya nini kilitokea mpaka nikajikuta pale.

Nilimkumbuka Tatu na vurugu nilizomfanyia, nilikumbuka yote mpaka nilivyomkazia macho kwa hasira mpaka akapiga kelele za maumivu ya kichwa, pia nilikumbuka nilivyoanza kutokwa damu kwenye vidonda ambavyo nilikuwa nimechanjwa chale na babu, haraka nilijiangalia mwilini ili nione vidonda, mhh!! Vidonda vilikuwa vimepona visionekane kabisa, nilistaajabu sana.

Babu aliingia ndani mle na kunita nijiandae kwenda kuoga dawa, alinitaka nivue nguo zote mle ndani kisha nitoke nje uchi wa mnyama, nilifanya kama alivyosema.

Tangulia twende, alisema babu.

Niliongoza njia kuelekea nje ambapo jua lilikuwa halijazama bado, muda huu wa saa 12 nilipofika mlangoni nilimwona yunge mdogo akiwa anaongea na bibi, nilisita kutoka nikataka kurudi chumbani.

Wevipi? Wiki 2 upo uchi wanakuona kila kiungo chako, eti leo unajificha! Alisema babu.
Unasemaje?
 
156
Nilimshangaa babu kuniambia eti wiki mbili nilikuwa uchi mbaya zaidi anataka nitoke nje ili bibi na yunge mdogo wamwone manyanda wangu na mayai yake akienda kulia na kushoto kama anakaanga karanga, kisha tena wayaone makalio yangu yanavyopishana moja likipanda juu, lingine linashuka chini, niliona upudhi huu, nilisimama pembeni ya mlango nisitoke.

Naona akili bado haijakuka sawa wewe, ebu tangulia ukaoge haraka kabla maji hayajapoa, alinikomalia babu.
Nilichungulia tena nje na kuwaona bibi na yunge mdogo wakiwa wanatazama huku tulipokuwa, niwazi waliisikia sauti ya babu akinilazimisha jambo, kabla sijafanya chochote nilimwona yunge mdogo akielekea tulipokuwa, yaani ndani mwangu, nikawa najiandaa kumbia chumbani.

Wamekuharibu sana mwanangu, aliongea babu akinitazama usoni huku akiwa kanishika mkono kwanguvu na kuanza kunivuta kuelekea nje, tulipishana yunge mdogo ambae aliambiwa angoje nioge kwanza kisha ataniona, hapo sasa badala ya kuvutwa na babu ilibidi nikimbie kukwepa yunge mdogo asiyafaidi matako!
 
Back
Top Bottom