True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Heading ya hii story haikunivutia kabisa,hvyo nilkuwa naipitiliza tu lakin kuna member niliona anaisifia kwenye ile story ya ujambaz wa chuga,tabora kigoma zambia ndo nikaamua niisake,nimeipenda sana

Weka weka na uongo ili iwe tamu zaidi
Aiseee ule uzi wa poker uko jukwaa gani mkuu nitag nahuo uzi nimeupoteza kabisa yaani.
 
179
Niliendelea kujipa matumaini huenda nikirudia maji nitamwona tatu hivyo nilifika nyumbani na kumimina maji mtungini, nilitoka nje ambapo nilimkuta bibi kajianika kwenye kijua kile cha asbuhi, sikutaka kuonesha utofauti bali nilimsalimia kwa uchangamfu naye akajibu salamu yangu kwa uchangamfu.

Niliondoka kuelekea bombani kuchota maji, lakini kabla sijafika mbali niligeuka nyuma na kumwangalia bibi, nilishangaa kumwona kaniangalia kwa jicho la kuogopesha, aliangalia pembeni mara tu nilipogeuka, alichelewa kwani nilikuwa nimemshitukiza.

Nilifika pale bombani huku kichwani nikiwa na mawazo juu ya vita aloniambia babu dhidi ya bibi na yunge, kwa muonekano ule wa bibi kunikata jicho kali nilikosa amani kabisa, yaani yeye ndie mpishi pale nyumbani, itawezekana kweli kukawa na usalama? Niliiona hatari mbele yangu.

Kumbe bado upo hapa nzehe? Mie nilifikri ulirudi mjini baada ya tukio la siku ile, nilishituliwa na sauti ya msichana aliyejulikana kwajina la mage, huyu alikuwa rafiki yake tatu.
Nipo tu mage.
 
KAZI IENDELEE MPAKA SAA SITA USIKUπŸ˜…πŸ˜…
 
180
Maana kwa hali tuliyokuacha nayo ile siku ya tukio hapa, nilijua lazima utarudi kwenu mara tu utakapo zinduka, aliendelea kuniongelesha mage ambae kiumri alikuwa mkubwa kuliko tatu.

Nilichota maji kisha nikavunga kama nimebanwa haja hivyo nilitokomea vichakani huku nikingoja zamu ya mage kuchota maji ili tuongozane naye kutoka pale bombani na hilo lilitimia baada ya dakika kama 15.

Mage tatu mbona simwoni siku hizi? Nilimwuliza mage ambae alikuwa mbele yangu, mbele yake kulikuwa na wasichana wengine wanne na wote walikuwa wamejitwisha ndoo za maji.

Baada ya kumwuliza swali lile nilimwona mage akipunguza mwendo na wale wenzie wakawa hatua kadhaa mbele yetu.
Tatu anaogopa kufata maji huku tangu siku ile ya tukio, yaani maji anafata kule kwenye kisima cha mshirimu ambacho kipo mbali sana, alisema mage.

Unajua mage huyu rafiki yako tatu hata sikuona sababu ya yeye kuanza kunifokea vile siku ile, nikweli tulikuwa na miadi ya kukutana naye siku moja kabla ya lile tukio la mimi na yeye kupigana.
 
181
Usiku wa siku ile nilibanwa na kichomi hivyo babu alijaribu kunifanyia dawa ili nipate nafuu, lakini kadri muda ulivyosonga hali ilizidi kuwa mbaya na kupelekea kupumua kwa tabu sana, kulipokucha asubuhi tuliondoka na babu kwenda kwa mzee mmoja ambae alinichanja chale mwili mzima, alinipaka dawa na kweli baada ya muda nilipata nafuu na tukarejea nyumbani muda ukiwa si rafiki tena,
Sasa nilishangaa siku ile nafika kisimani anaanza kunishambulia kwa maneno makali vile kweli? Nilimweleza mage aliyeonekana kuguswa sana na uwongo wangu ule.

Kiukweli hata mimi nilichukizwa na ulopokaji wake, yaani kumbe mlikuwa na miadi na yeye badala atulie umweleze tatizo nini akawa analopoka vile? Alishangaa mage huku akisema shoga yake huyu huwaga ni kilopolopo mno.

Sasa mage ninazawadi yako, naomba umwambie aje tuyaongee yaishe kwani mimi nampenda mno tatu na sitaki akae na wasiwasi vile, nilimwambia mage ambae alionekana kuvutiwa na maongezi yangu huku shoga zake wakiwa wametuacha umbali kiasi.

Zawadi gani hiyo?
 
Zawadi ya FC LIBOLO bangala LITOMBO😜😜
 
182
Aliuliza mage huku akigeuka na ndoo yake ya maji kichwani, nitakupa hela ya soda, nilimwambia mage.

Naenda kuja nae saa hiihii tu, wewe andaa tu zawadi hiyo, alisema huku akianza kuondoka kwa kasi, aliiacha njia iliyokuwa inaeleke kwetu na kukunja kushoto kisha akapotea kwenye upeo wa macho yangu.

Nilifurahi mno na nilijiona nakwenda kukutana na tatu sasa.
Nilipakata madumu yangu nikazipiga hatua mpaka nyumbani ambapo niliwakuta babu na bibi wamekaa wanapiga stori jikoni, sikutaka maongezi mengi, nilimimina maji kwenye mtungi wa pili kisha nikarudia tena maji.

Nilipofika kwenye makutano ya njia ambapo huwa wanakunja kona kina mage na tatu niligonja kwa muda wa dakika kadhaa, wanawake na mabinti kadhaa walinipita pale wengine wakitoka bombani na wengine wakienda bombani.

Macho nilikuwa muda wote nayatupa kule ambako mage aliekekea na muda kidogo niliwaona mage na tatu wameongozana huku wakiwa na ndoo kila mmoja, wasiwasi kidogo ulinizonga kumwona tena tatu.

Walinifkia huku tatu akionekana mwenye aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…