179
Niliendelea kujipa matumaini huenda nikirudia maji nitamwona tatu hivyo nilifika nyumbani na kumimina maji mtungini, nilitoka nje ambapo nilimkuta bibi kajianika kwenye kijua kile cha asbuhi, sikutaka kuonesha utofauti bali nilimsalimia kwa uchangamfu naye akajibu salamu yangu kwa uchangamfu.
Niliondoka kuelekea bombani kuchota maji, lakini kabla sijafika mbali niligeuka nyuma na kumwangalia bibi, nilishangaa kumwona kaniangalia kwa jicho la kuogopesha, aliangalia pembeni mara tu nilipogeuka, alichelewa kwani nilikuwa nimemshitukiza.
Nilifika pale bombani huku kichwani nikiwa na mawazo juu ya vita aloniambia babu dhidi ya bibi na yunge, kwa muonekano ule wa bibi kunikata jicho kali nilikosa amani kabisa, yaani yeye ndie mpishi pale nyumbani, itawezekana kweli kukawa na usalama? Niliiona hatari mbele yangu.
Kumbe bado upo hapa nzehe? Mie nilifikri ulirudi mjini baada ya tukio la siku ile, nilishituliwa na sauti ya msichana aliyejulikana kwajina la mage, huyu alikuwa rafiki yake tatu.
Nipo tu mage.