True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

152
Nikweli jana homa ilinibana na kichwa kikawa kinaniuma sana ndipo babu akanitengenezea dawa, ila kwa sasa najiona afadhali kidogo, nilimdanganya yunge mdogo.

Samahani nzehe, naweza kuja usiku wa leo tukaongea jambo muhimu sana? Aliniuliza kwa upole yunge mdogo ambapo nilimkatalia kistaarabu bila kumchukiza kwa kisingizio naumwa hivyo nahitaji kupumzika.

Aliondoka huku nikiwa nimemwahidi siku nikijisikia vizuri nitamwambia aje tuongee ishu yake hiyo ya muhimu huku nikiwaza atakua anataka sex tu.

Siku ilofuata mida ya saa 6 bibi aliniomba nimsaidie kufata maji japo dumu 1 kwani alikuwa kaishiwa maji ya kunywa na vibarua karibu wanakuja kupata msosi.

Nilifika kisimani na kuwakuta wasichana kadhaa na tatu akiwemo.

Kwahio ukanifanya mtoto mdogo kuniweka nakungoja hutokei mpaka nikachoka? Alinidaka tatu juujuu, alafu sijui unaringa nini tu, kwahiyo unajiona mzuri sana ama hizo chale alizokuchanja babu yako ndo zinakupa kiburi? Naunavyonuka jasho sijui umeambiwa usioge wiki nzima ili dawa ikukae sawasawa?
Tatu boya sana...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji28][emoji23]
 
Back
Top Bottom