True story: Jinsi nilivyopambana kutafuta mali za Mjerumani mkoani Morogoro, mauzauza na vimbwanga nilivyokutana navyo

Mzee kingalu si alishafariki? Ila huku kuna mambo mazito sana, nipo mitaa ya huko huko unapopazungumzia mkuu. Nna jambo langu. Na story za huku nazisikilizia kwa umakini, kuanzia kiloka, mkuyuni, tununguu na msitu wa kibungo..tuendelee mkuu. All in all huku kuna mali kibao, mbali na hizo ngumu kumeza ( mercury ) kuna mawe ya kutosha...
 
Wapeni watu dili hizi . maisha yanawavuruga huku kitaa! Wanahangaika kutafuta freemason /kupga watu risasi kumbe kuna njia ndogo tu ya kuwa na roho ngumu tu kuingia misitun!
 

brooo kimbiza. kweli haka ka paragraph unaita sehemu ya tatu??? sasa si zitafika elfu 1
 
Haya tuanze na shilingi ngapi kwa hayo ma Mercury [emoji23]
Nasubiri part nyingine
 
Ukiendelea nitag
 
Story za madini morogoro mjini zimejaa matapeli kibao Kuna vigenge mbalimbali huko kiroka matombo mkuyuni mpaka pale morogoro mjini maeneo ya mwembesongo na mafisa. Vijana wa mwanza wametapeliwa Sana morogoro mjini Kuna jamaa anaitwa mwita alitapeliwa mpaka tsh milioni 78 kuhusu hayo mambo ya mekyuri mtafuteni mtu anaitwa siasa ni maarufu Sana kwa watu wa mawe (germstones) morogoro mjini huyu ni jamaa poa Sana anawajua matapeli na wema na kijiwe Chao kikuu kipo kichangani darajani kwahiyo mi mtu akija na story za mawe namtazama tu najua huyu anaenda kupigwa.
 
Wapeni watu dili hizi . maisha yanawavuruga huku kitaa! Wanahangaika kutafuta freemason /kupga watu risasi kumbe kuna njia ndogo tu ya kuwa na roho ngumu tu kuingia misitun!
Babu hakuna njia ngumu na ya kidwanzi kama hizi, kupoteza mazima ni nje nje, yaan mpaka ujitoe sana, wengi wanakuwa na matatizo zaidi ya awali baada ya kujiingiza katika ishu izo, kwanza milolongo yenyewe inahudisha mauza uza kama yote, binafsi sifanyi ishu za madini ila niko nafanya biashara tu na nazungukia sana maeneo hayo. Mimi binafsi nimezishindwa ndugu, wanaoweza location ndio hizo wanaweza kwenda kufanya survey
 
SEHEMU YA 4
Baada ya kufahamu formula zao, nikapanga siku kuingia katika mapango yale. Ila kabla sijaingia nikaenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro maana nilisikia kama ukiwa wa kwanza kutoa taarifa ya kuwepo kwa madini eneo fulani basi ukigundua wewe unapewa fungu kubwa sana na serikali.

Ukweli nilifika kwa mkuu wa mkoa na nikaandikisha jina la kwenye kitabu cha watu waliofika kumuona. Nashukuru sna baada ya kumueleza nia yangu ya kutafuta mali hizo alinitia nguvu sana na kuniambia taarifa za kuwepo kwa madini katika mkoa wangu yapo sehemu nying sana hivyo kama utahitaji msaada wowote basi uje na nitakupatia. Miaka ile Moro walipata mkuu wa mkoa mwelevu sana.

Aliniamasisha sana basi safari yangu ilianza siku ya pili yake huku nikiwa na ndoo ya lita 20, nyundo imara ya kuvunjia jiwe lenye mercury pamoja na tochi. Maana nilivyoelezwa mercury inatokea kwenye jiwe

Nikaona haina haja ya nyimbo wala ngoma, ngoja niiingie mchana kweupe kwenye yale mapango. saa 2 asubuhi nikafika mlimani pale nikisikia sauti za ndege na wala hilo joka sikuliona. nikapanda mlima kidogo nikaona pango, nikafurahi sana nikaona leo nimeshapata mali.

kwa nje pango lilionekana dogo mwanamme nikaingia.... huku nikiwa makini sana kutafuata jiwe nilitegemea litakuwa kwa juu
nilivyosogea mbele kidogo huku mwanga ukianza kupotea nikakuta kuna mapango matatu, hapa nilijilaumu sana kwa nini sikuuliza vizuri, sasa hapa naingia pango lipi leneye mali?

mawazo yakanipa niingie hili la kati kati... mwanamme nikajitosa hapo huku nikiwa nimewasha tochi yangu.... ndani ya lile pango kulikuwa kimya sana na kadri nilivyotembea nilihisi hata mchanga unabadirika. lile pango lina kipengo kikubwa sana na kulikuwa na ubaridi ndani ya lile pango. nikaanza kumulika tochi kwenye ule mchanga ni kweli upo tofauti kwani weneyewe ni laini sana na kuna sehemu unang'aaa sana nikasogea zaidi na zaidi huku nikitafuta jiwe... nilitembea kama urefu wa kiwanja cha mpira ndani ya pango....mbele nikaona niaona vitu sikuelewa vinaruka ruka ni mithili ya kundi kubwa la ndege.

Nitaendelea
 
Jamii forum watu wake Ni wajinga sana katika forums zote duniani yan wanazidiwa maarifa na magroup ya Facebook.

Sasa mtu kasema analeta ushuhuda wake binafsi bado mtu unaanza kumpinga Mara hooo Mara heee jamani mumuache akifika mwisho tutaelewa mbivu na mbichi wakujifunza atajifunza, wakuburudika ataburudika, wakuumia ataumia.

The end will justify the means
 
Nawekabkitako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…