True story: Jinsi nilivyopambana kutafuta mali za Mjerumani mkoani Morogoro, mauzauza na vimbwanga nilivyokutana navyo

True story: Jinsi nilivyopambana kutafuta mali za Mjerumani mkoani Morogoro, mauzauza na vimbwanga nilivyokutana navyo

Mzee kingalu si alishafariki? Ila huku kuna mambo mazito sana, nipo mitaa ya huko huko unapopazungumzia mkuu. Nna jambo langu. Na story za huku nazisikilizia kwa umakini, kuanzia kiloka, mkuyuni, tununguu na msitu wa kibungo..tuendelee mkuu. All in all huku kuna mali kibao, mbali na hizo ngumu kumeza ( mercury ) kuna mawe ya kutosha...
 
Wapeni watu dili hizi . maisha yanawavuruga huku kitaa! Wanahangaika kutafuta freemason /kupga watu risasi kumbe kuna njia ndogo tu ya kuwa na roho ngumu tu kuingia misitun!
 
SEHEMU YA 3

Nimeombwa niendeleee japokuwa uko mbele kunatisha kidogo

Basi siku ya alhamisi nikafika kwa kuvizia vizia na kufika jioni watu wachache sana wakaanza kujikusanya. Sikutaka kuona na wafatilia bali siku ile nikaenda karibia na mlima ule na nikajificha mahala ili tu nijue formula za kupata mali.
Ilipofika saa 6 usiku kweli nikaanza kusikia sauti zikielekea mlimani na nyimbo pamoja na Ngoma. Nikathibitisha kuwa ni kweli. Formula yao ya kwanza nimeshaijua.basi sikutaka kuingilia mambo yao ni usiku mkubwa sana. Wakafanya ngoma zao kisha zikazima baada ya nusu saa wakaanza kurudi. Ilikuwa ni saa nane kasoro usiku.
Basi nikajibanza huko msituni mpaka jua likachomoza nikaenda zanu kijijini.
Saa 3 asubuhi nikaonana na mmoja wao ambaye alikuwa aliniambia mara ya kwanza nifanye subira.
Sasa akanifafanulia zaidi....
" tumeenda kuomba dawa, huku usiseme mercury utajua unafata mali, basi ukiwa na madhumuni hayo utapotea polini au kuonana na nyoka mkubwa sana wa kutisha. Huwa tunapika ngoma na kuimba kisha mzee kingalu ambaye ndiye mkuu wetu anasikiluza sauti ya bibi. Bibi huwa anasema mna shida gani? Mzee anajibu wajukuu zako wagonjwa sana tunaomba dawa, bibi anmruhusu aingie na chupa aweke na aje achukue wiki ijayo."
Anasema dawa hiyo inatoka kwa matone madogo sana na baada ya wiki tunapata kijiko kimoja tu ndio tunaruhusiwa kuchukua.

Nilifarijika sana nikapanga jinsi ya kuingia katika mapango hayo

Nitaendelea

brooo kimbiza. kweli haka ka paragraph unaita sehemu ya tatu??? sasa si zitafika elfu 1
 
Habarini za leo wanaJF

Niliombwa na baadhi yana JF kutoa ushuhuda wangu kidogo jinsi nilivyopambana kutafuta mali za mjerumani mkoani Morogoro. Hii ni baada ya kuona nikichangia baadhi ya thread kuhusiana na matukio hayo. Ni matukio ya kweli

Ndugu wana JF kwa wale wanaopenda kufuatilia habari hizi basi tutaelezana kwa ufupi tu ingawa nilipanga hapo baadaye kwenye uzee wangu basi niandae kitabu cha kueleza stori nzima ili uwe mchango wangu kwa vijana wanaotafuta maisha.

Stori ilianzia hapa:
Mimi ni Mluguru na kwetu hasa ni Mkuyuni sio mbali sana na Moro mjini. Ila shangazi alikuwa anakaa maeneo ya Mikese pia ni karibu na Morogoro Mjini. stori hii ni ndefu sana ila nitaeleza kwa mukhtasari sana kwa sehemu NNe. Leo nitaandika sehemu ya kwanza, kisha Jummanne nitaendelea na ikifika jumamaosi Ijayo nitakuwa nimetoa Mukhtasari tu.

kama unaenda Morogoro ukifika maeneo ya maseyu upande wa kulia unaanza kuona milima. inaonekana kam haipo mbali na barabara na pia inonekana kama milima ambayo haina miti wala msitu ndani yake. La hasha hali haipo hivyo. ile milima ipo mbali sana na hakuna bara bara ya kufika pale ni macho tu uanona ipo karibu. ukianza kutembea kwa njia za pale mpaka kufika kule sio chini ya dak 40 ndio utafika pale na pia kuna miti mikubwa mingi sana na msitu mkubwa sana. kuna wakati huwa kunatokea moto katika ile misitu na wakati huo kunakuwa sio msitu mkubwa kwani sehemu nyingi zinakuwa zinaonekana.

Mjomba wangu alikuwa anfanya kazi Forest na walikuwa wanakwenda kulinda watu wasichome mkaa. siku moja mjomba akaenda katika moja ya milima ile na walikuwa maofisa 3 wa forest. walipofika pale basi mjomba wangu akawatangulia mbele na kuwaacha kama mita 15 hivi, kisha wenzake wakasita kwenda mjomba wangu akasogea zaidi na kisha mjomba akasikia kelele za wenzake wakimwambia akimbie kwani kuna nyoka mkubwa sana juu ya miti ile. Mjomba wangu alishindwa kutembea maana alijisikia kuishiwa nguvu kabisa maeneo yale na kuanguka chini. wenzake wakaosogea mbali sna na mahali hapo huku wakiangalia nyokoa mkubwa sana aliyetanda miti 6 akiwa anaondoka pale taratibu, baada ya muda nyoka yule akatoweka bila ya kumdhulu mjomba wangu aliyekuwa ameanguka chini ya ile miti.

Wenzake wakamtoa mahali pale na kumsaidie na kisha akawa sawa na alismuliwa kuhusu lile tukio. mjomba akasema, "Nilivyofika mahali pale ghafla pakawa pana baridi kali sana na kuisi kuishiwa nguvu pamoja na pumzi, nilisikia mkipiga kelelele lakini sikuelewa chochote baada ya hapo sikujua kilichoendelea".

Ila nitaomba mlima huo nisiutaje ila ni mmoja unaonekana hata ukipita barabarani kwenda au kurudi Moro.

Lile tukio la mjoma wangu lilinifanya nijiulize maswali mengi sana, basi nikawa naenda kwa shangazi yangu mara kwa mara katika maeneo yale.

kumbe katika kile kijiji wanafahamu nini kimo katika milima ile, nilanza kusikia bahadi ya vijana wa pale kuhusu watu maalumu kwenda katika mmoja wa milima ile na kupata mali.

Nikaamua kwenda kukaa kwa shangazi yangu muda wa wiki 3 ili nifanye uchunguzi wa kina kuhusu kijiji kile na mali kwenye mmoja wa mlima ule.

nikapewa story hii kwa siri . " "watu wametajirika wamejenga majumba kwa ajili ya mali zilizomo katika milima ile, mle ndani kuna maji ya mercury"
Nilishtuka sana kusikia hivyo basi na mimi nikaanza harakati za kujitosa

Nitaendelea
Ukiendelea nitag
 
Story za madini morogoro mjini zimejaa matapeli kibao Kuna vigenge mbalimbali huko kiroka matombo mkuyuni mpaka pale morogoro mjini maeneo ya mwembesongo na mafisa. Vijana wa mwanza wametapeliwa Sana morogoro mjini Kuna jamaa anaitwa mwita alitapeliwa mpaka tsh milioni 78 kuhusu hayo mambo ya mekyuri mtafuteni mtu anaitwa siasa ni maarufu Sana kwa watu wa mawe (germstones) morogoro mjini huyu ni jamaa poa Sana anawajua matapeli na wema na kijiwe Chao kikuu kipo kichangani darajani kwahiyo mi mtu akija na story za mawe namtazama tu najua huyu anaenda kupigwa.
 
Wapeni watu dili hizi . maisha yanawavuruga huku kitaa! Wanahangaika kutafuta freemason /kupga watu risasi kumbe kuna njia ndogo tu ya kuwa na roho ngumu tu kuingia misitun!
Babu hakuna njia ngumu na ya kidwanzi kama hizi, kupoteza mazima ni nje nje, yaan mpaka ujitoe sana, wengi wanakuwa na matatizo zaidi ya awali baada ya kujiingiza katika ishu izo, kwanza milolongo yenyewe inahudisha mauza uza kama yote, binafsi sifanyi ishu za madini ila niko nafanya biashara tu na nazungukia sana maeneo hayo. Mimi binafsi nimezishindwa ndugu, wanaoweza location ndio hizo wanaweza kwenda kufanya survey
 
SEHEMU YA 4
Baada ya kufahamu formula zao, nikapanga siku kuingia katika mapango yale. Ila kabla sijaingia nikaenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro maana nilisikia kama ukiwa wa kwanza kutoa taarifa ya kuwepo kwa madini eneo fulani basi ukigundua wewe unapewa fungu kubwa sana na serikali.

Ukweli nilifika kwa mkuu wa mkoa na nikaandikisha jina la kwenye kitabu cha watu waliofika kumuona. Nashukuru sna baada ya kumueleza nia yangu ya kutafuta mali hizo alinitia nguvu sana na kuniambia taarifa za kuwepo kwa madini katika mkoa wangu yapo sehemu nying sana hivyo kama utahitaji msaada wowote basi uje na nitakupatia. Miaka ile Moro walipata mkuu wa mkoa mwelevu sana.

Aliniamasisha sana basi safari yangu ilianza siku ya pili yake huku nikiwa na ndoo ya lita 20, nyundo imara ya kuvunjia jiwe lenye mercury pamoja na tochi. Maana nilivyoelezwa mercury inatokea kwenye jiwe

Nikaona haina haja ya nyimbo wala ngoma, ngoja niiingie mchana kweupe kwenye yale mapango. saa 2 asubuhi nikafika mlimani pale nikisikia sauti za ndege na wala hilo joka sikuliona. nikapanda mlima kidogo nikaona pango, nikafurahi sana nikaona leo nimeshapata mali.

kwa nje pango lilionekana dogo mwanamme nikaingia.... huku nikiwa makini sana kutafuata jiwe nilitegemea litakuwa kwa juu
nilivyosogea mbele kidogo huku mwanga ukianza kupotea nikakuta kuna mapango matatu, hapa nilijilaumu sana kwa nini sikuuliza vizuri, sasa hapa naingia pango lipi leneye mali?

mawazo yakanipa niingie hili la kati kati... mwanamme nikajitosa hapo huku nikiwa nimewasha tochi yangu.... ndani ya lile pango kulikuwa kimya sana na kadri nilivyotembea nilihisi hata mchanga unabadirika. lile pango lina kipengo kikubwa sana na kulikuwa na ubaridi ndani ya lile pango. nikaanza kumulika tochi kwenye ule mchanga ni kweli upo tofauti kwani weneyewe ni laini sana na kuna sehemu unang'aaa sana nikasogea zaidi na zaidi huku nikitafuta jiwe... nilitembea kama urefu wa kiwanja cha mpira ndani ya pango....mbele nikaona niaona vitu sikuelewa vinaruka ruka ni mithili ya kundi kubwa la ndege.

Nitaendelea
 
Jamii forum watu wake Ni wajinga sana katika forums zote duniani yan wanazidiwa maarifa na magroup ya Facebook.

Sasa mtu kasema analeta ushuhuda wake binafsi bado mtu unaanza kumpinga Mara hooo Mara heee jamani mumuache akifika mwisho tutaelewa mbivu na mbichi wakujifunza atajifunza, wakuburudika ataburudika, wakuumia ataumia.

The end will justify the means
 
SEHEMU YA 4
Baada ya kufahamu formula zao, nikapanga siku kuingia katika mapango yale. Ila kabla sijaingia nikaenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro maana nilisikia kama ukiwa wa kwanza kutoa taarifa ya kuwepo kwa madini eneo fulani basi ukigundua wewe unapewa fungu kubwa sana na serikali.

Ukweli nilifika kwa mkuu wa mkoa na nikaandikisha jina la kwenye kitabu cha watu waliofika kumuona. Nashukuru sna baada ya kumueleza nia yangu ya kutafuta mali hizo alinitia nguvu sana na kuniambia taarifa za kuwepo kwa madini katika mkoa wangu yapo sehemu nying sana hivyo kama utahitaji msaada wowote basi uje na nitakupatia. Miaka ile Moro walipata mkuu wa mkoa mwelevu sana.

Aliniamasisha sana basi safari yangu ilianza siku ya pili yake huku nikiwa na ndoo ya lita 20, nyundo imara ya kuvunjia jiwe lenye mercury pamoja na tochi. Maana nilivyoelezwa mercury inatokea kwenye jiwe

Nikaona haina haja ya nyimbo wala ngoma, ngoja niiingie mchana kweupe kwenye yale mapango. saa 2 asubuhi nikafika mlimani pale nikisikia sauti za ndege na wala hilo joka sikuliona. nikapanda mlima kidogo nikaona pango, nikafurahi sana nikaona leo nimeshapata mali.

kwa nje pango lilionekana dogo mwanamme nikaingia.... huku nikiwa makini sana kutafuata jiwe nilitegemea litakuwa kwa juu
nilivyosogea mbele kidogo huku mwanga ukianza kupotea nikakuta kuna mapango matatu, hapa nilijilaumu sana kwa nini sikuuliza vizuri, sasa hapa naingia pango lipi leneye mali?

mawazo yakanipa niingie hili la kati kati... mwanamme nikajitosa hapo huku nikiwa nimewasha tochi yangu.... ndani ya lile pango kulikuwa kimya sana na kadri nilivyotembea nilihisi hata mchanga unabadirika. lile pango lina kipengo kikubwa sana na kulikuwa na ubaridi ndani ya lile pango. nikaanza kumulika tochi kwenye ule mchanga ni kweli upo tofauti kwani weneyewe ni laini sana na kuna sehemu unang'aaa sana nikasogea zaidi na zaidi huku nikitafuta jiwe... nilitembea kama urefu wa kiwanja cha mpira ndani ya pango....mbele nikaona niaona vitu sikuelewa vinaruka ruka ni mithili ya kundi kubwa la ndege.

Nitaendelea
Nawekabkitako
 
Back
Top Bottom