True story: Jinsi nilivyopambana kutafuta mali za Mjerumani mkoani Morogoro, mauzauza na vimbwanga nilivyokutana navyo

Huyu jamaa na story zake kule makete sijui njombe kulee

Akaingia misituni huko, mara wakapotea akakutana na minyoka.. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sasa analeta hadithi zile zile za kutafuta mali za wazungu.

Aisee.
 
Hii chai kabisa na ishapoa mapema kabisa
 
SEHEMU YA 5

Naomba niendelee kidogo leo kwa wale wanaofuatilia. Maisha usikate tamaa. Jaribu kila linalowezekana ingawa tu kiwe ni cha halali na usizulumu mtu. Mungu si athumani. Mgaa na upwa hali wali mkavu..

Basi mbele niakona kama kiza hivi na ilikuwa ni ishara ya kundi kubwa sana la ndege mbele yangu ndani ya pango. sikukata tamaa na wala sikuogopa kwani niliamnini nipo peke yangu mle ndani na nilijua wadudu watakuwepo, pamoja na huyo mlinzi niliyoambiwa. nikasogea kwenye lile kundi niliamni labda ndipo ilipo. kumbe pale mahala kwa chini kama bonde lenye mchanga mzuri sana yaani kama mtu unashuka bonde ndani ya pango na upandishe uwafikie popo ni kama mlima fulani hivi. basi kuangalia vizuri lile kundi ni kweli walikuwa ni popo wengi wamejaaa mahali pale kuangalia vizuri lile bonde ni kubwa na limeenda mbali kiasi kisha likapanda ni mlima mdogo hivi. mara mchanga ukaanza kama kuelekea bondeni na huku popo wakiruka ruka pale mahala walipo. wazo likanijia nitafikaje kwenye lile kundi la popo na hapa chini kama nikitembea uwenda nikaseleleka na mchanga mpaka bondeni lakini nitaweza kupanda na kufikia mahala pale. pale nilipo na popo walipo ni kama mita 20 hivi lakini kuna kama kaponde yaani mlima ushuke halafu upande ila ni michanga mitupu hakuna hata mawe ya kukanyaga.

niaona ngoja nirushe mchanga au nipige ukelele niwashtue wale popo wakimbie nione kama hilo jiwe la mercury lipo hapo. haraka likanijia wazo...nina plastic ya lita 20 basi labda nikiipiga kwa nguvu popo watatoweka pale halafu huyu bibi pia anapenda ngoma.....

Nilivyoanza kupiga ndoo yangu nikaanza kuhisi usingizi na nilijawa na hamasa ya kuendelea kupiga hiyo ndoo kwa lengo la kuwatimua wale popo...kadri nilivyofanya ndio usingizi ulizidi kunishika

Nitaendelea sehemu ya 6 na ndipo vimbwanga vilipoanza kama ni muoga quit....
 
Mkuu mmh! Natamani kusema kitu ila Behaviourist atapata sababu ya kunisema πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ acha ninyamaze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…