SEHEMU YA 7
Baada ya kuhisi usingizi ukinijia kwa kasi, zoezi la kupiga ngoma nikalisitisha,nikapata wazo niitumie ndoo ile ile kuirusha upande ule wenye popo.nikaishika vyema na kuanza kuhesabu kwa utulivu 1,2,3 nikairusha,sijui ni wenge au mazingaombwe badala ya kurusha ndoo nikajikuta nimerusha tochi,nikapoteza kabisa uwezo wa kuona maana baada ya tochi kugonga ng'ambo iliserereka kuufata mchanga bondeni sana.
Hapa ndipo nilianza kuona vitu ambavyo sikuviwaza kabla.baada ya macho kuzoea giza,nikaanza kupata taswira taratiibu upya ya eneo lile,ule mwinuko ilikuwa ni sehem ya mgongo wa nyoka mkubwa sana,ambaye mpaka muda huo kichwa kilikuwa hakionekani,kumbuka kwa tochi sikutambua.
Nikaanza kupata wazo la kuondoka,bahati haikuwa kwangu kwani nyuma sikuweza kuona hata uelekeo wa mlango uko wapi ni giza jeusi.
Nikaanza kusikia kama kuna sauti ya mnong'ono ikizungumza kiruga,"wewe ni nani umefata nini humu???kwa uoga nisiweze hata kujibu swali hili hali ya kushikwa na usingizi ikaanza kuja tena,hapa nilishindwa nifanyaje maana sikujua natakiwa nichukue hatua gani,nikaanza kuhisi naota,nyoka yule anajikunjua kisha ananibeba na mdomo wake na kunitoa nje,baada ya hapo nikalala jumla,nakuja kushtuka saa kumi na mbili jion jua limeanza kugusa kingo niko nje ya pango.
Nikiwa na nyanyuka na kujizoa zoa kujiweka sawa,nikahisi ubaridi mkali sana,halafu kama kuna kitu kinajiburuza,kumbe ni yule joka.
Kwa ujasiri nikainuka na kuanza kumfata,nilipomkaribia nikashangaa anazungumza,kwa sauti ya kizee(kibibi).
Wewe kijana unatafuta nini hapa??
Nikajibu "bibi mjukuu wako ninaumwa sana ninahitaji dawa"akaniuliza ile ndoo na kimuli ni vyako??,nikamjibu ndio bibi.haaya ingia ndani.
Niaingia ndani nashangaa kukutana na ndoo na ile tochi mlangoni tu baada ya mlango,ndoo imejaa Mercury,nikaifata ile ndoo,sikujua mercury ni nzito kupita kiasi,sikuweza hata kuitikisa ndoo ile.wazo la kufata chupa ndogo likanijia,nikiwa natoka nikahisi kuna kundi la watu nje wakiimba na ngoma......
Itaendelea.