True story: Jinsi nilivyopambana kutafuta mali za Mjerumani mkoani Morogoro, mauzauza na vimbwanga nilivyokutana navyo

True story: Jinsi nilivyopambana kutafuta mali za Mjerumani mkoani Morogoro, mauzauza na vimbwanga nilivyokutana navyo

Jamani acha uchonganishi. Kwanza mleta mada hajakimbia, pili mimi sijatia neno lolote. In fact hii stori haina mashaka. Au unasemaje Behaviourist 😁😁😁
Hii kamati yako inabidi ijiridhishe kwanza😁😁😁
AEHNYZ.jpg
 
Story za madini morogoro mjini zimejaa matapeli kibao Kuna vigenge mbalimbali huko kiroka matombo mkuyuni mpaka pale morogoro mjini maeneo ya mwembesongo na mafisa. Vijana wa mwanza wametapeliwa Sana morogoro mjini Kuna jamaa anaitwa mwita alitapeliwa mpaka tsh milioni 78 kuhusu hayo mambo ya mekyuri mtafuteni mtu anaitwa siasa ni maarufu Sana kwa watu wa mawe (germstones) morogoro mjini huyu ni jamaa poa Sana anawajua matapeli na wema na kijiwe Chao kikuu kipo kichangani darajani kwahiyo mi mtu akija na story za mawe namtazama tu najua huyu anaenda kupigwa.
Mkuu mbona inaonekana kama wewe ndo Siasa unajipigia. chapuo?
 
Tuachane na stori kwanza, hivi madini ya mercury yana thamani kama ilivyo kwa vito au dhahabu?
 
hapana mkuu, mimi nina account 1 tu humu. na ananifahamu mtu mmoja tu humu. siwezi fanya kama wanavyofanya wengine si vizuri kutaja ila wanaaccount 7.

naeleza kisa cha kweli hakuna hata chembe ya uongo
Tuendelee basi mkuu, unapaka sana rangi. Wenzako huwa wanaweka kwa parts kwa vile wanakuwa busy sana, sasa wewe unacomment lakini humalizii hii story. Sio vizuri, sijapenda kwa kweli.
 
Tuachane na stori kwanza, hivi madini ya mercury yana thamani kama ilivyo kwa vito au dhahabu?
Kwa wachimba dhahabu kuna vitu vnachawanywa na hyo mercury akienda machimbo yenyewe hutumika kupata dhahabu kiurahc!!! Hiyo n kwaufupi sana ila unaweza kuifanyia vtu vingi ikakupa utajiri
 
Story za madini morogoro mjini zimejaa matapeli kibao Kuna vigenge mbalimbali huko kiroka matombo mkuyuni mpaka pale morogoro mjini maeneo ya mwembesongo na mafisa. Vijana wa mwanza wametapeliwa Sana morogoro mjini Kuna jamaa anaitwa mwita alitapeliwa mpaka tsh milioni 78 kuhusu hayo mambo ya mekyuri mtafuteni mtu anaitwa siasa ni maarufu Sana kwa watu wa mawe (germstones) morogoro mjini huyu ni jamaa poa Sana anawajua matapeli na wema na kijiwe Chao kikuu kipo kichangani darajani kwahiyo mi mtu akija na story za mawe namtazama tu najua huyu anaenda kupigwa.
Haya mambo yanawatia watu wazimu sana.
Sasa milioni 78 si ni mtaji mkubwa sana huo wa biashara.
 
SEHEMU YA 4
Baada ya kufahamu formula zao, nikapanga siku kuingia katika mapango yale. Ila kabla sijaingia nikaenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro maana nilisikia kama ukiwa wa kwanza kutoa taarifa ya kuwepo kwa madini eneo fulani basi ukigundua wewe unapewa fungu kubwa sana na serikali.

Ukweli nilifika kwa mkuu wa mkoa na nikaandikisha jina la kwenye kitabu cha watu waliofika kumuona. Nashukuru sna baada ya kumueleza nia yangu ya kutafuta mali hizo alinitia nguvu sana na kuniambia taarifa za kuwepo kwa madini katika mkoa wangu yapo sehemu nying sana hivyo kama utahitaji msaada wowote basi uje na nitakupatia. Miaka ile Moro walipata mkuu wa mkoa mwelevu sana.

Aliniamasisha sana basi safari yangu ilianza siku ya pili yake huku nikiwa na ndoo ya lita 20, nyundo imara ya kuvunjia jiwe lenye mercury pamoja na tochi. Maana nilivyoelezwa mercury inatokea kwenye jiwe

Nikaona haina haja ya nyimbo wala ngoma, ngoja niiingie mchana kweupe kwenye yale mapango. saa 2 asubuhi nikafika mlimani pale nikisikia sauti za ndege na wala hilo joka sikuliona. nikapanda mlima kidogo nikaona pango, nikafurahi sana nikaona leo nimeshapata mali.

kwa nje pango lilionekana dogo mwanamme nikaingia.... huku nikiwa makini sana kutafuata jiwe nilitegemea litakuwa kwa juu
nilivyosogea mbele kidogo huku mwanga ukianza kupotea nikakuta kuna mapango matatu, hapa nilijilaumu sana kwa nini sikuuliza vizuri, sasa hapa naingia pango lipi leneye mali?

mawazo yakanipa niingie hili la kati kati... mwanamme nikajitosa hapo huku nikiwa nimewasha tochi yangu.... ndani ya lile pango kulikuwa kimya sana na kadri nilivyotembea nilihisi hata mchanga unabadirika. lile pango lina kipengo kikubwa sana na kulikuwa na ubaridi ndani ya lile pango. nikaanza kumulika tochi kwenye ule mchanga ni kweli upo tofauti kwani weneyewe ni laini sana na kuna sehemu unang'aaa sana nikasogea zaidi na zaidi huku nikitafuta jiwe... nilitembea kama urefu wa kiwanja cha mpira ndani ya pango....mbele nikaona niaona vitu sikuelewa vinaruka ruka ni mithili ya kundi kubwa la ndege.

Nitaendelea
Hii stori kama ni ya kweli wewe jamaa una roho ngumu sana.
Sehemu kama hiyo ambayo umeambiwa kuna joka kubwa unaingia ukiwa peke yako,nimekuvulia kofia.
 
Back
Top Bottom