Hidden Diamond
JF-Expert Member
- Jan 31, 2024
- 260
- 481
Jina langu naitwa Hidden Diamond.
Kwa mama, mimi ni mtoto wa tatu kuzaliwa (na kaka yangu mkubwa ambaye mama alimpata akiwa bado msichana mdogo), ila kwa baba ni mtoto wa pili baada ya kaka yangu ambaye kwa sasa ameajiriwa kwenye sekta mojawapo binafsi nchini.
Kwenye familia yetu, wote kwa jumla tuko watano na hakuna mwanamke hata mmoja.
Mama yangu alikuwa ni mwanamke jasiri ambaye hata ningezaliwa kwenye sayari ya Pluto, ningeomba kuzaliwa naye yeye tena na wala si mama mwingine hata kwa dawa.
Kuna ule msemo wa watu wa maskini wa kusema, “Bora kuzaliwa mbwa Ulaya kuliko binadamu Afrika.” Hii ina maana mtu kama huyu anaona ni bora angekuwa mtoto wa mbwa Ulaya kuliko kuzaliwa na mama wa Kiafrika. Daaah aaah aaah! (Watu kama hawa ndiyo huwa wanajipa moyo kwa tukauli twao vya mchongo, mara one day yes, huku wamelala kitandani au wanashinda vijiweni kupiga umbea).
Tuendelee na story.
Mama yangu alikuwa ni kati ya walimu bora sana kwa familia yetu kwani kupitia upambanaji wake aliweza kuitoa familia yetu kutoka kwenye kula msosi wa unga limited mpaka kupata msosi wa uhakika na kuridhisha.
Nakumbuka kipindi maisha yalikuwa magumu sana. Mzee alikuwa amesafiri maana alikuwa mfanyabiashara wa vitenge. Kuna siku ndani msosi umeisha na hatujala tangu asubuhi.
Mama akatuambia:
“Nendeni mkacheze na wenzenu.”
Aliona tukiendelea kuangaliana itakuwa shida.
Sasa ile tunacheza na wenzetu mpaka saa kumi na moja jioni, yaani bado nje kuna mwanga wa jua, alituita mimi, kaka yangu pamoja na mdogo wangu. Kipindi hicho tulikuwa tunaishi kwenye nyumba ya kupanga.
Alivyotuita akatuambia:
“Ingieni ndani mkalale.”
Daaah! Tukawa tunajiuliza, mbona hatujala halafu mama anatuambia tulale tena?
Kimoyo moyo tukatambua kwamba leo mazingira magumu; siku nzima inaisha bila kuweka chochote tumboni.
Basi ilibidi tufanye kama bi mkubwa alivyotuambia.
Imagine guys, saa kumi na moja tunaingia kulala huku matumbo yanatetemeka.
Yaani tulivyoingia kulala, sijui usingizi ulitokea wapi mpaka nakuta bi mkubwa anatuamsha:
“Jiandaeni muende shuleni.”
Nisifiche, hii ni kati ya kumbukumbu mbaya sana kwenye maisha yangu.
Basi bhana, maisha yaliendelea hivyo hivyo. Bi mkubwa aliendelea kutupambania na kuhakikisha watoto zake wote tunakuwa kwenye misingi imara, heshima, upendo pamoja na adabu iliyotukuka.
Nakumbuka kuna baadhi ya mambo yalikuwa yananishangaza sana kwake kuhusu huyu kaka yangu wa kwanza.
Kwa mfano, alikuwa akileta ripoti yake ya mtihani kutoka shuleni, bi mkubwa alikuwa anamfinya mashavu kama kawaida akiwa wa tatu au wa pili. Alichokuwa anataka ni awe wa kwanza tu.
Halafu mimi na ndugu yangu, hata tuwe wa arobaini, hatuchapwi wala hatuguswi.
Nilikuwa nashangaa sana, ila baadaye nilikuja kuelewa kwa nini alikuwa anafanya hivyo.
Bi mkubwa wangu, kama walivyo kina mama wengine, alianza kujishughulisha na biashara mbalimbali ndogo ndogo kwa ajili ya kulinda familia yake; mara kuuza mchele, mara mahindi.
Nakumbuka wakati anauza mahindi, kuna kakisa ka kuchekesha kalitokea kati yake na huyu kaka yangu ninayefuatana naye.
Tulikuwa na utaratibu wa kumpelekea bi mkubwa chai pindi anapokuwa sokoni.
Sasa kuna siku kaka yangu huyu, kama kawaida yake, kamuandalia chai na viazi mviringo akawa anampelekea sokoni.
Sasa alipofika mitaa fulani karibu na sokoni, akakutana na mdingi fulani akaanza kumsalimia.
Mdingi: Uncle, vipi uko poa?
Brother: Niko poa, shikamoo.
Mdingi: Mama yupo?
Brother: Ndiyo yupo, ndiyo naenda sokoni kumpelekea chai.
Mdingi: Daaah! Dada yangu yule sijaonana naye muda sana.
Mdingi: Kwa hiyo umembebea chai na nini?
Brother: Chai na viazi mviringo.
Mdingi: Sawa uncle wangu kipenzi, basi wewe nipe chupa ya chai na hivyo viazi, halafu wewe tangulia. Mimi nakuja navyo nyuma, sawa uncle?
Brother: Sawa.
Akaanza kuondoka.
Ile kufika sokoni tu...
Bi mkubwa: Wewe, chai iko wapi? Mbona unakuja mikono mitupu?
Brother: Anakuja nayo uncle nyuma.
Bi mkubwa: Uncle gani?
Brother: Kuna mbaba alisema yeye ni uncle wangu, kwa hiyo alisema nimkabidhi chupa ya chai na hotpot la viazi, atakuja navyo, mimi nitangulie.
Bi mkubwa: Mama yangu! Hii mbwa ishatapeliwa!
Hapo anaongea tu, brother kashapigwa ndala ya kichwa.
Watu sokoni ni vicheko hatari, brother yeye kabaki kaduwaa tu.
Jamani, tutaendelea na next episode wakati mwingine.
NEXT EPISODE LOADING*************