Trump aanzisha Trump TV baada ya Vyombo vya habari kumsusia

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Ikulu ya Marekani imezindua kituo cha matangazo ya kidijitali cha saa 24 kinachoitwa “Trump TV: The Essentials Station" huku mvutano kati ya utawala wa Rais Donald Trump na baadhi ya mashirika makubwa ya habari nchini humo ukizidi.

Kwa mujibu wa Ikulu, jukwaa hilo litaangazia video muhimu, hotuba kubwa na matukio muhimu kutoka katika utawala wa Trump, likirusha maudhui muda wote na kusasishwa moja kwa moja.

Uzinduzi huo umefanyika wakati kukiwa na mvutano kati ya utawala wa Trump na baadhi ya vyombo vikubwa vya habari ambapo Trump alizuia CNN, Politico na MS NOW kuingia katika maeneo ya Ikulu, hatua iliyosababisha vyombo hivyo vitatu kuishtaki serikali.

Baadaye, mitandao mikubwa ya televisheni ya ABC, CBS, Fox na NBC zilisimamisha kwa pamoja kuripoti shughuli za Ikulu kwa kuunga mkono vyombo vilivyoathiriwa.

Ikulu imetetea msimamo wake kuhusu upatikanaji wa vyombo vya habari, huku Trump akiendelea kukosoa kile anachokiita habari zisizo za haki au “fake news” kuhusu utawala wake.

1790079601274.png
 
Ajiandae na kipigo cha midterms
 
Akipigwa bun popote kesho yake anakuja na plan B

Si tunakumbuka mgogoro na Twitter ya sasa X❗️
 
Ila Trump huyu mwamba kichwa yake anaijua mwenyewe. Kuna siku eti anasema anataka kuinunua afrika.
 
Hawa watu walioshindwa kujitawala afadhali wanunuliwe tu, eti bara lina kila kitu lakini ndilo linaoongoza kwa kuwa na watu fukara zaidi duniani. Bure kabisa.
 
1790103960528.png

base za marekani kuziepuk uwe na msuli kwelikweli
 
Back
Top Bottom