Trump adai Mauaji Iran Yamesitishwa, lakini kama hali bado ni tete nchi humo

Trump adai Mauaji Iran Yamesitishwa, lakini kama hali bado ni tete nchi humo

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Rais wa Marekani Donald Trump ameongelea hali ya usalama nchini Iran. Katika kauli yake ya hivi punde, Trump amewahakikishia watu kuwa mivutano na mauaji yanayoripotiwa nchini humo yamefika kikomo.


Trump ameongelea mambo muhimu mawili:
  • Kukoma kwa Mauaji: Trump amesema amearifiwa kuwa mauaji nchini Iran yamesimama kabisa.
  • Kuhusu Kunyongwa kwa Watu: Amesema hakuna mipango inayofahamika kwa sasa ya kuendelea kwa hukumu za vifo, akiongeza kuwa: "Tutakuja kujua ukweli baada ya muda."
Licha ya Kauli hii na bado kuna maoni tofauti juu ya hali ya kiusalama nchini Irani

Ingawa Rais Trump ameongea kwa kutumia lugha ya upole mbele ya kamera, bado makundi ya watu mbali mbali wanadai hali ya kiusalama nchini ya Iran inaashiria jambo tofauti kabisa. Wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa za kijiografia wanasema kuwa mivutano inazidi kupamba moto na hakuna ishara za kupungua kwa ukatili kama inavyodaiwa. Hii inaleta maswali mengi:

  1. Je, hii ni mbinu mpya ya kidiplomasia ya Trump?
  2. Au kuna habari ambazo umma bado haujazipata?
Kuna utofauti mkubwa kati ya maneno ya Trump na ripoti za siku ya jana na leo juu ya kile kinachoendelea kwenye mitaa ya nchi ya Iran.

Wajuvi husema muda utaongea, Ngoja tuone nini kitajiri hapo baadaye.
 
Fisi huyo anaogopa kuingia cha kike
Anajua mziki wa Ayatollah mpaka aliomuombea poo mzayuni
Asipoingia ni muoga, akiingia anaitwa mharibuji wa Amani Mashariki ya kati na katili kwa nchi Kiislamu

Wabongo hamueleweki
 
Huyu udevu kunoga akianza kubutuliwa utasikia tu "Marikani mwonevu thana" mamaqe nyie wale watu wachukulieni poa tu hivyo hivyo alafu mje mshangazwe
 
Trump naye ni mjanja mjanja tu. Kwa Maduro ilikuwa ni rahisi sana kwake kumkwapua kama mwewe. Ila baada ya kuona Iran wako vizuri kijeshi, ameona atafute visingizio dhaifu.

Awashambulie kwanza ili tuone namna watakavyo mjibu.
 
Kwani Irani ni moja ya majimbo ya USA?

Trump naye kama Luhaga Mpina ( Mbunge wa kitaifa)
 
Back
Top Bottom