Tetesi: Trump afadhaika kukatazwa kutumia simu zake

Tetesi: Trump afadhaika kukatazwa kutumia simu zake

Kama ilivyo kila wakati Rais mpya anapoingia madarakani huko Marekani hupewa masharti ya kiusalama ambayo ni LAZIMA ayazingatie.

Rais mteule Donald Trump amekatazwa na wataalamu wa kiusalama wa WHITE HOUSE kwamba hataruhusiwa kuitumia simu yake simu zake za SMARTPHONE -za Kupangusa (Android) akiwa IKULU na hata kaba hajaingia IKULU ya White House!

Badala yake ameambiwa atumie Blackberry na simu maalumu atakazo pewa na wataalamu wake wa kiusalama kama vile Obama naye alivyokatazwa na kuanza kutumia Blackberry mara tualipochaguliwa kuwa rais!

Backberry inadaiwa ni salama.Maana iko ENCRYPTED - Mawasilano yaliyovurugwa.
Mtu mwingine hawezi kuelewa mnachoongea ila ni yule tu anayepigiwa simu ndo ataelewa.
Hii ni kuzuia USIRI wa Rais Trump na Ikulu ya White.

Tukio hili limemfadhaisha sana Trump na kulalamika akisema atapoteza marafiki zake aliozoea kuongea nao.
Na unajua Marekani watu wa usalama wa Rais -SECRET SERVICE nk ndo walio na usemi wa mwisho kuhusu usalama wake

Swali Trump atawezaje mambo ya utawala na biashara zake bila simu zake hizo?
Maana amehuzunika sana!
Ameshasema biashara zake atawaachia watoto wake "to avoid any possible conflict of interest."

Hii itakuwa muhimu kwake kwa kuwa ana kesi nyingi za kibiashara mahakamani.Majuzi tu amelazimika kulipa US$25 million kwa wanafunzi ambao aliwa-enroll kwenye chuo chake kikuu hewa!Huwezi amini, hata Marekani kuna vyuo vikuu hewa,tena cha President Elect wa Marekani.
 
Alikuwa hajajiandaaa
Laiti angejua asingegombea.
Mzushi haya majamaa hivi unawezaje kuomba nafasi ya kazi usiejua hata life style ya kazi hiyo??
Anajuta eeeh!!!
Aombewe sana na yeye

Haha, jamani ajute tena kuukwaa Urais. 🙂
 
Ni sawa mkuu, ila kwa Mungu ni hapana usimweke yeye ni wa kipekee haitaji ulinzi wa kibinadamu.
Mkuu Miungu ipo mingi inategemea tu yeye kamkusudia Mungu yupi maana hata Ng'ombe na sanami ni Mungu kwa imani zingine na anahitaji ulinzi.
 
hapa kwetu zinatumika zipi?
tecno?
htc?

lumia?
blacbrry?

ttcl?

au za tochi.....
 
Linapokuja suala la usalama, haijalishibwewe ni Rais au Mungu.
Lazima ufuate masharti.

Hii ndio marekani, nchi yenye misingi.

Hata Tanzania tuna na misingi mizuri tu iliyodumu miaka mingi sana. Kama haipo sasa tujiulize ilienda wapi? Ilipoteaje? Ujamaa ni utu; Binadamu wote ni sawa; Kila mtu anastahili heshima; elimu ya kujitegemea; uhuru na umoja; maendeleo ya nchi huletwa na watu, siasa safi na uongozi bora; cheo ni dhamana nitakitumia cheo changu kwa faida ya wote; fitina kwangu mwiko; kila mtu anahitaji maji safi, malazi bora na chakula bora; rushwa ni adui ya haki; nchi hujengwa na wenye moyo; adui wa watu ni maradhi, ujinga na umaskini...................Haya ndio tulifundishwa katika miaka ya sitini katika somo la uraia.
 
Cha kuongezea hapo ni kwamba ule uswahiba wake na Putin umeisha kwa sasa, yupo White House kuserve interests za America na sio zake tena
 
Nakumbuka Obama naye alilalamika sana. Alisema anakatzwa kila kitu na kubadirishiwa kila kitu, na kwamba ni kama amekatazwa maisha aliyoyazoea na watu aliozea kuwasiliana nao. Na kuna siku alitaka kutumia simu tofauti jama wa secrete service alimnyang'anya mbele ya watu.
Ukimfanyia ivyo sizonje kesho yake anakutumbua
 
Ukimfanyia ivyo sizonje kesho yake anakutumbua
Mmmmh hiyo kunyang'anywa simu mbele za watu umetunga tu na pamoja na usalama wa rais lakini anakuwa na mambo yake binafsi na kwa marekan rais anaruhusiwa kuchagua mtu yeyote wa karibu yake,anaitwa first officer kama sikosei.
 
Sijasema mm likin
 
Tutamiss post zake nyingi zenye utata maana atofanya kama alivyokuwa anafanya kwenye Twitter na Facebook kabla hajapata Urais ..
Asee nimemfollow twitter ilikuwa nafurahia post zake hahaha
Ntazimiss
Naenda ku mfollow kwenye account ya POTUS sikubali.
 
Acha kupotosha wewe, rudi kasome chanzo cha yeye kulipa faini alafu irudi tena

Ameshasema biashara zake atawaachia watoto wake "to avoid any possible conflict of interest."

Hii itakuwa muhimu kwake kwa kuwa ana kesi nyingi za kibiashara mahakamani.Majuzi tu amelazimika kulipa US$25 million kwa wanafunzi ambao aliwa-enroll kwenye chuo chake kikuu hewa!Huwezi amini, hata Marekani kuna vyuo vikuu hewa,tena cha President Elect wa Marekani.
 
Mmmmh hiyo kunyang'anywa simu mbele za watu umetunga tu na pamoja na usalama wa rais lakini anakuwa na mambo yake binafsi na kwa marekan rais anaruhusiwa kuchagua mtu yeyote wa karibu yake,anaitwa first officer kama sikosei.
Hiyo kauli ilitolewa na Obama mwenyewe, kwamba alinyang'anywa simu mbele ya other officers alipotaka kuitumia. Yeye alikabidhiwa simu ya kutumia na akaelezwa kwamba atakua akitumia simu hiyo kuanzia siku hiyo. Alipotaka kufanya mawasiliano na marafiki zake, akaamua kuchukua katia ya simu zake binafsi ndipo akanyang'anywa mbele ya maofisa wa Ikulu. Sasa kama Obama alidanganya, hilo ni suala lingine.
 
Back
Top Bottom