The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Rais wa Marekani Donald Trump amejibu ripoti kuhusu tathmini iliyovuja ya kijasusi juu ya shambulizi la Marekani dhidi ya Iran.
Akichapisha ujumbe kwenye jukwaa la Truth Social, Trump alivisuta vyombo vya habari vya Marekani na taarifa zao.
"TAARIFA ZA UWONGO CNN, PAMOJA NA NEW YORK TIMES ILIYOSHINDWA, WAMESHIRIKIANA KATIKA JARIBIO LA KUDHALILISHA MOJA KATI YA MASHAMBULIO YA KIJESHI YALIYOFANIKIWA SANA KATIKA HISTORIA. MAENEO YA NYUKLIA NCHINI IRAN YAMEANGAMIZWA KABISA! TIMES AND CNN ZOTE ZINAZOMEWA NA UMMA!"
Utawala wa Trump umeendelea kupinga ripoti inayosema kuwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran hayakumaliza mpango wake wa nyuklia.
Wakati huo huo, mjumbe maalum wa Trump katika Mashariki ya Kati Steve Witkoff ameita tathmini ya kijasusi iliyovuja kuhusu shambulizi la Marekani dhidi ya Iran kuwa "uhaini".
"Ni jambo la kuchukiza, ni uhaini na ni lazima uchunguzi ufanyike. Yeyote anayehusika nayo anapaswa kuwajibika," aliiambia Fox News.
Aliongeza kuwa amesoma ripoti zote za tathmini ya uharibifu, akisema "hakuna shaka" kwamba maeneo yote matatu ya nyuklia ambayo Marekani ilishambulia "yaliharibiwa kabisa