Trump akerwa kunyimwa Tuzo ya Amani ya Nobel, asema tuzo hiyo imepoteza hadhi yake

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ameelezea kutoridhishwa kwake na uamuzi wa Kamati ya Nobel kutomtunuku Tuzo ya Amani ya Nobel, akielezea uteuzi wa mwaka huu kuwa "aibu na fedheha".

Kamati hiyo ilimtangaza jaji wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, Navi Pillay, kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel jana Oktoba 09, 2026 hata hivyo, saa chache baada ya tangazo hilo, Trump aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara kwamba hajawahi kumsikia mshindi huyo.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika mjini Syracuse, New York, Trump alisema uamuzi huo ni doa kwa Norway na akaonya kwamba hatua hiyo haitasahaulika kirahisi.

Rais huyo amekuwa akieleza mara kwa mara kwamba anaamini anastahili kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel. Hii si mara ya kwanza kulalamikia uamuzi wa kamati hiyo, kwani mwaka 2025 pia alikosoa tuzo hiyo baada ya kutolewa kwa kiongozi wa upinzani wa Venezuela, María Corina Machado.

Mwaka jana, Waziri Mkuu wa Norway, Jonas Gahr Støre, alimkumbusha Trump kwamba mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel huchaguliwa na kamati huru ya Nobel yenye makao yake nchini Norway, na sio serikali ya nchi hiyo.

Katika hotuba yake, Trump alirudia madai kwamba alisaidia kumaliza vita nane na alikuwa karibu kusuluhisha migogoro mingine miwili, ingawa hakutoa ushahidi wa kuthibitisha kauli hizo.

"Tuzo ya Amani ya Nobel imepoteza hadhi yake kutokana na kundi dogo la watu wenye misimamo mikali wanaopinga demokrasia na ambao, kwa mtazamo wangu, ni maadui wa ustaarabu," alisema Trump.
 
Kwanza iko wapi ile bodi yake ta Amani ?. Hastaili kabisa iyo tuzo huyo mzee
 
Mzee anaitamani Nobel kweli kweli...😃😃😃.

Kichuguu
 
Mie mwenyewe nilitakiwa nipate tuzo ya uchumi ya Nobel kwa sera za fedha nilizozianzisha tangu mwaka 2016, ambazo zinatumika mpaka leo Duniani, lakini kwa kuwa ni muafrika, mweusi niliwekwa pembeni na yale niliyoyatunga, ingawa yanaendesha Dunia kwa mwaka wa kumi sasa, walisema yalitungwa na Mmarekani mwenzao.
Mimi niliwaambia haina noma, lengo langu halikuwa kujipatia jina kubwa hapa Duniani. Ingekuwa hivyo nisingefanya hayo kwa majina ya kubuni.
Lengo langu ilikuwa ni kusaidia vizazi vya sasa na vya baadae katika mambo yanayowatatiza, ili baadaye wasije kusema profesa Bemendazole, pamoja na kusoma vitabu vingi, umeshindwa kuisaidia Dunia !
 
Back
Top Bottom