Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Huu ni kama mchezo mgumu wa drafti unaochezwa kwa viwango vya juu sana.
Hii ni kwenye mahojiano na Waandishi siku ya jana ambapo Rais Donald Trump alikiri kuwa changamoto ya kuishughulikia Iran sio rahisi kama wengi wanavyodhani kwani yupo kwenye hali inayomfanya ashindane na watu anaodai;
Trump analejerea ugumu wa vita ya Iran kwa hapo ilipofikia. Ni wazi Rais Trump matarajio yake yalikuwa kuiona Iran ikisalimu amri ndani ya siku chache tu baada ya vita kuanza, matarajio hayo yalijikita kwa kufanikisha malengo makubwa ikiwemo kuangamiza uongozi wote wa juu.Ni wachezaji waerevu sana. Hawa ni watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria. Vingenevyo wasingeweza kufika hapo walipo.
Kutokea kwa kizazi kipya chenye msimamo ule ule wa kile kilichoondoka kumefanya vita ya Iran ichukue sura mpya.
- Nani ataanza kumfuata mwenzake na kumtaka wakae mezani kwa mazungumzo na atampata vipi?
- Makubaliano yatakuwa yapi?
- Je, Iran itakubali kuacha mpango wake wa Nyuklia?