Mimi binafsi kwenye jambo lolote la kitaifa siweki udini au uchama.
Kiongozi akifanya vizuri nitampa pongezi zake lakini siwezi kugeuka kuwa mtumwa wa mtu. Never
Sitakuwa mtumwa wa mwanasiasa yeyote mpaka nitakufa.
Tulipiga kelele humu inakuwaje mtu unamsifia Rais huku mpaka vyoo vya shule vinajengwa kwa pesa za msaada ?
Bajeti yetu tunayosomewa na akina Mwigulu ni bajeti hewa, maana unapanga bajeti huku pesa huna. Ikitokea jambo la kutikisa Dunia bajeti inafail kwa 80%.
Tuna rasilimali nyingi hata kuzitaja naona uvivu lakini serikali ya CCM ambayo Watanzania wachache wamejitoa akili kuisifia kila asubuhi, mchana, jioni na usiku imeshindwa kuzitumia badala yake nchi inaishi kwa misaada.
Hii miezi 3 ya mapitio ya misaada ya Marekani ni pigo kubwa sana kwa wananchi mafukara maana ndio waathirika wakubwa.
Huenda hali ya maisha ya Watanzania ikabadilika zaidi na kuwa duni maana Trump ni kama amechomoa betri bila taarifa.