Salaam, Shalom,
Akisubiri kuapishwa, Rais Mteule Donald Trump ameapa kuirudisha tena BIBLIA Marekani, amedai BIBLIA na wahubiri walikuwa wakitishwa kuhubiri au kusoma BIBLIA hadharani, jambo hili lilichangia kuharibu Maadili ya watu wa Marekani.
Huyu ni Rais wa Nchi aliyechaguliwa kuongoza Nchi na makundi yote, wenye dini na wasio na Dini, lakini Yeye hakujikita katika Dini Bali katika kuwafanya watu kumwamini Mungu aliyeandikwa ndani ya BIBLIA.
Je ingekuwa jambo hili amesema kiongozi mkuu Nchi ya maziwa makuu, jambo hili lisingetafsiriwa kama kuchanganya dini na siasa?
Mungu ibariki Marekani,
Mungu Mbariki D. Trump,
Mungu ibariki BIBLIA ( Neno lako).
Ameen
Karibuni 🙏
PIA SOMA
-
Trump atoa biblia yake. Ina bendera na katiba ya US pamoja na mwimbaji ampendae