Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,335
- 1,967
Salaam wakuu.
Rais Donld trump wa marekani yupo kasi sana,anaunadi ukubwa wa taifa lake,anatamani kuwa na mamlaka mbele ya wenye mamlaka wenzie na anatumia nguvu na hadaa kuwaongoza viongozi wa mataifa mengine kufuata maono yake!
Kabla mzozo wake na rais Zele wa ukreine haujapoa tayati ameshadai kuwasiliana na kiongozi mkuu wa Iran Imam khomenei,madai ambayo yamekanushwa na utawala wa Iran.
Siku chache baada ya kuhitalifiana na Rais wa Ukreine akatangaza kuwa wasaidizi wake watakutana na wawakilishi wa Rais Putin wa Urusi huko Saudi arabia,tayari rais Zele kishatangulia Saudia,waziri wa mambo ya nje wa Marekani na mshauri wa masuala ya kiusalama wa rais Trump wapo hewani wanaelekea Saudia, chakushtua nikwamba Urusi imekana kuwa na taarifa za mkutano huo,kwahiyo hawatahudhuria.
Hii imeekaaje!?
Nakumbuka wiki iliyopita kiongozi Muadham wa taifa kubwa la Iran Sayid Al khomenei akiwahutubu Wairan aliiwaambia"mazungumzo na Marekani sio jambo lakujivunia,si jambo la heshima bali ni kujidhalilisha na kujidunisha na kwamba taifa la Iran halina mpango wowote wakufanya mazungumzo na Marekani mpaka pale watakapoondoa vikwazo vyao na kuacha kuitishia Iran.
Kwa khutba hiyo napata hisia kuwa huenda hata Putin na viongozi wenzie wa Urusi wamewaidhika na kuamua kula kona,kuchukua tahadhari dhidi ya Trump na viongozi wenzie wasioaminika wa Marekani.