Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Rais Trump ameendeleza ubabe na kuendelea kupunguza mahusiano ya Marekani na mataifa mbalimbali:
Marekani, chini ya Trump, kwa muda mfupi imejenga mazingira ya kupunguza mashirikiano dhidi ya mataifa ya Ulaya, Asia, America na Afrika.
1. Kwa Afrika, Trump amefuta misaada.
2. Kwa Ulaya, Trump amejiondoa kuisaidia Ukraine kwenye vita yake dhidi ya Mvamizi Russia.
3. Kwa Asia, Trump aliongeza kodi kwa 10% kwa bidhaa zote toka China, na sasa ameongeza tena 10%; kwa hiyo ni ongezeko la 20%. China imesema ipo tayari kujadiliana na USA kuhusu kodi, lakini haitakubali kuburuzwa. Trump pia ameionya Japan kuwa inashusha thamani yake ya fedha, na hiyo inasababisha bidhaa za Marekani kuonekana aghali sana. Japan imekataa kuwa huwa haishushi thamani ya pesa yake.
4. Kwa America, ameweka kodi ya 25% ya bidhaa kutoka Canada na Mexico. Canada imesema na yenyewe italipiza kisasi.
5. Kwa Dunia, Trump ameiondoa USA kwenye uwanachama wa WHO, anafikiria kuiondoa USA kwenye Umoja wa mataifa na taasisi zake zote.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuna dalili ya Trump na Putin kutengeneza umoja wao. Lengo ni kuifanya Dunia nzima kuwa chini ya mataifa haya yenye nguvu za kijeshi, Marekani na Russia.
Dunia ijiandae kwa mpangilio huu mpya wa Dunia unaoweza kutokea ambao utakuwa wa block ya mataifa makubwa mawili ya Dunia, dhidi ya China na mataifa madogo madogo.