Trump asaini sheria inayolenga Kuibana Mitandao Ya Kijamii Ikiwemo Twitter, Facebook na Youtube

Trump asaini sheria inayolenga Kuibana Mitandao Ya Kijamii Ikiwemo Twitter, Facebook na Youtube

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729
1590744049415.png


Rais Donald Trump wa Marekani jana Alhamisi alisaini Amri ya Utendaji (Executive Order on Preventing Online Censorship) inayolenga kuongeza uwezo wa serikali kusimamia na kuibana mitandao ya kijamii. Amri hiyo inalenga kampuni zilizopewa ulinzi wa kisheria kupitia kifungu cha 230 cha Sheria ya mawasiliano ya staha (Communications Decency Act).

Kwa mujibu wa kifungu hicho, kampuni kubwa za mitandao ya kijamii hazitashitakiwa kutokana na maudhui yaliyowekwa na watumiaji kwenye tovuti zao lakini zinaweza kuhusika kwa upande wa usamaria mwema wa kuondoa maudhui hayo mtandaoni ambayo labda yana maudhui ya unyanyasaji, chuki na yanaaibisha

Amri hiyo imekuja siku mbili baada ya mtandao wa kijamii wa Twitter, kwa mara ya kwanza, kuweka alama ya onyo kwenye jumbe mbili alizoandika rais Trump kwenye ukurasa wake, inayowashauri wasomaji "kuhakiki ukweli wa taarifa hizo".

Twitter ilichukua hatua hiyo ambayo haraka ilichochea mvutano kati yake na Trump, baada ya rais huyo wa Marekani kuandika Tweet mbili akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta huwa una udanganyifu mwingi. Ilichofanya Twitter ni kuweka kiungo kingine chini ya ujumbe wa Trump kinachosema "Pata taarifa za ukweli juu ya kura ya njia ya posta,” na baadae kiungo hicho kinampeleka mtumiaji kwenye makala ya habari inayompa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo, na orodha ya maelezo yanayopinga madai ya Trump.
 
Sheria hiyo inawapa watu uhuru wa kutoa maoni yao mtandaoni bila censorship.
 
Sheria hio haibani Bali inawapa wana nchi Uhuru wa kutoa maoni yao, hapo juzi twitter wali edit post ya Trump utafikiri wao ndio waliopost na CEO wa Facebook nae aliungana na mawazo ya Trump na wengi duniani kwamba huu ni udikteta wa free speech.

Trump 2020
 
Trump kuna kitu anafanya kwenye hii sheria, watu hawajui.
Lazima itakua kuna MABADILIKO mengi zaidi ya haya.
Waweke wazi MABADILIKO hayo ya sheria, itakua vyema
 
Sheria hio haibani Bali inawapa wana nchi Uhuru wa kutoa maoni yao, hapo juzi twitter wali edit post ya trump utafikiri wao ndio waliopost na CEO wa Facebook nae aliungana na mawazo ya trump na wengi duniani kwamba huu ni udikteta wa free speech.

Trump 2020

Huo ndio uongo wenyewe twitter wali add caption ya kusema wasomaji wa-verify the info ambayo Trumpet aliandika ambayo haikuwa facts.
 
Watanzania wengi hawajui kua hiyo sheria inasaidia Raia waandike wapendacho bila kufutwa
 
Huo ndio uongo wenyewe twitter wali add caption ya kusema wasomaji wa-verify the info ambayo Trumpet aliandika ambayo haikuwa facts.
Kwa hio twitter wameacha misleading information za Russian hoax ndio wameona waanza huu ujinga??
 
Trump anaiga sheria yetu ya 2016, Tz imekuwa kiigizo chema cha Mabeberu recently
 
Sheria inawapa Uhuru watumishi wa mitandao, kitu ambacho jiwe na serekali yake wangefanya kinyume ingewanyima Uhuru watumishi Kama ilivyofanya kwa Idris
 
Back
Top Bottom