The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
kwamba atajaribu kurejesha baadhi ya maeneo ya Ukraine wakati wa mkutano wake na Rais wa Urusi Vladimir Putin Ijumaa ijayo.
"Urusi imechukua sehemu kubwa ya Ukraine. Wamechukua eneo muhimu. Tutajaribu kurudisha baadhi ya eneo hilo kwa Ukraine," alisema katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu ya White House.
Trump na rais wa Urusi wameratibiwa kufanya mazungumzo huko Alaska wikendi hii. Trump amesema atajua ndani ya dakika mbili za mkutano wake na Putin ikiwa maendeleo yanaweza kupatikana.
Trump alielezea mkutano wa Ijumaa kama "mkutano wa uchunguzi" unaolenga kumtaka Putin kumaliza vita, akionyesha kwamba anauona mkutano huo kama mkutano wa awali tu.
Trump alionya tena kwamba kutakuwa na "mabadilishano na mabadiliko ya eneo" kati ya Urusi na Ukraine.
Hii si mara ya kwanza kwa rais wa Marekani kutumia neno "kubadilishana maeneo," ingawa bado haijafahamika ni eneo gani ambalo Urusi inaweza kukabidhi kwa Ukraine, hasa kwa vile Kyiv haijawahi kudai eneo lolote la Urusi