Jackson94
JF-Expert Member
- Sep 14, 2016
- 492
- 560
Trump amesema anafikiria wagombea wote wa urais wanapaswa kupewa mtihani wa uelewa, huku akisisitiza kwamba yuko sawa kiafya ya akili na muafaka kuingia madarakani.
Akimzungumzia Kamala Harris huko Pennsylvania, alisema: "Sina tatizo la uelewa – lakini yeye anaweza kuwa na tatizo hilo."
Trump mwenye umri wa miaka 78 aliambia ukumbi wa jiji la Lancaster: "Kwa kweli natoa wito wa mtihani wa uelewa kwa watu wote wanaotaka kugombea urais. Sio kulingana na umri. Sina miaka 80, na siko karibu miaka ya 80. Upande wa Biden, ana miaka 81 au 82, na unajua, hiyo inaeleweka".
Trump aliendelea: "Tumekuwa na baadhi ya viongozi bora katika historia ya dunia ambao wako katika miaka ya 80. Nimefanya mtihani mara mbili na niliwashinda wote wawili. Daktari wakati mmoja alisema, 'Sijawahi kuona mtu bora kama wewe."
Trump anasema aliambiwa mtihani wa lazima wa afya ya akili utakuwa kinyume na katiba.
Kampeni ya Harris imerudia kutilia shaka afya ya kiakili ya Trump na kumkosoa kwa kukataa kutoa rekodi zake za matibabu.