Trump asema magonjwa ya akili yanayosababishwa na msongo wa mawazo kwa amri ya kutotoka nje yameongezeka Marekani

Trump asema magonjwa ya akili yanayosababishwa na msongo wa mawazo kwa amri ya kutotoka nje yameongezeka Marekani

Kumbe Mbowe alitaka tuugue magonjwa ya akili ili waendelee kutudanganya

Sent using Jamii Forums mobile app
Dhihaka zitakapoisha, pengine hata Mungu anaweza akaingilia Kati janga hili

Ukitaka kujua kwamba Tanzania ni nchi ya hatari sana, ni pale ambapo Giza la mauti limetanda nchi nzima halafu watu wake bado wakiendekeza Ujinga Ujinga wa siasa zisizo saidia katika Giza Hilo mauti,

Ikifikia hatua ya Giza la mauti kutamalaki, kila mmoja akiomboleza, labda hapa Mungu atatukuzwa!!

Mungu wa Rehema, Irehemu Nchi yetu na Dunia Kwa ujumla, maana hatujui kama kesho itakuwa salama

Fuata maelekezo Yote yanayotolewa na serikali ili kuzuia Jamii yako na wewe mwenyewe kuambukizwa na Corona,
 
Kwa sasa Corona inasambaa kama moto wa msituni hivi tunavyo ongea Cirona inaelekea Vijijini

Labda mkakati wetu uwe Herd immunity Magufuli ameonyesha udhaifu wa ajabu katika hili wala hagai kupewa muhula wa pili
 
Haihitaji bunduki inahitaji akili ndicho anachofanya JPM anatumia akili nying kuliko nguvu
Umeelewa mantiki ya SWALI?? Au kwasababu tu umewaza ulivyoelewa?? Kamanda wa Vita hawezi kutoa maagizo akiwa ndani wakati watu wako kwenye mpambano. Sio Kila ukiona neno Vita unajua kunahitajika bunduki!!! Bunduki zinaweza kuwa washauri wako/ nation think tank wako wapi katika hi vita??
 
Kwa sasa Corona inasambaa kama moto wa msituni hivi tunavyo ongea Cirona inaelekea Vijijini

Labda mkakati wetu uwe Herd immunity Magufuli ameonyesha udhaifu wa ajabu katika hili wala hagai kupewa muhula wa pili
Ulitakaje ww awafungie watu wamekuwa kuku wa kideri? Acheni umagharibi wenu
 
Ulitakaje ww awafungie watu wamekuwa kuku wa kideri? Acheni umagharibi wenu
Huu mkakati wa Magufuli dhidi ya Corona ni "Do nothing" ambao huenda ukatusaidia

Mkakati wa pili ni "Hide in Chato bunker" huu pia sio mkakati mbaya huenda pia ukalisaidia Taifa

Naona kama tuko kwenye win win
 
Ni upumb.avu wa hali ya juu kuleta mada za kishabiki wakati huu.

Kwa mtu mwenye akili, anajua kuwa mpaka sasa hakuma mwenye uhakika ni njia ipi iliyo sahihi kupambana na ugonjwa huu. Ukiona mtu analeta mada kama hizi, unashindwa kuelewa kama ni mzima au amepungukiwa kichwani.

Wakati huu siyo wa kufanya ushabiki wowote ule, hasa kwa suala hili la ugonjwa wa corona. Kama kungekuwa na njia iliyo wazi na sahihi ya kupambana na ugonjwa huu, Dunia nzima ingeiga, na hakuna ambaye angeangamia. Kwa sasa hakuna njia hata moja iliyoonekana ni efficient kwa 100%. Ni mwendawazimu tu anayeweza kumsifia yeyote yule nyakati hizi wakati hakuna mahali walipofanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu kwa 100% perfection.

Nadhami ambaye atastahili pongezi ya pekee ni yule atakayewezesha chanjo kupatikana.
Usisahau kwa kiduku hakuna mgonjwa hata mmoja mpka sasa.na wakati hio huo majirani zake wanagaragazwa vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa njia ya kujifungia na kutokujifungia bado hazijaleta unafuu wa kuwa ndiyo njia ya kupunguza maambukizi ya Corona,

Hii ya kujifungia inanikumbusha Stori moja hivi ya wakoma, hawa watu walikimbia mjini na kwenda kujificha kuskojulikana Kwa sababu mjini mlikuwa na vita Kali Sana,

Wakoma hawa wakakaa huko ktk maisha ya dhiki kubwa, hapakuwa na chakula, mizizi na majani ndiyo ilikuwa ni chakula Chao huko

Siku moja walipoona njaa imewazidi Sana na miili Yao kuchoka taabani, wakakaa kushauriana, Jambo moja wakakubaliana kwamba, iwe mvua ama jua ni lazima twende mjini, mjini wakituu na watuuwe, maana hata tukibaki hapa bado tutakufa, mjini Kuna chakula, ya nini kubaki hapa tufe tunajiona?

Wakoma wakaamua Jambo moja, tunakwenda mjini ili kama ni kufa, tufe, kama tukibaki tutamshukuru Mungu,

Kumbe buana wale jamaa, katika tembea Yao Ile, Mungu aliweka mshindo mkubwa katika miguu Yao, kishindo kilichokuwa kinasikika ni kikubwa kiasi kwamba watu walio kilomita 10 Mbele, wanakisikia,

Watu wa mjini waliposkia hicho kishindo, walikimbia wakaacha kila kitu, silaha waluacha, madufulia ya chakula n.k

Basi ikawa ndiyo pona Yao hao jamaa,

Nataka kusemaje, Serikari zetu hizi zinazojaribu kujenga nchi zao ni za kiumaskini, kama serikali za nchi tajiri wanahofia uchumi Wao kuwafungia watu, hapa kwetu wakijaribu kufanya hivyo, Shure, nakwambia, ni Baada ya siku chache Tu, mfano wa watu wakoma watajitokeza, wataamua moja, ama kufa, ama kuishi, mtu huwezi kaa na njaa kisa eti nje kuna corona, wajaribu waone, kuna watakao kufa Kwa sababu watapigwa eiza na police ama watu watakaokuwa wakilinda watu wastoke Nje

Hili janga salama yake, ni mtu ujikabidhi Kwa Mungu, ili ukifa iwe faida
Agiza kinywaji bro chahalali nalipia kwa jamiiforum pesa.

Sent using My COVID-19
 
Back
Top Bottom